BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Unapoitaja Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA jina linalokujia kwa haraka ni DK Ages Kijazi Mtaalam wa tasnia ya utabiri wa Hali ya Hewa kwa miongo kadhaa sasa.
Licha ya ubobevu wake wa masuala ya Hali ya Hewa, DK Kijazi ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi mbali ya kuifanya TMA kuwa chombo kinachoaminika sasa kwa kutoa utabiri wenye usahihi kwa asilimia 97.3 umri wa utumishi Serikali umemtupa mkono.
Ili kuendelea kutoa mchango wake DK Kijazi sasa anakwenda kujiunga na WMO kama Mkurugenzi anayesimamia taasisi za hali ya hewa kwa upande wa Bara la Afrika.
TMA imetoa taarifa za DK Kijazi Kustaafu kama Mkurugenzi Mkuu, CMG na Wadau wa Hali ya Hewa ikiwemo wakulima, wavuvi na sekta ya usafiri watamkumbuka kutokana na mchango mkubwa aliotoa kwa jamii ya Watanzania na dunia kwa ujumla.