mwanamwana,
Pole sana kama Bashiru ambae ni dhahiri kafilisika kisiasa,nawe unakiri na kujivunia udhaifu. Ndio maana bila ya soni unajaribu kupindisha hoja.
1.Kwa Marekani Trump na Rais mwingine yeyote anaweza kuondolewa kupitia
uchaguzi. Historia inathibitisha hilo. Marekni hakuna chama iwe Democrats au Republicans, kilichofanikiwa kung'ang'ania madarakani.
2.Nelson Mandela pamoja na machungu/maonevu aliopitishwa hakuvaa viatu vya uonevu na ukandamizaji. Hakulipa visasi. Wasiokuwa na busara/uwezo wa kuongoza wakikosa mvuto ndio hukimbilia na kujivunia maguvu ya dola.
3.Sir Robert Mugabe alianza vizuri wakati wa ukombozi, na hata miaka ya mwanzo baada ukombozi. Baada ya (Sally) Mke mwenye busara kufariki shetani aliingia kichwani mwake kupitia Dogodogo Joyce. Akawa mpya dikteta asie busara, asietaka(yeye binafsi) kuachia madaraka kama walivyofanya, wakombozi wa kweli, akina Mandela. Lakini dola hiyohiyo ndo ilikuja mtoa.
CCM wala Jiwe wanajijua hawana mvuto. Ndio maana mnashinda mwaimba mapambio na kutajataja majina yake yote wakati wote, mahali pote pamoja kutegemea maguvu ya dola kutoa vitisho na kukanadamiza wenye mawazo tofauti/mbadala. Mungu wa kweli YUPO.