Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Habari inayo-trend sana kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa ni kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally, kuwa wao wanaendelea kubaki madarakani kutokana na kutumia vyombo vya dola

Katika maelezo yake aliyoyatoa kwenye luninga ya ITV siku chache zilizopita, aleleza kuwa chama cha KANU cha Kenya na UNIP ya Zambia, kuwa waliondolewa madarakani, kutokana na viongozi wake kufanya uzembe wa hali ya juu, kwa kutoweza kutumia vyombo "vyake" vya dola kuendelea kubaki madarakani!

Hivi kwenye nchi yoyote inayoendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, si kwa kutumia kura za wananchi, kupitia sanduku la kura, ndivyo vinavyoendelea kukibakiza chama kilchoko madarakani?

Sasa inakuwaje Katibu Mkuu wa CCM atamke hadharani kuwa chama chake, kinatumia nguvu za vyombo vya dola, kukibakisha madarakani?

Huo ndiyo ninaouita ulevi wa madaraka uliopindukia, alioufanya Katibu Mkuu huyo wa CCM.

Hivi anajua alichotamka ni kinyume cha Katiba yetu ya nchi, ambayo kwenye ibara ya 3(1) inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa ni ya mfumo wa vyama vingi?

Kumbe mateso yote wanayopitia viongozi wetu wa vyama vya siasa vya upinzani yanatokana na chama cha CCM kutumia madaraka yake vibaya, kwa kuviagiza vyombo vya dola, kuwashughulikia viongozi hao wa upinzani?

Ninachofahamu ni kuwa Katibu huyo Mkuu amefikia kiwango hicho cha ulevi wa madaraka, kwa kuamini kuwa hakuna chombo chochote hapa nchini kinachoweza kumchukulia hatua, za uvunjifu wa waziwazi Katiba yetu ya nchi, kutokana na ubovu wa Katiba yetu ya nchi, ambayo imempa mamlaka ya ki-mungu mtu, Rais wa nchi hii, ambaye pia ndiyo kiongozi wa chama kilichoko madarakani cha CCM, ambaye ndiye "engineer" wa kuvitumia vyombo vya dola, kukandamiza demokrasia hapa nchini

Naamini kabisa, kauli hiyo inatosha kabisa kuifikisha CCM kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya The Hague, ili waweze kujibu mashitaka, ni kwa vipi wao watumie vyombo vya dola, ili waendelee kubaki madarakani.
 
2306076_1572191514899.jpeg
 
Habari inayo-trend sana kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa ni kauli aliyoitoa Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally, kuwa wao wanaendelea kubaki madarakani kutokana na kutumia vyombo vya dola...
Tushukur Mungu ameongea ukweli pasipo shaka...asingeongea hivi angekua hajafumbua macho ya watu kuhusu majukumu ya dola...watu wangeamini kwamba dola inafuata katiba na sheria za nchi na sio kufuata maelekezo ya mtu au tasis fulani..

Mimi nimependa amejibu vile ukweli unavyoonekana machoni PA wananchi!! B. ALLY endelea kutumia dola kama ulivosema hata kama ni kinyume cha sheria tumia tu!

Kama ni kukamata wala rushwa tumia tu!

Kama ni kuminya upinzani tumia tu.

Kama ni kununua watu tumia tu.

Kama ni kulinda wezi wa Chama fulani tumia tu.

Kama ni kukamata wanaotumia uhuru wa kikatiba kuhusu kujieleza tumia tu..!! Nk.

Ila msisahau iko siku dola hyohyo itatumika kuwarudi..!!wakati si ukuta!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu 'Mystery'

Wewe huoni kwamba Katibu Mkuu anastahiri kushukuriwa kwa kuwa muwazi; waTanzania tumezoea sana unafiki wa kufichaficha mambo hata wakati tunapokuwa tunajua yanayofanyika, sisi tunabaki kufichaficha, sijui kwa faida ya nani?

Safari hii tumewapata watu (watawala) hasa hao wawili ndani ya CCM wasioficha kitu. Wanakupa ukweli, hata kama ni mchungu uhangaike nao mwenyewe!

Sasa tatizo linakuja kwetu tunaosikia ukweli huo tunaopewa, halafu badala ya kuupokea na kuufanya uwe changamoto ya kutafuta ufumbuzi wake, tunabaki hapo tukilialia; sijui tunamlilia nani!

