Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Return Of Undertaker,
Hongera Dr. Bashiru kwa kusema ukweli kuwa bila dola CCM haiwezi kushinda. Nataka nimfundishe kidogo kuwa dola haijawahi kushinda umma, akaliulize Kaburi la Dikteta Gadafi kama Dola ilishinda nguvu ya Umma. Sisi tunajivunia nguvu ya Umma na wao watumie Dola na ICC itawahusu.
 
Hata wakati wa hayo mazungumzo na mahojiano huko ITV Comrade Bashiru alizungumzia TAFSIRI POTOFUKAMA HII. Lakinihuwezi kumzuia mtu kutoa tafsir yake kadri apendavyo TO SUIT HIS/HER NEEDS AND GOAL! Hiii ni mfano hai wa hilo alilosema Comrade Bashiru.
 
Tatizo la bashiru ni moja kapewa kazi ya kuwa mtendaji mkuu wa chama lakini yeye mwenyewe hajui siasa. Huu aliousema ni ukweli mchungu. Hakuna ubishi kwa alichokisema labda tu kwa jinsi ulivyowasilishwa..!
Tunajuwa kuwa huo ndiyo ukweli ila kwa kukiri hadharani anaonekana siyo mkomavu na mambo haya. Yaani ukweli huu ulipaswa kuwa siri yake na CCM wenzie. Kiuongozi amefeli kwa vile ameshafichua siri za uwizi wa kura. Hilo tamko siyo zuri kwa kipindi hiki ambacho Big Brother (Marekanı) anafuatilia mchakato wa uchaguzi wa Tanzania bumper to bumper.

Kwa vile Magufuri huwa anawatukana wateule wake wakikosea, naamini AMESHA MTUKANA Bashiru Ally kuwa PUMBAVU. Au atamtukana usiku kwa vile ndiyo muda wake wa ku review issues
 
Bashiru ameongea ukweli ambao kama ukiuchanganua kwa mapana sana unaweza kumpa room ya kutokea kwamba hakumaanisha vibaya, ila kwa tafsiri rahisi tu ambazo watz wengi ndio tunazozitaka hapa atakuwa amejikaanga mwenyewe! Jamaa anajua kila mtu ni msomi na ana falsafa kama zake anatakiwa ajue jamii anayoona anaieleza ukweli kuwa haihitaji kuusikia huo ukweli wake zaidi atajiponza tu mwenyewe
 
Lengo namba moja ya Chama chochote cha Siasa ni kushika Dola..na Chama kinachoongoza Dola mara nyingi ni Ngumu Sana kukinyanganya Dola unless kiwe kimechokwa na Kada zote especially Dola yenyewe.
 
hawa watu hawaishi kukitaja chama chetu pendwa CHADEMA.
 
mwanamwana,
Pole sana kama Bashiru ambae ni dhahiri kafilisika kisiasa,nawe unakiri na kujivunia udhaifu. Ndio maana bila ya soni unajaribu kupindisha hoja.

1.Kwa Marekani Trump na Rais mwingine yeyote anaweza kuondolewa kupitia uchaguzi. Historia inathibitisha hilo. Marekni hakuna chama iwe Democrats au Republicans, kilichofanikiwa kung'ang'ania madarakani.

2.Nelson Mandela pamoja na machungu/maonevu aliopitishwa hakuvaa viatu vya uonevu na ukandamizaji. Hakulipa visasi. Wasiokuwa na busara/uwezo wa kuongoza wakikosa mvuto ndio hukimbilia na kujivunia maguvu ya dola.

3.Sir Robert Mugabe alianza vizuri wakati wa ukombozi, na hata miaka ya mwanzo baada ukombozi. Baada ya (Sally) Mke mwenye busara kufariki shetani aliingia kichwani mwake kupitia Dogodogo Joyce. Akawa mpya dikteta asie busara, asietaka(yeye binafsi) kuachia madaraka kama walivyofanya, wakombozi wa kweli, akina Mandela. Lakini dola hiyohiyo ndo ilikuja mtoa.

CCM wala Jiwe wanajijua hawana mvuto. Ndio maana mnashinda mwaimba mapambio na kutajataja majina yake yote wakati wote, mahali pote pamoja kutegemea maguvu ya dola kutoa vitisho na kukanadamiza wenye mawazo tofauti/mbadala. Mungu wa kweli YUPO.
 
Oct 2020 ifike tu kwa kweli.,watanzania wanaweza wakawastaajabisha!!
 
Back
Top Bottom