Dkt. Bashiru Ally Katibu wangu kama hiki nilichokisikia kimetokea Kawe katika Uchaguzi wa CCM ni kweli, basi kazi ipo 2020

Dkt. Bashiru Ally Katibu wangu kama hiki nilichokisikia kimetokea Kawe katika Uchaguzi wa CCM ni kweli, basi kazi ipo 2020

Kuna watu wangu (wana medani) jirani na Kawe niliwatembelea siku ya Jumapili na wakati huo nilikuwa sijui nini kinaendelea hadi pale wenyeji wangu hao waliponiambia kuwa, ilikuwa ni siku ya kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Nakumbuka nilikuwa eneo hilo la Kawe hadi usiku wa saa tatu ambapo kwa kujiridhisha zaidi ilinibidi nizungukie maeneo mawili muhimu ya kiuchaguzi kwa Kawe ya Mzimuni alipo mkongwe Mzee Ngonyani (ambaye inasemekana alishakatwa na hatakiwi kugombea tena ila ndiyo kinara wa fitina zote akisaidiwa na Mwenezi wake aitwae Poti Poti ) na Ukwamani alipokuwa kijana makini Sultani Jeta (ambaye kwa bahati mbaya alisema kuwa hatogombea tena kwa sababu zake binafsi).

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa CCM sitaki kujua ‘ vimbwanga ‘ vya maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam vilivyotokea hiyo juzi (Jumapili ) ila kwa kilichotokea katika haya maeneo ya Mzimuni na Ukwamani ‘ nimekitathmini ‘ kwa kina na kugundua kuwa kama wana CCM hasa nyie mlio ngazi za juu msipokuwa makini, basi kuna hatari mwakani vyama vya upinzani vikashinda na hamtoamini macho na masikio yenu.

Haya ni baadhi ya mambo niliyopata kutoka hayo maeneo ya Kawe Mzimuni na Ukwamani:

Rushwa za wazi wazi wana CCM kwa wana CCM

Usaliti wa wana CCM uliopitiliza

Fujo ambako kuna muda wana CCM walikuwa wakionyesha kuwa hata wao fani ya ubondia wanayo pia.

Ushirikina wa wazi wazi na kuna mtu mmoja wa Kawe Mzimuni ‘Mkongwe' ambaye nimemtaja hapo juu anajulikana na kuogopeka sana ‘Kiuchawi' kwani na ‘Uchawi ‘ wenyewe nao anaujua mno, kasema kwa kuwa jina lake mlilikata huko juu kwa juu basi na yeye hakubali na ataondoka na mtu ‘ kindumba' kiasi kwamba kuna baadhi ya watu (Wagombea) makini sasa wanatafakari kujitoa kwa ‘kumuogopa' huyo Mzee ambaye amedumu hapo Mzimuni kwa miaka takribani 20 ila ameshindwa tu hata kuitafutia gari ya wagonjwa Hospitali ya Shamba Kawe ambayo ipo mita chache na ofisi yake.

Upandikizaji wa watu ambako inasemekana kuna Mbunge mmoja (jina kapuni) aliandaa watu wake ambao wengine walikuwa ni wa Kiume ila walivalia ‘ Hijab' na waliletwa na Usafiri wa Bajaji (ambao aliwahonga pesa nzuri tu) ili waje wawapigie Kura za Maoni hao Wagombea wa CCM ambao huyo Mbunge ‘ Fulani ‘ anawamudu ili kama kawaida mwakani awatumie tena katika Kukisaliti Chama na aweze Kupita kama ambavyo baadhi yao walimsaidia huko nyuma ( bado nasisitiza kuwa hii ni Tetesi kwani hata Mimi GENTAMYCINE basi sijaithibitisha wala kuiamini kwa 100% )

Vitisho kwa baadhi ya wana CCM wa hayo maeneo kwamba kama hawatowapigia Kura basi Wao wakitumia Ujanja wao na kupita watakuja ‘ Kuwakoma ‘ na lazima tu watawafanyia tu Kitu mbaya. Na wengi wanaotishiwa hivi ni wale wana CCM ambao wanaendesha Bishara zao katika Soko la Kawe lile la Ukwamani na hili jipya lilipo Mzimuni pamoja na wale wengine waliopo mazuri kwa ‘ Fursa ‘ za Kibiashara.

