Dkt. Bashiru Ally awakaribisha ndani ya CCM Halima Mdee na wenzake

Dkt. Bashiru Ally awakaribisha ndani ya CCM Halima Mdee na wenzake

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushawishi mkubwa.

''Upinzani walikuwa na wakinamama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni @ccm_tanzania milango iko wazi'' - Dr. Bashiru
Walikuwa na ushawishi sana ndio maana wakashindwa vibaya na sampuli za Askofu Rashidi? Kama kweli walikuwa wanawathamini basi wangeruhusu uchaguzi wa haki na uwazi ufanyike ili ushawishi wao ndio ungewapa ubunge na sio huu wa kubebwa.

Hawa wanawake shupavu wameonewa sana, wamepigwa, wametupwa ndani, wamefunguliwa kesi za ajabu, wamefukuzwa bungeni na wametukanwa matusi ya nguoni lakini hata siku moja hakuwatetea. Leo wamefukuzwa kwenye chama chao baada ya kukubali kuapishwa kwenye "gereji", kukaidi wito wa Halmashauri Kuu na mbaya zaidi kukubali kutumika kwa kupitia nyaraka ambazo sio halali ndio mnawaita mashupavu? Mbona hamkuwaona mashujaa walipoungana na wenzao kuwatimua wakina Silinde kwa kukataa tu kukubaliana na uamuzi wa chama chao kutoingia bungeni?

Mngeruhusu haki itendeke wakati wa uchaguzi haya yote yasingetokea. Ukweli ni kuwa kwa kufanya walichokifanya wamewanyima wanawake wenzao wa Bawacha walioshinda kura za viti maalum nafasi za kuteuliwa walizostahili. Wao, sio wakina Mbowe, ndio waliowanyanyasa wenzao kijinsia.

Amandla...
 
Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushawishi mkubwa.

''Upinzani walikuwa na wakinamama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni @ccm_tanzania milango iko wazi'' - Dr. Bashiru
Halima Mdee kwenda CCM itakuwa sawa na muislamu kuritadi!
 
Unajifanya hujui kwamba mtu yeyote anaingia nyuma ya CCM huwa anaambiwa aache akili zote mlangoni kabla hajaingia kwani hazitakiwi ndani?
Sawa na wanaoingia nyumba ya Chedema tu huwa wanaambiwa waache nguo zao zote mlangoni waingie ndani wakiwa uchi wa mnyama .
 
Namtazama Mdee Na wenzake kama wana waokovo, wameokoka sasa, wamezaliwa upyaa! Sasa wachape Kazi Kwa manufaa ya taifa.
 
Huu ni upumbavu wa Hali ya juu kina Halima Mdee wamenasa kirahisi kiasi hiki Ila bado wanaweza kufanya Jambo. Waeleze ukweli maana siyo wao Ni kweli tamaa na njaa lakini kikubwa ni wao kuongozwa mtego wa CCM bila wao kujua. Waombe radhi.
Nakataa unaposema kuwa hawakujuwa huo mtego wa CCM.
 
Huu uzi hauna uhusiana na uchochezi au kejeli. Hivyo naomba ubaki hapa mpaka yatakapotimia haya tunayoyaota.

Halima Mdee na wenzake 18 wametimuliwa uanachama wa CHADEMA.

Kuna uwezekano wakahamia CCM au chama kingine mamluki ili tu kuleta picha kuwa Tanzania tuna kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Lakini huu uhamisho wao unaweza usiathiri nafasi zao za ubunge wa Viti Maalumu.
 
Kwa hiyo Chadema ndiyo Kuna wanawake wa shoka CCM Kuna wanawake wa kutandika mashuka tu? Hiyo Ni Dharau kubwa kwa wakina mama wafia CCM
 
Hii kitu ni tamu sana, wasanii wa katuni wanafikiri sana
 
Sauti ya zege akija ccm atakua mtu safi Sana Ni vile tuuh anapoteza muda na dikteta wa anga gwiji wa kususia
 
Back
Top Bottom