Dk. Lwaitama ahoji, kama Lissu anasema hataki maridhiano, je anataka kuchukua silaha kupambana na serikali? Asisitiza umuhimu wa mazungumzo ya vyama

Lissu anataka kuigiza watu mstituni kidai Katiba...CDM kuweni makini.

Huwezi kudai katiba mpya bila kumshirikisha mkuu wa dola, mwambieni Lissu hapa siyo Somalia.
 
Mdo maana jamaa yenu anakwenda kukwama asbh tu.
 
Yote sawa ila#£ mbowe must go
 
Hayo unayosema yamekubaliwa siyo maridhiano bali hayo ni haki yao ya kikatiba ni kwa vile tu yule mwendawazimu aliyaweka kibabe.
Na nani alikuwa na ubavu wa kumlazimisha Rais azingatie hizo unazoita haki yao ya kikatiba? Tupende tusipende ulikuwa ni uamuzi wa Rais peke yake na moja ya mapungufu ya Katiba yetu inampa haki ya kuikiuka bila kuzuiwa na mtu yeyote. Mbowe alijua hilo.
Maridhiano katika maeneo hayo hayakufikiwa. Hapa tena msimamo wa Lissu ilikuwa chama chake kisishiriki mpaka Tume Huru ipatikane. Unadhani CDM wasingeshiriki wangekosekana wapinzani wa kushiriki? Unaona Chaumma wamejipatia ushindi kwa mara ya kwanza. Kushiriki kwa CDM umeweka wazi namna mfumo uliopo hauwezi kutoa matokeo ya haki. Matokeo yale yanaipa CDM nguvu katika madai yao ya Tume Huru ya Uchaguzi. Na hata kama watagombea serikali itahakikisha kuwa angalau matokeo yawe yana uhalisia. Sidhani kama ushindi wa 99% ya vitu vya ubunge utarudiwa tena.

CDM ingefuata msimamo wa Lissu ( ambae hakujisumbua kujiandikisha kupiga kura. Kama nakumbuka vizuri hakufanya hata kampeni ya maana) wangekosa huo ushahidi na CCM wangesema kuwa wangeshindana wangeweza kushinda. Kama Chaumma wameshinda itakuwa CDM? Aidha, CDM na wapinzani wengine wana nafasi ya kujipanga vizuri kwa sababu wanajua hamna lililobadilika. CDM hawezi kubeba lawama ya watu wake kutotendewa haki.

Amandla...
 

..Tundu Lissu aliunga mkono maridhiano mpaka pale alipojiridhisha kwamba CCM hawana nia njema ndipo alipoyapinga.

..Kuachiwa kwa Mbowe, kufutwa kwa kesi za kubambikiwa, mahabusu 400+ kufunguliwa, wakimbizi kuhakikishiwa ulinzi, zilikuwa PRE-CONDITIONS za kuanza mazungumzo, na sio madai au dondoo za maridhiano.

..According to Lissu, maridhiano yalikuwa yanahusisha kufumuliwa na kuundwa upya kwa mifumo na taratibu zetu za uchaguzi, na kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.

..Mwenyekiti Mbowe alikuwa mgumu kidogo kubaini na kujitokeza kueleza kwamba maridhiano yamefeli, lakini na yeye baadae alijitokeza na kuungana na kauli kwamba maridhiano yalifeli.
 
Mbona sasa katiba mpya haipatikani na ni haki ?

Unadhani katiba,mpya ni sawa na kwenda haja kubwa chooni?

Key boards warriors mnashangaza sana.

Sijui umeelewa kilichoandikwa.
Kimsingi hakuna mahala niliposema nataka katiba mpya, bali nimeshangaa kuona watu wanataka maridhiano kwa masuala ambayo yapo kikatiba na sio favour.

Uwe na siku njema, lakini Mwenyezi akubariki pia nakukupa hekima na busara za kutosha pamoja na kuibariki familia yako ndugu yangu.
 
..Tundu Lissu aliunga mkono maridhiano mpaka pale alipojiridhisha kwamba CCM hawana nia njema ndipo alipoyapinga.
Lakini hii sio narrative ambayo inasambaa. Kinachosambaa ni kuwa aliistukia toka Mbowe alipoipendekeza kwa mara ya kwanza. Kuwa yeye na wenzake wanne walimkatalia na ndio maana Mbowe amewashughulikia kutokana msimamo wao( Aliyepona ni Wenje peke yake kwa sababu zilizo wazi). Ndio maana watu wanadai kuwa mazungumzo yale hayakuwa na faida yeyote. Kitu ambacho ni uongo. Na Lissu anajua hilo.
..Kuachiwa kwa Mbowe, kufutwa kwa kesi za kubambikiwa, mahabusu 400+ kufunguliwa, wakimbizi kuhakikishiwa ulinzi, zilikuwa PRE-CONDITIONS za kuanza mazungumzo, na sio madai au dondoo za maridhiano.
Kwa hiyo mazungumzo yalianza kabla Mbowe hajaachiwa? Wakati huo Boss si alikuwa Lissu? Sasa mbona watu wanadai yalianza baada ya Mbowe kulambishwa asali alipoenda Ikulu mara baada ya kutoka gerezani? Na kama yalikuwa ni pre-condition tu kwa nini Mbowe abebeshwe shutma za usaliti?
..According to Lissu, maridhiano yalikuwa yanahusisha kufumuliwa na kuundwa upya kwa mifumo na taratibu zetu za uchaguzi, na kuendeleza mchakato wa Katiba mpya.
Nae ni lazima alijua ugumu wa CCM kukubali hilo. Kuna wakati zilikuwa zinatoka taarifa zisizo rasmi zikielezea jinsi Kinana anavyokuwa na wakati mgumu kushawishi wengine.
..Mwenyekiti Mbowe alikuwa mgumu kidogo kubaini na kujitokeza kueleza kwamba maridhiano yamefeli, lakini na yeye baadae alijitokeza na kuungana na kauli kwamba maridhiano yalifeli.
Ni kweli unalosema. Lakini yeye kuendelea na mazungumzo kulionyesha kuwa walishiriki in good faith kuliko wenzao. Kinachonishangaza ni watu kuongea kama vile mazungumzo hayo bado yana endelea. Na Lissu haisahihishi hiyo imani.

Amandla...
 
Kinachokera wengi ni Mbowe kusifia maridhiano, na hata kuonyesha maridhiano yalikua na manufaa makubwa, haliyakua watu wazima wote tunaona.
 
Mikutano ya hadhara ilizuiwa wakati ipo kikatiba na kisheria mbona Lissu hakufanya wakati ilipozuiwa?
 
Maridhiano yamepelekea ccm kushinda 99% uchaguzi serikali za mitaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…