Nikupongeze pia Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kwa ‘ Kuamuru ‘ Uchaguzi huu wa ndani wa CCM urejewe / urudiwe baada ya hizo ‘ Sarakasi ‘ ila kupitia tu huu Uzi wangu GENTAMYCINE nakuomba kama itawezekana basi nakuomba katika Siku ya Uchaguzi ( ambayo bado hamjaipanga ) tafadhali omba Msaada wa Kiusalama kutoka Kituo cha Polisi Kawe au hata ikibidi hawa Jamaa zangu wana ‘ Medani / Wanajeshi ‘ wasimamie tu hivi Vituo viwili vya MZIMUNI na UKWAMANI kwani kama hili halitotendeka basi tegema taarifa za Watu ‘ Kujeruhiana ‘ vibaya na hata ‘ Kuuana ‘ pia kwani hali si nzuri kabisa.
Heshima yako Mzee Dawa GENTAMYCINE . Mimi nasubiria tu kwa hamu hapo mwezi wa saba mwaka 2020 kama Mungu atanipa pumzi nione namna udiwani na Ubunge utakavyomwaga damu za Wanaccm. Naamini kwasasa CCM wanaona kila kitu ni chao na hawana mpinzani so atakayepita kwenye maoni ana uhakika wa jimbo na ulaji. Hapo watauana. Walahh watauana.
 
Ama kweli kuwa mwana CCM kunahitaji kujikana maani ni aibu
Haswaaaaa. Kuna sehemu fulani walikuwa na wagombea watatu. Wapiga kura wakasema huyo mwingine ni msomi atatusumbua akiwa mwenyekiti. Mwingine wakasema amekuwa kwenye halmshauri ya kijiji kwa miaka 15. Wakampa aliyewanunulia pombe za kienyeji. Mie nikasema kwa mitazamo hii. Safari bado ndefu sana
 
Mkuu unaijua ccm au unaisikia.hapo anaweza akafanya figisu kwa huyo mgombea hadi mtaa ukaenda upinzani.Siasa za ccm za ndani zina fitina hatari.

Na huu Mpango ndiyo nasikia anao huyo Mzee kama sehemu ya Kuwakomoa CCM na Wagombea wake ambao anajua kama Mmoja wapo akishinda tu basi wanaweza Kumfungulia Kesi kadhaa za ' Ufisadi ' ambazo amekuwa akihusishwa nazo Siku nyingi sana pale Kawe akishirikiana na Mzee Mwenzie Meya wa zamani wa Wilaya husika ( jina nalihifadhi ) ambao wote ' wamepiga ' Pesa za Kuuza na Kudhulumu Ardhi na mengineyo. Sifa Kubwa ya huyo Mzee ni ' Uchawi ' wake na ameshawamiza mno ' Maadui ' zake hasa katika ' Gombea ' kama hizi na ndiyo maana anaogopeka sana. Anashirikiana mno na Kijana Mmoja aitwae Poti Poti mwenye Cheo cha Mwenezi wa CCM hapo Mzimuni kwa kufanya ' Fujo ' za Kiuchaguzi na Hila zote ili mradi tu Watu wawili ambao ndiyo wanakubalika na Wananchi wasipote na hata Mmoja wao asifanikiwe.
 
Ni Jana tu nilikua maeneo ya mbezi chini mitaa ya rainbow, kwenye kijiwe cha boda boda nilisikia wakitaja hilo jina la mzee Ngonyani. Walikua wakizungumza fitina za mzee huyo kuwepo madarakani kwa miongo kadhaa... Na dhuluma ya ardhi za watu miaka hiyo ya nyuma. Leo pia nasoma hapa kuhusu huyo mzee, inaonekana kuna jambo

