Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Chama cha CCM kupitia katibu mkuu wake kimesema kitatumia dola kubaki madarakani hivyo kura yangu si haki yangu. Mimi kushiriki kupiga kura yangu haitakuwa usaliti wa kushindana na dola? Wajuzi wa JF of GT nielimisheni.
Swadakta hata mimi sito piga kura ni upotezaji wa muda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi hata kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura sitoenda,kitambulisho cha nida kitanitosha
Dk katusaidia kuokoa mda wakushinda foleni,na kama inawezekana na uchaguzi wangeufuta,hela ya uchaguzi wafanyie Mambo mengine kuliko kuzitumia kwenye uchaguzi,Dk amenifulahisha sana kawa muwazi,Sasa kazi imebakia kwa vyama vya siasa waamue kuacha au waingie hivo hivo kwenye uchaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikiliza wewe Mwenyewe maelezo ya Bashir

Bashir kafafanua kuwa Dola ni Raia na Ccm itatumia Dola kubaki madarakan

Ukitumia Dola kuimarisha amani na Usalama watu wakiridhika na kukupa idhin maana yake umetumia dola

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama cha CCM kupitia katibu mkuu wake kimesema kitatumia dola kubaki madarakani hivyo kura yangu si haki yangu. Mimi kushiriki kupiga kura yangu haitakuwa usaliti wa kushindana na dola? Wajuzi wa JF of GT nielimisheni.

Naenda kupiga kura saa kumi na moja asubuhi nipo mstarini

Kwenye karatasi natafuta Chadema ilipo!

Wakiiba kura then naloga serikali nzima...mawe atakua analala makaburini kila siku!

We run this shit!
 
Chama cha CCM kupitia katibu mkuu wake kimesema kitatumia dola kubaki madarakani hivyo kura yangu si haki yangu. Mimi kushiriki kupiga kura yangu haitakuwa usaliti wa kushindana na dola? Wajuzi wa JF of GT nielimisheni.
Kwa kupiga kura kuchagua yeyote zaidi ya CCM ni kushindana na dola, na kwamwe huwezi kuishinda dola bila ncha ya upanga, hivyo kupiga kura kutegemea utaishinda dola ni kupoteza muda wako
 
mwanamwana,

Mnachoshangaa ni nini alichoongea ndio kinachofanyika siku zote nanyi ni mashahidi, kwani mlitaka aongope. Huyu ni msomi si mwanasiasa ameeleza walichofanya kwa kipindi chote cha miaka 4 na watamalizia kufanya hicho hicho mpaka 25/10.

Uchaguzi wa 25/10/2015 Zanzibar ni mfano dhahir. Unaweza kuitaja hata mifano 1000 iliyofanyika katika kipindi hiki cha miaka 4 toka Bungeni, mahakama, chaguzi zote ndogo n.k.

Msubirini POLE POLE aje azitafsiri sentensi zote za Bashiru kisiasa. Ataanza kwa kusema nyie hamkumuelewa.......... hapo alimaanisha...........
 
Ameongea ukweli kabisa. Tatizo watanzania hatupendi kuambiwa ukweli
 
Wasalaam!

Kwa muono wangu nikajua mwenyekiti peke yake ndiye msemakweli mpenzi wa Mungu!

Maana Mwenyekiti kwa upenzi wake wa Mungu, kuwa hapimi kina, yeye chochote kinacho bipu ubongo, hukimwaga hadharani! Mfano " nikupe Gari, nyumba then umtangaze mpinzani mshindi"

Hapo alimwaga hadharani na kutujuza kumbe kuna waamuzi zaidi ya kura za wananchi, kumbe hamna tume za chaguzi ila kuna "kichwa chaguzi" msemakweli alisema kweli!

Sasa cha ajabu kumbe hata Katibu naye " mpenzi wa Mungu" wanajua kutoa ukweli! Kumbe ambacho msemakweli namba moja alikiweka moyoni Katibu kaja kumalizia, kumbe huwa hawashindi ila dola ndio huharibu chaguzi!

Wenyeviti waliopita waliharibu ila walichokosa ni kuwa "wapenzi wa Mungu" safari hii timebahatika kupata haiba zinazoshabihiana Mwenyekiti na Katibu wapenzi wa Mungu!

Kazi ipo Tanzania!
 
Back
Top Bottom