Na kama hatuwezi kupata ufumbuzi wa changamoto zinazotokana na hayo wanayotutangazia watayafanya, si basi tubaki na ukweli huo ambao wameuweka wazi, na kukubali kusalimu amri na maisha yaendelee!
 
Mkuu 'Mystery'
Wewe huoni kwamba Katibu Mkuu anastahiri kushukuriwa kwa kuwa muwazi; waTanzania tumezoea sana unafiki wa kufichaficha mambo hata wakati tunapokuwa tunajua yanayofanyika, sisi tunabaki kufichaficha, sijui kwa faida ya nani?....
Sasa Mkuu Kalamu1 unategemea wananchi tutumie mbinu gani, wakati Katibu Mkuu keshaweka wazi kuwa wao CCM wanatumia vyombo vya dola kuwatetemesha wananchi, ili waendelee kubaki madarakani?
 
Sa

Sasa Mkuu Kalamu 1 unategemea wananchi tutumie silaha gani, wakati Katibu Mkuu wa nchi keshaweka wazi kuwa wao CCM wanarltumia vyombo vya dola kuwatetemesha wananchi, ili waendelee kubaki madarakani?
Uelewa wangu ni kwamba 'DOLA' ni mali ya wananchi, wao wamekabidhiwa tu na wananchi hao kuitumia kwa kazi zinazofahamika.

Wenye 'DOLA' ndio wenye mamlaka ya kuichukua mali yao wakati wowote wasipopendezwa jinsi inavyotumika.

Najua utasema ni rahisi kuyaandika haya kuliko uhalisia unavyotakiwa kuwa.

Ndio, nitakubaliana nawe ni rahisi kuaandika, kwa sababu ugumu unakuja wakati tunapokosa dhamira ya kutekeleza kwa kuiogopa kazi ngumu.

Kuwafikia na kuwaeleza wananchi juu ya haki zao ni kazi ngumu sana, ndio maana wengi wetu hatupo huko kwenye siasa.

Lakini kwa mtu ambaye ni kiongozi, aliye na dhamira kamili kabisa ya kukataa unyanyasaji, hana njia mbadala bali kuikabiri kazi hiyo ngumu.
HKwenye historia kuna mifano mingi. Akina Mwalimu Nyerere waliamua kuweka rehani kazi ya ualimu na kukabili kazi ngumu ya kumkabili mkoloni.

Kauli kama aliyoitoa Katibu Mkuu, inastahili kabisa kuwa kichocheo cha kuwaibua watu kama hao kulinda heshima ya taifa letu hili.

Viongozi hao wapo, hata huko CHADEMA na ndani ya CCM yenyewe wamo.
 
Ukiingia kwenye siasa ubongo unakuwa utopolo automatically

Sent using OnePlus 6T Maclaren Edition
 
Uelewa wangu ni kwamba 'DOLA' ni mali ya wananchi, wao wamekabidhiwa tu na wananchi hao kuitumia kwa kazi zinazofahamika.

Wenye 'DOLA' ndio wenye mamlaka ya kuichukua mali yao wakati wowote wasipopendezwa jinsi inavyotumika...
Wewe umeongelea nadharia, na ndivyo inavyotakiwa kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Lakini hao tuliiowapa madaraka ndiyo "wanaojimwambafai" na kutotaka kutekeleza hivyo, badala yake wanataka kutumia "short cut" kwa kutumia vyombo vya dola, kuendelea kusalia madarakani
 
Huyu jamaa hata sura inaanza kubadilika!

Ukitaka kufanya mlinganisho wa uwezo walionao kama makatibu wa chama: hebu mlinganishe huyu mtu na Mzee Kinana?

Huyu ni msomi, tena mwenye PhD, kwenye nini..., 'Political Science,'? Kinana ana digrii gani.
Ni watu wenye uwezo tofauti kabisa.

Simtetei Kinana, naangalia tu matamshi na utendaji wa hawa makatibu wawili ndani ya CCM.
 
Tatizo ni "condition" wanayokuwekea viongozi wa CCM, kabla hujaingia Lumumba........

Ni lazima kwanza "usurrender" ubongo wako kabla hawajakukabidhi rasmi madaraka.

Ukweli ni kuwa, Dkt Bashiru of UDSM and Dkt Bashiru of Lumumba, are two very different people
 
Back
Top Bottom