Dkt. Bashiru Ally, Mjamaa aliyeshindwa kutuonesha ujamaa kwenye Uchaguzi

Kijana wa falsafa ya Mwalimu Nyerere ya Kijamaa anaposhiriki dhambi ya wizi wa kura tena waziwazi bila kificho katika uchaguzi mkuu ni hatari kubwa !! ni hatari kubwa!

Ni nani basi aliyebakia atakayetetea falsafa ya mwalimu kwa vitendo?
 
Eti wanataka Tanzania ifuate mfumo wa China. China wana miaka zaidi ya 5000 ya kujitawala wale, wana experience ya kufa mtu kwenye mambo ya kuendesha nchi yao!, eti CCM wanataka kujilinganisha nao.
Miaka 5000 huanza na mwaka mmoja, tutafika tu huko kwenye Chama Cha Kikomunist, dalili ni nzuri maana ni CCM tu iliyo na mfumo dhabiti wa kupika na kuandaa viongozi! Saccos ya Mbowe ina jifia yenyewe taratibu baada ya mlija wa ruzuku kukatika!
 
Hawa waliopatikana kwenye kura za maoni kwa rushwa kisha wakashindishwa kwa kura za kwenye vikapu?

Hakuna chama pale!
 
Mkuu unaelewa vizuri hata maana ya Control of Market Forces, Command Economy and Economic Planning ???
Ungekuwa unafahamu basi usingenitolea huu mfano usio na kichwa wala miguu hapa, maana hata nchi za kibepari huwa zinafanya Blocks to IPO Auctions, Blocks to Mergers and Acquisitions au kulazimisha kampuni kufanya IPO. Hili swala liko kiuchumi na kisheria zaidi na hata sielewi utaliwekaje kunithibitishia kwamba hichi kilichofanyika ndiyo Uchumi wa Kijamaa.

Sababu za mamlaka husika kuzuia IPO-Auction and Listings huwa ni nyingi lakini kubwa na za kisheria huwa ni Usalama (National Security), Ushindani ( Fair Competition and Anti-Trust Laws) na Rushwa kwa makampuni yanayouza hisa. Hili la kupinga IPO ya Ant Group halijaanzia Uchina bali limeanzia Marekani ambako baadhi ya wawakilishi wao kama Marco Rubio alishauri serikali ipinge IPO ya Ant kwasababu ya sheria za Ushindani (Anti Trust Laws): Kwa Marekani IPO ya Ant Group itayaumiza mabenki yao.

Haya sasa sema jingine, ukishindwa endelea kumfanyia Raisi Magufuli Ibada ya sifa na kuabudu............
Wajuwaji ni wengi na wewe unaonekana ni mmoja wapo, ila kwa haya ya China inaonyesha China yako ni ya kusoma kwenye vitabu na magazeti.

Hivi kuna nchi duniani itacha tu market to go wild and risk inflection or deflation? Kuna kiwango ambacho serikali au regulators wanaweza kuachia soko liamue kwenda juu au chini, na ni kwakiwango gani. Unachosema wewe eti serikali ya China ni ya kijamaa lakini ikija swala la biashara, basi wanaachiwa soko ndio liamue, that is an illusion. Ingekuwa hivyo makampuni ya West yasingekuwa yanalalamika the amount of regulations they've to go through. Hata makampuni ya ndani hawawezi kuzalisha and flood the market bila ridhaa ya serikali.

Kuna vitu vinne vinavyo fanya market forces iwepo, Gov, international trade, speculation, supply 'n' demand. Kila kimoja kina muhitaji mwenzake ili kitimize malengo yake. Serikali haiwezi kuamua bei huku hakuna mwenye uwezo wa kununua kwa bei hiyo au ishushe bei kiasi kwamba mfanyabiasha ana pata hasara. Upande mwingine hivyo hivyo soko haliwezi kulazimisha bidhaa iwepo sokoni bila kibali cha serikali au mdhibiti.

Halafu hii notion ya kusema serikali ya kijamaa ndio tatizo ni upuzi wa kishamba sana. Nchi nyingi tuu dunini kuanzia New Zealand, Australia, South Africa, all EU states, USA, Canada, Latin America etc zina vyama vya kijamaa na vingine vinaongoza serikali hivi sasa.
 
