Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Kuna mjadala mkali kwa sasa mitandaoni, mitaani na viringeni juu ya kauli ya Dkt Bashiru Katibu mkuu wa CCM, Kwa ufupi ni kuwa Dkt. Bashiru alikuwa sahihi kabisa alipo jenga hoja ya kuendelea kutumia dola kubaki madarakani. Baadhi yetu tumeipokea kauli hii katika mrengo hasi na wa kiushabiki zaidi kutokana na tofauti zetu za kiitikadi. Sharti ieleweke kuwa lengo kuu la chama chochote cha kisiasa ni kushika dola, dola (state), ni dhana pana na hili ushike dola lazima upate ridhaa ya wananchi yaani umma wa Watanzania kupitia mifumo rasmi ya kidemokrasia.
Kama dola iliyopo madarakani ni sauti ya wananchi basi dola hiyo hiyo utumia mifumo ya kidola kujitawala na kuwatumikia wananchi ili iendelee kuaminika na kujichimbia madarakani. Dkt. Bashiru hajatishia kutumia vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani, ingetumika kauli ya namna hiyo kwa vyovyote vile yangekuwa ni makosa makubwa
kisiasa hasa kwenye siasa za mfumo wa vyama vingi, Kwa ufupi Dkt. Bashiru yupo sahihi kabisa kwa kauli yake.