Wasalaam!
Kwa muono wangu nikajua mwenyekiti peke yake ndiye msemakweli mpenzi wa Mungu!
Maana Mwenyekiti kwa upenzi wake wa Mungu, kuwa hapimi kina, yeye chochote kinacho bipu ubongo, hukimwaga hadharani! Mfano " nikupe Gari, nyumba then umtangaze mpinzani mshindi"
Hapo alimwaga hadharani na kutujuza kumbe kuna waamuzi zaidi ya kura za wananchi, kumbe hamna tume za chaguzi ila kuna "kichwa chaguzi" msemakweli alisema kweli!
Sasa cha ajabu kumbe hata Katibu naye " mpenzi wa Mungu" wanajua kutoa ukweli! Kumbe ambacho msemakweli namba moja alikiweka moyoni Katibu kaja kumalizia, kumbe huwa hawashindi ila dola ndio huharibu chaguzi!
Wenyeviti waliopita waliharibu ila walichokosa ni kuwa "wapenzi wa Mungu" safari hii timebahatika kupata haiba zinazoshabihiana Mwenyekiti na Katibu wapenzi wa Mungu!
Kazi ipo Tanzania!