Unaniita mimi mjuaji halafu umeokoteza mavitu kutoka mtandaoni ambayo hata huyaelewi. Huu ndiyo ukilaza wenyewe sasa. Ndani ya mfumo Communist Command Economy/Planned Economy haya mambo unayoyataja hayapo kabisa: Kama yapo ntajie walau nchi moja basi. Rules of Demand & Supply and Speculation hazipo kwenye Command Economy. Katika uliyoyataja vilivyopo ni viwili tu, Government and International Trade vikiendeshwa kwa ruzuku.

kila kitu hupangwa, huzalishwa, kuendeshwa na kuuzwa na serikali kwa dhumuni la matumizi ya raia na siyo kupata faida (Surplus and Profit). Narudia tena kukwambia hili na likukae vizuri akilini mwako: Rules of Demand and Supply hazitumiki kabisa kwenye Uchumi wa kijamaa (Command and Planned Economy). Ukisema haya mbele za watu utadharaulika.

Uchina na Urusi Command and Planned Economy ziliwashinda ndiyo maana Raisi Deng Xao Ping akaamua kuruhusu soko huria na uwekezaji miaka ya 1979-1980, huku Urusi akiangukia pua mwaka 1991. Unavyosema serikali haiwezi kupanga bei, kulazimisha na kuamua ni bidhaa ipi iwepo sokoni basi napata shaka sana na shule uelewa wako, maana mifano iko dhahiri. Huu ndiyo ulikuwa mfumo wa Tanzania kipindi cha Nyerere: No rules of Demand and Su

Halafu hii notion ya kusema serikali ya kijamaa ndio tatizo ni upuzi wa kishamba sana. Nchi nyingi tuu dunini kuanzia New Zealand, Australia, South Africa, all EU states, USA, Canada, Latin America etc zina vyama vya kijamaa na vingine vinaongoza serikali hivi sasa.
Hapa ndiyo umeudhihirishia ulimwengu wote ukilaza wako na mabonde matupu yaliyopo kichwani kwako. Siyo kila Ujamaa ni Umarki (No every socialist government is Marxist). Ujamaa unaofanywa Ulaya ni ule uitwao Social Democracy na siyo Marxism au Marxist Socialism wa wakina Mao, Lenin na Mzee Nyerere. Social Democracy hata Marekani upo na unafanywa kupitia kitu kiitwacho The Welfare State.

Ulianza kutumika Ulaya na kanisa Katoliki hata kabla ya Umarksi (Marxism/Marxist Socialism) kuzaliwa. Haya mambo hata watoto wa sekondari kule Chato wayanafahamu, lakini wewe kilaza muimba sifa yamekupita kushoto.

Haya leta na lingine tena, ukishindwa endelea kufanya Ibada ya Sifa na Kuabudu kwa mungu John Magufuli........
 
Kila mstari nikisoma ni kejeli matusi na dharau, inaonyesha tatizo liko kwenye upangaji wa hoja zaidi kuliko kwenye kujibu hoja.

Rudi kwenye hoja yako ya kwanza hapa chini, kwamba China ujamaa upo kwenye mgawanyo wa rasilimali na sio kwenye uendeshaji masoko.

Hata kule nchini Uchina, Ujamaa uko tu kwenye mgawanyo wa rasilimali (distribution of wealth) na siyo kwenye uendeshaji wa masoko (control of market forces): Command Economy nao iliwashinda.

Swali langu kwako ambalo umelikwepa kwa kuandika riwaya ndefu, kuna nchi yoyote duniani imaachia market to control the prices 100% bila kuwa na usimamizi? Na kama ipo wanawezaje kudhibiti mfumuko wa bei? (Inflation). Ikiwa serikali au benki kuu inauwezo wa kupanga riba za mikopo, kitu ambacho kimaweza kulazimisha bei za bidhaa kupanda au kushuka. (If you control interest rate, you control the market.)

kila kitu hupangwa, huzalishwa, kuendeshwa na kuuzwa na serikali kwa dhumuni la matumizi ya raia na siyo kupata faida (Surplus and Profit). Narudia tena kukwambia hili na likukae vizuri akilini mwako: Rules of Demand and Supply hazitumiki kabisa kwenye Uchumi wa kijamaa (Command and Planned Economy). Ukisema haya mbele za watu utadharaulika.