Ni Mzee mwenye ' Kashfa ' nyingi tena za ' Kiupigaji ' kwa Kawe ila bahati mbaya CCM imekuwa ikimlea sana tu na Kumuogopa pengine kutokana na ' Ushirikina ' wake ambao anauamini kuliko Kitu kingine chochote kile. Huko nyuma katika Uchaguzi wa miaka Mitano ( 5 ) iliyopita kuna Kijana Mmoja aitwae Mbozi alishindana nae na alionekana kuwa ni Mshindani mzuri Kwake ila cha Kushangaza Wiki Moja kabla ya Uchaguzi tu huyo Kijana Mbozi Mdomo ulivimba upande Mmoja, Kichwa nacho Kikaongezeka Ukubwa na Meno yake yakiwa yameanza Kuvurugika ndipo akaamua Kujiondoa na alipojiondoa katika ' Kinyang'anyiro ' ndani ya Saa 24 alirudi kuwa mzima kama kawaida. Huwezi amini nasikia huyu Kijana tena Mbozi safari hii nae ameingia tena katika Nafasi ya Kugombea na sijui Kajiamini nini japo mwenyewe kila akiulizwa kuwa amesahau Kuvimbishwa Mdomo, Bichwa lake Kuongezeka Ukubwa ghafla na Meno yake Kukosa mwelekeo Kamili akasema kuwa ametoka Kwao Mbeya hivi karibuni na ameshaaga japo hata Yeye katika Uchaguzi wa Juzi ( ambao unarudiwa ) alichinjiwa mbali na wana CCM wa Mzimuni.
 
Hahaha sawa bwana mkuu

Uwe na usiku mwema ngoja wengine tuingie kazini

Majukumu mema na hakikisha hakipiti Kitu bila Kukijua vyema ili ukiwa unakiandikia Ripoti ya Wiki kwa Mabosi zako wa Makao Oysterbay iwe ni sahihi na uzidi Kuaminika Kiutendaji.
 
Chadema kuna uchaguzi lini wa mwenyekiti?
wabunge vitu maalum wanateuliwaje?
Rushwa za ngono zilikuwa na ukweli?
Kuna vitu vingine ambavyo hata ashuke malaika awe mwenye kiti wa CCM,ndani ya CCM haviwezi vikaisha kwa kuwa ni maisha ya CCM, rushwa ni sehemu ya maisha ya CCM, kuhubiri udini kwa wananchi ni sehemu ya maisha ya CCM, kubambikiza kesi ni sehemu ya maisha ya ccm, wizi wa kura ni sehemu ya maisha ya CCM, ubaguzi kwa wananchi ambao hawakuichagua CCM na katika hili kinara wa ubaguzi ni mwenyekiti wa taifa mwenyewe,n.k.
 
Chadema kuna uchaguzi lini wa mwenyekiti?
wabunge vitu maalum wanateuliwaje?
Rushwa za ngono zilikuwa na ukweli?
Wewe Nabii Tito mambo ya Chadema hayakuhusu
tapatalk_1571921669725.jpeg
 
Kawe kuna wenyeviti wa mitaa wala rushwa sana; safari hii wengi wamekatwa akiwemo yule wa Mbezi Beach A ambaye alikuwa anashirikiana na wauza madawa ya kulevya pamoja na majangili!! Nasikia baada ya jina lake kukatwa anakusanya wafuasi wake na kuandamana eti kuonesha kuwa anakubalika hivyo jina lake lirudishwe!!!Bashiru itabidi akomae hivyo hivyo hawa wanaokichafua chama wakae kando.
 
Eti wanajeshi wasimamie kumbe wako cheap kiasi hivi cha kushirikishwa Mambo ya chama?
 
Kuna watu wangu (wana medani) jirani na Kawe niliwatembelea siku ya Jumapili na wakati huo nilikuwa sijui nini kinaendelea hadi pale wenyeji wangu hao waliponiambia kuwa, ilikuwa ni siku ya kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Nakumbuka nilikuwa eneo hilo la Kawe hadi usiku wa saa tatu ambapo kwa kujiridhisha zaidi ilinibidi nizungukie maeneo mawili muhimu ya kiuchaguzi kwa Kawe ya Mzimuni alipo mkongwe Mzee Ngonyani (ambaye inasemekana alishakatwa na hatakiwi kugombea tena ila ndiyo kinara wa fitina zote akisaidiwa na Mwenezi wake aitwae Poti Poti ) na Ukwamani alipokuwa kijana makini Sultani Jeta (ambaye kwa bahati mbaya alisema kuwa hatogombea tena kwa sababu zake binafsi).

