Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Ameongea ukweli ila tatizo ni pale msomi wa Tanzania mwenye Phd anaongea maneno kama hayo akijua wazi kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi!

Maana yake ni
  • Hakuna maana ya uchaguzi
  • hakuna haja ya vyama vingi vinavyokula rukuzu lakini havina tija kwa wananchi
  • Wananchi hawachagui viongozi wao bali chama tawala huamua nani awaongoze
  • Vyama vya siasa na wananchi huwa wanapoteza muda wao tu kwenda kwenye mikutano
Wako wasomi wachache nchi wako kwa ajili ya wananchi
 
Return Of Undertaker,
Hongera Dr. Bashiru kwa kusema ukweli kuwa bila dola CCM haiwezi kushinda. Nataka nimfundishe kidogo kuwa dola haijawahi kushinda umma, akaliulize Kaburi la Dikteta Gadafi kama Dola ilishinda nguvu ya Umma. Sisi tunajivunia nguvu ya Umma na wao watumie Dola na ICC itawahusu.
Wanaamini ukiwakamata viongozi Wa juu wa vya dola Kwa kuwapa minofu basi wamewakamata wote yaani Wa chini wao ni kutii tu maagizo kumbe awaelewi Wa chini wwengi nao ni wahanga sawa Na jamii inayoumia maana ni sehemu ya jamii pia hivo kutegemea dola ni upofu
 
Ndio maana kumtoa Mbowe kwenye uwenyekiti ni kazi mno, ukijaribu tu unaambiwa sumu haijaribiwi kwa kuonjwa.
Hatimaye mnakiri kuwa CCM inatumia dola kubaki madarakani!Mtasema yote mnayoyafanya,ipo siku mtakiri kujaribu kumtoa roho Lissu!
 
Dola unahusikaje na uchaguzi? Kwa kweli hapa sijaelewa kabisa.
Hukuona kilichotokea zanzibar 2015?Hiyo ndio maana ya dola!Au pia muulize kafulila,jumla ya kura zilionesha yeye ndiye kashinda lakini mkurugenzi kamtangaza yule mama wa CCM ndiye mshindi,alihangaika na ushahidi mahakamani akapigwa kalenda mpaka akachoka,wakaona wampe ofa ajiunge nao kisha apewe shavu!Hiyo ndio maana ya alichokisema Bashiru!
 
the truecaller,
Nimejikuta nakumbuka maneno ya polepole kuwa uchaguzi ukiwa huru na haki basi CCM ijiandae kukabidhi nchi kwa wapinzani!Nikiunganisha ujumbe huu na hayo aliyosema Bashiru napata picha kamili!
 
Anaonekana hata USA haijui hakuna chama USA kinategemea dola kushinda.Trump kashinda sababu Democratic hawakuwa Na mgombea smart. Kama watasimamisha mgombea smart trump hawezi rudi
 
c33cf55c37e844aa818d600e4e29aac1_18.jpg
Jemadari Tundu Antipas Lissu 2020
 
Yaani pamoja na maelezo aliyoleta undetaker huyu ole mushi kashindwa kumuelewa bashiru?
Ukitaka kupata picha kamili,unganisha na maneno aliyowahi kusema JK kuwa CCM iache kutegemea kubebwa na dola badala yake ijibu hoja kwa wananchi!

Pia inapata back up ya maneno aliyowahi kusema Polepole kuwa kukiwa na tume huru ya uchaguzi basi CCM ijiandae kukabidhi nchi!

Nadhani hayo yote yalithibitika kwa kilichotokea Zanzibar 2015,dola ilizuia ushindi wa CUF wazi wazi!
 
Mie nilipenda na kufurahia Zimbabwe ambako Jeshi lilikuwa linawakata makofi askari wanaozuia RAIA kuandamana, always soldiers are smart than policemen

Sent using Jamii Forums mobile app
Jeshi huwa linalinda maslai ya nchi polisi wao ulinda maslai ya wanasiasa. Jeshi huwa linapima nguvu ya wananchi ikiwa kubwa umtosa mtawala Na kuungana Na wananchi iko duniani kote jeshi uamini ni heri wamtose mtawala ili wengi wapone sababu uogopa kutengwa kimataifa ndio kilichotokea Zimbabwea, Malawi, Sudan, Egypt nk.
 
amedhihirisha kwa uwazi pasi na shaka alicholonga ndicho kilivyo.

ila hapo maana yake tanzania hakuna demokrasia uhuru wa kujieleza, tume huru ya uchaguzi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa,

kuna sheria kandamizi, utawala wa kimabavu, vyombo egesha vya usimamizi wa haki na usimmizi wa uchaguzi

Eeh Mungu tunusuru na janga hili la CCM na mazalia yake
 
Huu ni ukweli sana au kuongea sana!
Nina watani zangu usiombe mambo yao yakukute. Bora yasikie kwangu kama michapo. Akikukanyaga, ukirogwa ukamuuliza, utashangaa jibu lake. Umemuuliza tu kwa sababu za kuchangamsha baraza.

Sio kwamba umekasirika kihivyo. Kwa jibu lake utazimia. Kitakachokukasirisha sio kukanyagwa bali jibu. " Nimekukanyaga, sasa unasemaje? Ndilo jibu la katibu mkuu wa CCM! Ulevi mtupu wa madaraka.

Hajui hata uchaguzi ulio huru na wa haki? Shame on him!
 
Back
Top Bottom