Uchina na Urusi Command and Planned Economy ziliwashinda ndiyo maana Raisi Deng Xao Ping akaamua kuruhusu soko huria na uwekezaji miaka ya 1979-1980, huku Urusi akiangukia pua mwaka 1991. Unavyosema serikali haiwezi kupanga bei, kulazimisha na kuamua ni bidhaa ipi iwepo sokoni basi napata shaka sana na shule uelewa wako, maana mifano iko dhahiri. Huu ndiyo ulikuwa mfumo wa Tanzania kipindi cha Nyerere: No rules of Demand and Su

Hapa ndiyo umeudhihirishia ulimwengu wote ukilaza wako na mabonde matupu yaliyopo kichwani kwako. Siyo kila Ujamaa ni Umarki (No every socialist government is Marxist). Ujamaa unaofanywa Ulaya ni ule uitwao Social Democracy na siyo Marxism au Marxist Socialism wa wakina Mao, Lenin na Mzee Nyerere. Social Democracy hata Marekani upo na unafanywa kupitia kitu kiitwacho The Welfare State.

Ulianza kutumika Ulaya na kanisa Katoliki hata kabla ya Umarksi (Marxism/Marxist Socialism) kuzaliwa. Haya mambo hata watoto wa sekondari kule Chato wayanafahamu, lakini wewe kilaza muimba sifa yamekupita kushoto.

Haya leta na lingine tena, ukishindwa endelea kufanya Ibada ya Sifa na Kuabudu kwa mungu John Magufuli........

Hapa juu umeweka maelezo mengi sana ambayo sidhani kama yanasaidia kujibu hoja yako. Kupitia maelezo yako, je Tanzania bado ni Marxist Socialism? Ambapo kila kitu kinapanga na kuzalishwa na serikali? Maana hii ndio ilikuwa argument yako ya kwanza kwamba China's socialism iko kwenye wealth distribution na sio kwenye market forces, Tanzania tuko upande gani? Labda ukienda mbali zaidi, kuna nchi kwenye dunia ya leo ambayo bado ni Marxist ikiwa hata North Korea na Cuba wana private sector which is slowly picking up the pace.
 
Swali langu kwako ambalo umelikwepa kwa kuandika riwaya ndefu, kuna nchi yoyote duniani imaachia market to control the prices 100% bila kuwa na usimamizi? Na kama ipo wanawezaje kudhibiti mfumuko wa bei? (Inflation). Ikiwa serikali au benki kuu inauwezo wa kupanga riba za mikopo, kitu ambacho kimaweza kulazimisha bei za bidhaa kupanda au kushuka. (If you control interest rate, you control the market.)
Uchina kuna sekta binafsi ambayo inasimamiwa na hizi mamlaka, zikifanya kazi kama kusimamia ushindani na kuhakikisha zinadhibiti mfumuko wa bei. Nini kizalishwe, kiuzwe wapi na kwa kiasi gani hilo siyo la serikali, watu wana uhuru wa kufanya watakacho: Tofauti kabisa na miaka ya nyuma ambapo serikali ya ndugu yenu Mao Zedong ilikuwa ndiyo inaamua nini kizalishwe, kiasi cha uzalishaji na kiuzwe wapi huku wakicheza na mbinu ya kutoa ruzuku.

Uchina ya leo Ujamaa unaonekana sana sehemu kuu mbili: Katika Siasa na katika falsafa ya ugawanyaji wa keki ya taifa. Sekta binafsi inafanya kazi, watu wanatozwa kodi kubwa ambazo zinaenda kutumika kuwasaidia wachina wengine milioni hamsini ambao wako kwenye umasikini: Hili ni jambo la nadra sana kulikuta kwenye nchi za kibepari kama Uingereza na Marekani ambao hupenda kutumia The Keynesian Economic Model ambapo the more you get rich the less you are taxed. Ndiyo maana nikasema hivi "Uchina Ujamaa uko kwenye distribution of wealth na siyo control of market forces".Wengine huita Uchina A Mixed Economy: Hapa sasa unakomaa nini ???

Hilo la Uchina Blocking of ANT IPO ni suala za usimamizi na uelekezi (Regulatory Actions) na siyo suala za kuendesha Uchumi (Command of the Economy) na wala sielewi kwanini ulilileta.Unajikanyaga mwenyewe na kutengeneza Straw-Men: Sheria na kanuni za kimataifa kama zile za WTO, WB na IMF zinataka kila nchi iwe na mamlaka za kudhibiti Uchumi wa nchi, ili Uchumi uwe na afya (These are International Standards and have got nothing to do with being a mrxist).

