Dkt. Abbas: Dira ya maendeleo ya 2025 haina sehemu inayoonyesha pato la Nchi kuingia Uchumi wa Kati. WB ndio yenye vigezo vyake

Dkt. Abbas: Dira ya maendeleo ya 2025 haina sehemu inayoonyesha pato la Nchi kuingia Uchumi wa Kati. WB ndio yenye vigezo vyake

Watu waovu hawajifichi

JK mtu muungwana kabisa

Jk amesema kwenye mpangilio
1. Kuingia uchumi wa kati by 2025
2. Pia katika safari, by 2025 basi walau kipato kifikie usd 3500

Huu ni mpango wa kimaendeleo Tanzania...(DIRA) By 2025.

Sasa huyu anayeleta world bank ametokea wapi? Iwapo JK aliongelea dira yetu watanzania?
Waliosema tumeingia uchumi wa Kati world Bank , sio kwa Kauli yako au mtu Mwingine
 
Nadhani wewe ndo hujaelewa nilichoandika soma upya tena!
Ndiyo maana nime-quote..
Alimaanisha GNI ya sasa inatuweka kwenye uchumi wa kati according to World Bank. Na tumefikia hatua hiyo kabla ya 2025.
 
Watu waovu hawajifichi

JK mtu muungwana kabisa

Jk amesema kwenye mpangilio
1. Kuingia uchumi wa kati by 2025
2. Pia katika safari, by 2025 basi walau kipato kifikie usd 3500

Huu ni mpango wa kimaendeleo Tanzania...(DIRA) By 2025.

Sasa huyu anayeleta world bank ametokea wapi? Iwapo JK aliongelea dira yetu watanzania?
Uwe unaelewa bwashee...... Hiyo $ 3500 umeitoa wapi?
 
Kuna mtu kakurupuka vibaya

JK alisema mzee mkapa alikuwa na matamanio ya kufikia uchumi wa kati kwa per capita kuwa USD 3000 hata kama tunajua kwamba uchumi wa kati ungetuhitaji kuwa na per capital around 1080.

Yaani ni sawa sawa na mtu uwe na matamanio ya kufaulu chuo na First Class badala ya ule ufaulu wa kawaida wa wengi wa Lower second.

Itakuwa maneno ya Kikwete yamewachoma sana
Wameshajua 2025 uwezekano wa kufikia hio $3,000 haupo na hautakuwepo imebidi waanze kupiga propaganda mapema sana.

JK amemwaga mafuta ya taa shimoni sasa nyoka wameanza kujitokeza wakihaha.
 
Siku hizi ile methali inayosema muungwana akivuliwa nguo huchutama imebadilika.
Sasa muungwana akivuliwa nguo hukimbia kutafuta nguo nyingine, maana anaweza kuchutama muda mrefu bila msaada.
Tuache kwanza mkuu
 
sasa yeye kama nani anabishana na JK? walioasisi hiyo vission 2025 (JK na BWM) wao waliweka target ya usd 3000 mpaka nchi itakapofikia middle economy. Abbas acha kujidharirisha.
Ameongea kama serikali na kama mtaalamu wa uchumi!
 
Ndiyo maana nime-quote..
Alimaanisha GNI ya sasa inatuweka kwenye uchumi wa kati according to World Bank. Na tumefikia hatua hiyo kabla ya 2025.
JK alieleweka sana! JK alisema lengo lao lilikua by 2025 tuwe kwenye uchumi wa kati ambapo tufikie pato la $3000

Na akamtakia heri Magufuli kufikia hapo sasa shida ni nini?

Tafsiri ni kuwa hatujafikia bado lengo tulilojiwekea kama ambavyo makuwadi mnatuimbia.
 
Hajakurupuka. Anajua anachokifanya. Anatetea tumbo lake hata pale ambapo haina haja ya kutetea. Sisi kama nchi tuma malengo yetu. WB haiwezi kutuwekea malengo. Tunajiwekea malengo sisi wenyewe. Na ndicho alichokisema JK jana.
Kuna mtu kakurupuka vibaya

JK alisema mzee mkapa alikuwa na matamanio ya kufikia uchumi wa kati kwa per capita kuwa USD 3000 hata kama tunajua kwamba uchumi wa kati ungetuhitaji kuwa na per capital around 1080.

Yaani ni sawa sawa na mtu uwe na matamanio ya kufaulu chuo na First Class badala ya ule ufaulu wa kawaida wa wengi wa Lower second.

Itakuwa maneno ya Kikwete yamewachoma sana
 
Unaelewa maana ya utaalamu?

Unapoongelea utaalamu kwenye uchumi basi angetakiwa mtu mwenye elimu ya uchumi!

Je huyo msemaji ni mwana uchumi?

Kama sio kwanini unasema "ametoa ufafanuzi wa kitaalamu"?
Yeye ni msemaji kwahiyo hata kama siyo mchumi basi amezungukwa na wachumi!
 
Waliosema tumeingia uchumi wa Kati world Bank , sio kwa Kauli yako au mtu Mwingine

Mpango ulipangwa na world bank?

Kama taifa huru tulitengeneza road map

By 2025 kufikia, maana yake tunaweza kuwahi kabla kama tulivowahi ila tusizidi

Katika mpango pia tukajiwekea malengo kwamba kwa kipato chetu kiwe usd 3000

Tulipanga sisi kama watanzania sio world bank.

World bank ilichofanya nikutuambia tumeshafikia uchumi wakati lakini rod map tumejipangia

Tuache upumbavu
 
Ndiyo maana nime-quote..
Alimaanisha GNI ya sasa inatuweka kwenye uchumi wa kati according to World Bank. Na tumefikia hatua hiyo kabla ya 2025.
Ndo walewale mnaopotosha rank za WB middle income inaanzia USD 1062-12065 lkn lengo la dira ya maendeleo 2025 ni kuwa na kipato cha USD 3000 na hata Jana mchumi kikwete kalielezea vizuri kabisa.
 
Yeye ni msemaji kwahiyo hata kama siyo mchumi basi amezungukwa na wachumi!
Unaelewa maana ya hii sentensi uliyo andika?

"Ameongea kama serikali na kama mtaalamu wa uchumi!"

Je inahusiana vipi na ulichoandika hapa kwamba kazungukwa wanauchumi?

Kwa hiyo magufuli tumuite injinia kisa kazungukwa na mainjinia?
 
Mpango ulipangwa na world bank?

Kama taifa huru tulitengeneza road map

By 2025...... kufikia, maana yake tunaweza kuwahi kabla kama tulivowahi ila tusizidi

Katika mpango pia tukajiwekea malengo kwamba kwa kipato chetu kiwe usd 3000

Tulipanga sisi kama watanzania sio world bank.

World bank ilichofanya nikutuambia tumeshafikia uchumi wakati lakini rod map tumejipangia

Tuache upumbavu
Hukuwa na ulazima wa kuweka hiyo sentesi ya mwisho!
 
Unaelewa maana ya hii sentensi uliyo andika?

"Ameongea kama serikali na kama mtaalamu wa uchumi!"

Je inahusiana vipi na ulichoandika hapa kwamba kazungukwa wanauchumi?

Kwa hiyo magufuli tumuite injinia kisa kazungukwa na mainjinia?
Kwani utaalamu wa uchumi ni nini?

Acha kukariri bwashee!
 
Back
Top Bottom