Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Kuna mjadala mkali kwa sasa mitandaoni, mitaani na viringeni juu ya kauli ya Dkt Bashiru Katibu mkuu wa CCM, Kwa ufupi ni kuwa Dkt. Bashiru alikuwa sahihi kabisa alipo jenga hoja ya kuendelea kutumia dola kubaki madarakani. Baadhi yetu tumeipokea kauli hii katika mrengo hasi na wa kiushabiki zaidi kutokana na tofauti zetu za kiitikadi. Sharti ieleweke kuwa lengo kuu la chama chochote cha kisiasa ni kushika dola, dola (state), ni dhana pana na hili ushike dola lazima upate ridhaa ya wananchi yaani umma wa Watanzania kupitia mifumo rasmi ya kidemokrasia.

Kama dola iliyopo madarakani ni sauti ya wananchi basi dola hiyo hiyo utumia mifumo ya kidola kujitawala na kuwatumikia wananchi ili iendelee kuaminika na kujichimbia madarakani. Dkt. Bashiru hajatishia kutumia vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani, ingetumika kauli ya namna hiyo kwa vyovyote vile yangekuwa ni makosa makubwa
kisiasa hasa kwenye siasa za mfumo wa vyama vingi, Kwa ufupi Dkt. Bashiru yupo sahihi kabisa kwa kauli yake.
 
Mystery, Wekeni tafsiri yenu yenye mawazo hasi lakini ukweli unabaki kuwa ukweli.

Kwamba, chama chenye Serikali iliyoko madarakani kisipoisimamia vizuri Serikali kutimiza wajibu wake kitaondolewa madarakani. Hata katika maisha ya kila siku kama mme/mke hatimizi wajibu wake ipasavyo ndoa inakuwa mashakani. Kama umeajiriwa, usipotimiza wajibu wako unafukuzwa.
 
Kuna mjadala mkali kwa sasa mitandaoni, mitaani na viringeni juu ya kauli ya Dkt Bashiru Katibu mkuu wa CCM, Kwa ufupi ni kuwa Dkt. Bashiru alikuwa sahihi kabisa alipo jenga hoja ya kuendelea kutumia dola kubaki madarakani. Baadhi yetu tumeipokea kauli hii katika mrengo hasi na wa kiushabiki zaidi kutokana na tofauti zetu za kiitikadi. Sharti ieleweke kuwa lengo kuu la chama chochote cha kisiasa ni kushika dola, dola (state), ni dhana pana na hili ushike dola lazima upate ridhaa ya wananchi yaani umma wa Watanzania kupitia mifumo rasmi ya kidemokrasia.

Kama dola iliyopo madarakani ni sauti ya wananchi basi dola hiyo hiyo utumia mifumo ya kidola kujitawala na kuwatumikia wananchi ili iendelee kuaminika na kujichimbia madarakani. Dkt. Bashiru hajatishia kutumia vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani, ingetumika kauli ya namna hiyo kwa vyovyote vile yangekuwa ni makosa makubwa
kisiasa hasa kwenye siasa za mfumo wa vyama vingi, Kwa ufupi Dkt. Bashiru yupo sahihi kabisa kwa kauli yake.

..uhalisia ni kwamba ccm inavitumia kisiasa VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA kuvikandamiza vyama mbadala.
 
Inawezekana lakini sijafanya utafiti wa jambo hili kwa undani siwezi kubisha wala kukubali lkn haipaswi kuwa hivyo kutokana na nchi kuwa na mfumo wa kidemokrasia na vyama vingi, tunapaswa kuwa na minzania sawa katika ulingo wa kisiasa.
 
..kwa mfano Mh.Tundu Lissu alishambuliwa baada ya walinzi wa serikali kuondolewa ktk eneo ambalo hulindwa 24/7. Mambo kama hayo ndiyo yanachukiza wananchi na kuchafua taswira ya nchi yetu.
 
tuondoe tofauti za itikadi zetu na tuwaombee wote walioshiriki kwenye issue hiyo Mungu awalipe kadiri anavyoona inafaa.
 
Return Of Undertaker,
Duh...............

Hatimaye wameamua kuukiri ukweli kuwa bila dola hakuna CCM!

Kweli vyama vya upinzani mna kazi ngumu sana kuking'oa hiko chama madarakani.........

Lakini maandiko yamenena Haki huliinua Taifa,na usipotenda haki hakika unajiangamiza

Hao watawala wetu wanapaswa kujifunza kwa kile kilichomtokea Mugabe, ambaye alamini kuwa "State Organs" vipo kumsimamia yeye, lakini ni vyombo hivyo hivyo vya dola ndivyo vilivyomtoa madarakani

Hao CCM wanatenda maovu yote hayo wakiamini kuwa "watabebwa" na Polisi

Lakini ipo siku inakuja hao hao Polisi, watawageuzia kibao na kuwaambia tuacheni tutekeleze majukumu yetu kwa mujibu wa Katiba ya nchi, ambapo tunatakiwa tuwe "neutral"

Hapo ndipo hiko chama kitatamani ardhi ifumuke na wafukiwe ndani kwa kukwepa aibu!
Umeshau na Kanu kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clearly kuna harakati za waz za ccm kuwakatisha wananchi tamaa ili namba ya wapigakura ipungue ili wajichukulie ushindi kwa kutumia dola kwahiyo ni wajibu wa wananch wakipiga kura wakumbuke kuzilinda bila hivyo wajilaum wenyewe
 
Huo ni ushahidi tosha CCM wanatumia dola kukandamiza, kudhulumu, kuuwa , kupoteza tena bila kuchunguza mradi wabaki madarakani!
Kasema wazi katikiro wa chama dola.
Ndio maana tunataka katiba nzuri ya kuondoa huo uozo!!
Watu wanapigwa risasi mchana kweupe wanapotezwa hakuna uchunguzi, unasema tuna dola kweli katikiro??
Watanzania wanahitaji katiba nzuri kutengeneza taifa lenye haki, kwa sasa ni uonezi tuu!!
 
Kwa tafsiri ndogo sana. Katafute sehemu yoyote vilipozungumziwa vyombo vya dola hapa Tanzania uone ni vyombo gani vimetajwa. Vyombo vilivyotajwa ni vyombo vya ulizi na usalama.

Back
Top Bottom