Ndiyo maana zinataka kuwe na mamlaka za ushindani zikisimamia Capital Markets, mamlaka za ukusanyaji wa kodi na taasisi nyingine za kifedha kama mabenki na benki kuu ili kutoa mikopo, kutengezea sarafu, kulinda sarafu na kusimamia mwelekeo mzima wa uchumi wa nchi.

Hapa juu umeweka maelezo mengi sana ambayo sidhani kama yanasaidia kujibu hoja yako. Kupitia maelezo yako, je Tanzania bado ni Marxist Socialism? Ambapo kila kitu kinapanga na kuzalishwa na serikali? Maana hii ndio ilikuwa argument yako ya kwanza kwamba China's socialism iko kwenye wealth distribution na sio kwenye market forces, Tanzania tuko upande gani?
Tanzania ni taifa lisilo na dira wala falsafa yoyote ile ya kiuchumi, leo tuko huku kesho kule muhimu tu maisha yaende.
We are simply a corrupt, ramshackle oligarchic state ruled my military discipline and terror.
Labda ukienda mbali zaidi, kuna nchi kwenye dunia ya leo ambayo bado ni Marxist ikiwa hata North Korea na Cuba wana private sector which is slowly picking up the pace.
Private Sectors zipi hizo za Korea Kaskazini ambazi zina "Slowly picking up the pace" ???
Naomba ututajie walahu tatu tu.
 
Miaka 5000 huanza na mwaka mmoja, tutafika tu huko kwenye Chama Cha Kikomunist, dalili ni nzuri maana ni CCM tu iliyo na mfumo dhabiti wa kupika na kuandaa viongozi! Saccos ya Mbowe ina jifia yenyewe taratibu baada ya mlija wa ruzuku kukatika!
CCM hii ya kura za lumbesa kwenye vikapu ndo yakutufikisha mahali pazuri?
 
Uchina kuna sekta binafsi ambayo inasimamiwa na hizi mamlaka, zikifanya kazi kama kusimamia ushindani na kuhakikisha zinadhibiti mfumuko wa bei. Nini kizalishwe, kiuzwe wapi na kwa kiasi gani hilo siyo la serikali, watu wana uhuru wa kufanya watakacho: Tofauti kabisa na miaka ya nyuma ambapo serikali ya ndugu yenu Mao Zedong ilikuwa ndiyo inaamua nini kizalishwe, kiasi cha uzalishaji na kiuzwe wapi huku wakicheza na mbinu ya kutoa ruzuku.

Uchina ya leo Ujamaa unaonekana sana sehemu kuu mbili: Katika Siasa na katika falsafa ya ugawanyaji wa keki ya taifa. Sekta binafsi inafanya kazi, watu wanatozwa kodi kubwa ambazo zinaenda kutumika kuwasaidia wachina wengine milioni hamsini ambao wako kwenye umasikini: Hili ni jambo la nadra sana kulikuta kwenye nchi za kibepari kama Uingereza na Marekani ambao hupenda kutumia The Keynesian Economic Model ambapo the more you get rich the less you are taxed. Ndiyo maana nikasema hivi "Uchina Ujamaa uko kwenye distribution of wealth na siyo control of market forces".Wengine huita Uchina A Mixed Economy: Hapa sasa unakomaa nini ???

Good, angalau unakubali kama hakuna nchi inaweza kuachia market iwe na kauli ya mwisho kwenye masuala ya uchumi. Ila mifano uliotoa ya Uingereza na Marekani kwamba zinafuata Keynesian Economic Model si za kweli, some elements za hiyo theory walizibwaga siku nyingi only applying them when there is need like economic shock 2008 or current pandemic. Na sidhani kama China wana lipa kodi kubwa kuliko nchi za West, mfano nchi ya Uingereza mwenye kipato cha £45,000 na zaidi ana nalipa kodi 45% kulinganisha na mtu wa uchina anyepata kipato hicho hicho analipa 30%. Nchi za West ndio zinaongoza kusaidia wanachi wao kupitia ruzuku (subsidies), and nyongeza kwenye vipato vya chini (tax credit). Sasa kwa mtazamo wako sijuwi nani anayeendesha nchi kijamaa kati ya China na western countries.