Mheshimiwa Katibu Mkuu wa CCM sitaki kujua ‘ vimbwanga ‘ vya maeneo mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam vilivyotokea hiyo juzi (Jumapili ) ila kwa kilichotokea katika haya maeneo ya Mzimuni na Ukwamani ‘ nimekitathmini ‘ kwa kina na kugundua kuwa kama wana CCM hasa nyie mlio ngazi za juu msipokuwa makini, basi kuna hatari mwakani vyama vya upinzani vikashinda na hamtoamini macho na masikio yenu.

Haya ni baadhi ya mambo niliyopata kutoka hayo maeneo ya Kawe Mzimuni na Ukwamani:

Rushwa za wazi wazi wana CCM kwa wana CCM

Usaliti wa wana CCM uliopitiliza

Fujo ambako kuna muda wana CCM walikuwa wakionyesha kuwa hata wao fani ya ubondia wanayo pia.

Ushirikina wa wazi wazi na kuna mtu mmoja wa Kawe Mzimuni ‘Mkongwe' ambaye nimemtaja hapo juu anajulikana na kuogopeka sana ‘Kiuchawi' kwani na ‘Uchawi ‘ wenyewe nao anaujua mno, kasema kwa kuwa jina lake mlilikata huko juu kwa juu basi na yeye hakubali na ataondoka na mtu ‘ kindumba' kiasi kwamba kuna baadhi ya watu (Wagombea) makini sasa wanatafakari kujitoa kwa ‘kumuogopa' huyo Mzee ambaye amedumu hapo Mzimuni kwa miaka takribani 20 ila ameshindwa tu hata kuitafutia gari ya wagonjwa Hospitali ya Shamba Kawe ambayo ipo mita chache na ofisi yake.

Upandikizaji wa watu ambako inasemekana kuna Mbunge mmoja (jina kapuni) aliandaa watu wake ambao wengine walikuwa ni wa Kiume ila walivalia ‘ Hijab' na waliletwa na Usafiri wa Bajaji (ambao aliwahonga pesa nzuri tu) ili waje wawapigie Kura za Maoni hao Wagombea wa CCM ambao huyo Mbunge ‘ Fulani ‘ anawamudu ili kama kawaida mwakani awatumie tena katika Kukisaliti Chama na aweze Kupita kama ambavyo baadhi yao walimsaidia huko nyuma ( bado nasisitiza kuwa hii ni Tetesi kwani hata Mimi GENTAMYCINE basi sijaithibitisha wala kuiamini kwa 100% )

Vitisho kwa baadhi ya wana CCM wa hayo maeneo kwamba kama hawatowapigia Kura basi Wao wakitumia Ujanja wao na kupita watakuja ‘ Kuwakoma ‘ na lazima tu watawafanyia tu Kitu mbaya. Na wengi wanaotishiwa hivi ni wale wana CCM ambao wanaendesha Bishara zao katika Soko la Kawe lile la Ukwamani na hili jipya lilipo Mzimuni pamoja na wale wengine waliopo mazuri kwa ‘ Fursa ‘ za Kibiashara.

Nikupongeze pia Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally kwa ‘ Kuamuru ‘ Uchaguzi huu wa ndani wa CCM urejewe / urudiwe baada ya hizo ‘ Sarakasi ‘ ila kupitia tu huu Uzi wangu GENTAMYCINE nakuomba kama itawezekana basi nakuomba katika Siku ya Uchaguzi ( ambayo bado hamjaipanga ) tafadhali omba Msaada wa Kiusalama kutoka Kituo cha Polisi Kawe au hata ikibidi hawa Jamaa zangu wana ‘ Medani / Wanajeshi ‘ wasimamie tu hivi Vituo viwili vya MZIMUNI na UKWAMANI kwani kama hili halitotendeka basi tegema taarifa za Watu ‘ Kujeruhiana ‘ vibaya na hata ‘ Kuuana ‘ pia kwani hali si nzuri kabisa.
Uko vizuri Sana na kwangu haya nikiyategemea maana watoa rushwa ni wababe kuliko watu makini
Watu wameona majina yao hayajarudi hivyo fujo ni lazima ok la watazoea tu na kuelewa
 
Ccm toka lini waliendesha uchaguzi huru ndani ya chama?uchaguzi huru wa ndani

umesahau Magufuli kupata 100% kule Dodoma?
Sasa kama CCM hawajawahi kuendesha uchaguzi huru wa ndani, ni chama gani kimewahi kuendesha uchaguzi huru?
 
Back
Top Bottom