Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Huyu Bashiru sasa ndio anakuja na ile sura yake kamili ya Mujahedeen, anaongea kabisa kama "A True Militant" ambaye kubaki kwake ikulu hakuhusiani kabisa na matakwa ya wananchi ila DOLA.

Kuna kipindi aliyekuwa rais wa Kenya Bw. Daniel Toroitich arap Moi (Rip) alikuwa akiropoka exactly hayo hayo anayoropoka huyu Bashiru leo tena kwa jeuri.

Ila mimi nasema siku zote kuwa majaliwa ya ccm kuendelea au kutokuendelea kubaki madarakani yako mikononi mwa wazungu, wakiamua tu leo kuwa ccm sasa basi ndio utakuwa mwisho wao.

Wakigoma leo kuwa hakuna mikopo yoyote wala misaada mara moja ccm itakuwa kama mgonjwa wa Corona na hata mwaka serikali yao haitadumu madarakani kwani hii serikali iko very vulnerable to sanctions than the beleaguered Zimbabwean government. They can't make it.
 
Sioni sababu ya upinzani kushiriki huu uchaguzi. Kumbe vyama vya upinzani vinashindana na CCM pamoja na dola. Katibu mkuu wa CCM bora akae kimya maana hajielewi. Kalewa vibaya mno.
Hata Rais Kaunda wa Zambia aliposhondwa uchaguzi wa vyama vingi kwa mara ya kwanza, Mzee Daniel Toroitich Arap Moi alimshangaa sana akasema inakuwaje Kaunda anashindwa uchaguzi wakati ana dola?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saddam, Gaddafi, yahya jameh,Mobutu, idi amini ,al bashir,walimiliki dola waliondolewa Kwa uzembe in Bashiru voice
 
Dr. Bashiru aende akamuulize Marehemu Robert Mugabe, kuhusu wananchi wakimchoka mtawala hali huwa inakua vipi.

CCM wanajidanganya sana, halafu huwa wanajisahaulisha kwamba ipo siku raia wataamua la kuamua.
Mazingira ya Zimbabwe ni tofauti na ya Tanzania, kule alikuwa mtawala mmoja muda wote lakini huku kwetu ni watawala tofauti tofauti ila chama ndo cha muda wote na kila mtawala anakuja kwa staili yake.

Huyu wa sasa anapendwa zaidi na masikini na wale wa kipato cha kati wanaoishi kihalali na kuchukiwa na wapigaji ambao ndo wanabwabwaja tofauti na mtangulizi wake alowakumbatia wapigaji.

Leo hii zile kauli za mpumbavu fulani tu kukutishia eti nitakulaza ndani hazina nafasi tena maana zilikuwa zinawapa unafuu wenye nacho kwa kuwatishia wasio nacho. Kwa hivyo kuna utofauti mkubwa kati ya Zimbabwe na Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichokisema ndio ukweli wenyewe, labda kosa lake ni kusema hadharani mbele ya vyombo vya habari.

Mkuu Bashiru anaongea kwa kupanic, hiyo panic sio bure. Haya madai ya tume huru ya uchaguzi yanamtia wazimu. Akiangalia idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo, anaona kabisa hao wachache waliojiandikisha kupiga kura ni wanaccm, wengi ambao hawajajiandikisha ni wapiga kura wa upinzani.

Sasa anapiga mahesabu iwapo watu watashikilia hilo suala la kudai tume huru ya uchaguzi, na ikabidi iwepo anahofia ccm itakuwa na hali gani? Hao akina Mbatia wanajaribu kutumiwa lakini haionyeshi kuubadili umma unaojielewa. Huyo Bashiri anaongea hayo kwa ghadhabu maana kujengea hofu umma ndio suluhu yao.

Mimi nawashauri wapinzani washikilie hapo hapo upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi, ili waiweke ccm kwenye kona mbaya zaidi kitaifa na kimataifa.
 
''Mchakato wa katiba mpya ni kiporo kilichochacha, ukila utaumwa matumbo''-Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu @ccm_tanzania

#BashiruAllyIPPMedia
 
Yupo sahihi,wapinzani waliposusa walisababisha haya yanayotokea sasa. Acha tupambane na hali zetu.

macson
 
Kweli pale Mlimani ni jalalani...ati kasema nini??

Everyday is Saturday................ 😎
 
2316889_FB_IMG_1582491848963.jpg
 
Hiyo ni lugha ya Dk, siyo ya pole pole, watakaomuelewa ni wachache, ila kaongea ukweli na wajinga hapa wamechukulia dola kama ni polisi.
 
''Mchakato wa katiba mpya ni kiporo kilichochacha, ukila utaumwa matumbo''-Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu @ccm_tanzania

#BashiruAllyIPPMedia
Bashiru 👎 ni kielelezo cha wasomi wa tumbo street. Unganisha uzi huu na matamshi ya kutumia dola kulinda ushindi wa ccm hapo. Tunzeni vielelezo vya ICC mwakani.
 
Back
Top Bottom