Hilo la Uchina Blocking of ANT IPO ni suala za usimamizi na uelekezi (Regulatory Actions) na siyo suala za kuendesha Uchumi (Command of the Economy) na wala sielewi kwanini ulilileta.Unajikanyaga mwenyewe na kutengeneza Straw-Men: Sheria na kanuni za kimataifa kama zile za WTO, WB na IMF zinataka kila nchi iwe na mamlaka za kudhibiti Uchumi wa nchi, ili Uchumi uwe na afya (These are International Standards and have got nothing to do with being a mrxist).

Ndiyo maana zinataka kuwe na mamlaka za ushindani zikisimamia Capital Markets, mamlaka za ukusanyaji wa kodi na taasisi nyingine za kifedha kama mabenki na benki kuu ili kutoa mikopo, kutengezea sarafu, kulinda sarafu na kusimamia mwelekeo mzima wa uchumi wa nchi.
Sasa ukizungumzia suala la ANT IPO kuwasimamisha na ukasema halana uhusianio na uendeshaji wa uchumi inashangaza kidogo. IPO halikuwa iwe floted dunini kote na uwezekano wa kileta pesa nyingi ndani ya China ulikuwa mkubwa lakini hivyo hivyo pesa nyingi ingeza kutoka nje na kupunguza thamani ya pesa ya ndani. Pamoja ANT group inajushulisha na teknolojia, ina jihusisha na biashara ya fedha ikiwa pamoja na mikopo kwa watu binafsi and SME. kama serikali haikuwajiridhisha, na kibaya kutokea, watu wengi wangeweza kupoteza vipato vyao. Sasa kama haya ya serikali kuingilia biashara hayamna uhusiano na Command Economy, sijuwi unamaanisha nini.
Tanzania ni taifa lisilo na dira wala falsafa yoyote ile ya kiuchumi, leo tuko huku kesho kule muhimu tu maisha yaende.
We are simply a corrupt, ramshackle oligarchic state ruled my military discipline and terror.

Private Sectors zipi hizo za Korea Kaskazini ambazi zina "Slowly picking up the pace" ???
Naomba ututajie walahu tatu tu.
Mtazamo wako wa Tanzania uko nje ya reli, huwezi kusema Tanznia hatuna dira ya kiuchumi huku uchumi unapanda kwa wastani wa 6%. kwani kuna mtu hapa Tanzania amekatazwa kufanya biashara yoyote ya halali? au ni watu wenyewe ndio hawachangamkii fursa? kauli kama corrupt, ramshackle etc ni kauli nyepesi za vijana wasiopenda kufunguwa macho na kukimbilia fursa, wanategemea mtu aje awashike mkono na kuwapa kazi. vijana wengi ni wepesi kupenda vya jirani na kudharau kilicho karibu yao.

SME in North Korea inatoa ajira kwa nusu ya wananchi, sekta ya mawasiliano, IT, viwanda hata madini zimeingia ubia na kampuni za nje mainly Chinese and Europian. kampumi kama VEON kwenye simu, au Nosotek kwenye IT, Kuna kampuni za South korea na China wamefunguwa indutries kwenye SEZ

Hata yule (mzee kijana kwa sura) kipindi kile ziko timamu hajanywa maji ya rangi ya kijani, alisema.
"Uchaguzi ukiwa huru na wa haki ccm ijiandae kukabidhi ikulu"
Aliamini hivyo na ndiyo ilivyo hata leo ,ila njaaa , njaaa njaaa, ni ya kuisikia tu kwa mwenzio.

Sio kila aokotae chakula ni kichaa, wengine ni tumbo humtuma kufanya matendo kama kichaa .
Hahahahaaaaa
 
Hata kule nchini Uchina, Ujamaa uko tu kwenye mgawanyo wa rasilimali (distribution of wealth) na siyo kwenye uendeshaji wa masoko (control of market forces): Command Economy nao iliwashinda.
Mkuu, za masiku kidogo.

Hapa nimeona nichangie kidogo.

Nadhani si sawa usemayo kwamba China wameshindwa kwenye kudhibiti market forces.

Hawa jamaa walinza kuutengeneza uchumi wao tangu 1978 na tokea hapo uchumi wao umekuwa wasimama kwenye asilimia 6.

Ila hadi sasa uchumi wa China umekuwa ni wa kubadilika mara kwa mara yaani diversified economy huku wakiwa ni moja ya wachezaji wakuu kwenye international market.

Sekta kubwa inayowabeba wachina ni viwanda na ni viwanda khasa kuanzia retail, mining, steel, textiles, automobiles, energy generation, green energy, banking, electronics, telecommunications, real estate, e-commerce na tourism.

China tangu mwaka 2010 iliipita Marekani na kuwa namba 1 kwenye viwanda, tangu mwaka 2012 imekuwa ya 2 kwa kutengeneza high tech products.

Pia duniani China ni ya pili kwa maduka makubwa yaani retail market na mwaka 2019 imekuwa na largest market share in the world na yaongoza kwenye e-commerce (Alibaba na Ali express) na zingine za kichina.

Mwisho, China yaongoza duniani kwa kutengeneza magari ya kutumia battery (malighafi yaitwayo Cobalt yatoka Congo DRC na Zambia) yale ya BEV na PHEV ambayo wachaji hizo battery anywhere penye charger.

Sema chama cha kikomunisti ndicho kimeweka sera ya kuwa na mixed economy ambayo inaangaliwa na chama.

Pia kuna special economic Zones kwa ajili ya kusambaza utajiri kwa wachina wajasiriamali.

Hivyo basi uchumi umelalia kwenye kitu chaitwa private property ownership ambapo waweza kutafsiri kuwa ni state capitalism.

Yaani hapa zile nyanja kuu za uchumi zinakuwa chini ya serikali lakini private enterprise zinashamiri.

Kwenye hii ya "private enterprise" ndipo serikali imeshindwa kwa kuwa wengi waliomo humo ni mafisadi na wako kuitumbua serikali kwa kukwepa kulipa kodi stahidi.

Hawa wakiwa well structured basi wataweza kufanya biashara zao katika uhuru kamili bila kuona kwamba kulipa kodi ni kama kwenda kituo cha polisi.
 
Kijana wa falsafa ya Mwalimu Nyerere ya Kijamaa anaposhiriki dhambi ya wizi wa kura tena waziwazi bila kificho katika uchaguzi mkuu ni hatari kubwa !! ni hatari kubwa!

Ni nani basi aliyebakia atakayetetea falsafa ya mwalimu kwa vitendo?
Ni aibu kubwa, hii maana yake ni unafiki uliokubuhu!
 
Walienda shule kukariri hao, hawana msaada kwa Afrika na watu wake!
Kwa kiwango kikubwa sana Africa inaangushwa na kizazi ilichokitengeneza yenyewe baada ya uhuru, ilitengeneza kizazi cha ill-Discplined militants walioshiriki kufanya mapinduzi everywhere, ikazalisha despot politicians, ikazalisha corrupt politicians at the same time ikazalisha incompetent and subservient public servants and weak public institutions.

Why kizazi walichokitengeneza wazungu kilikuwa patriotic zaidi mpaka kufikia hatua ya kupigania uhuru ?

What went wrong with Africa after independence ?
 
Mkuu, za masiku kidogo.

Hapa nimeona nichangie kidogo.

Nadhani si sawa usemayo kwamba China wameshindwa kwenye kudhibiti market forces.

Hawa jamaa walinza kuutengeneza uchumi wao tangu 1978 na tokea hapo uchumi wao umekuwa wasimama kwenye asilimia 6.

Ila hadi sasa uchumi wa China umekuwa ni wa kubadilika mara kwa mara yaani diversified economy huku wakiwa ni moja ya wachezaji wakuu kwenye international market.

Sekta kubwa inayowabeba wachina ni viwanda na ni viwanda khasa kuanzia retail, mining, steel, textiles, automobiles, energy generation, green energy, banking, electronics, telecommunications, real estate, e-commerce na tourism.

China tangu mwaka 2010 iliipita Marekani na kuwa namba 1 kwenye viwanda, tangu mwaka 2012 imekuwa ya 2 kwa kutengeneza high tech products.

Pia duniani China ni ya pili kwa maduka makubwa yaani retail market na mwaka 2019 imekuwa na largest market share in the world na yaongoza kwenye e-commerce (Alibaba na Ali express) na zingine za kichina.

Mwisho, China yaongoza duniani kwa kutengeneza magari ya kutumia battery (malighafi yaitwayo Cobalt yatoka Congo DRC na Zambia) yale ya BEV na PHEV ambayo wachaji hizo battery anywhere penye charger.

Sema chama cha kikomunisti ndicho kimeweka sera ya kuwa na mixed economy ambayo inaangaliwa na chama.

Pia kuna special economic Zones kwa ajili ya kusambaza utajiri kwa wachina wajasiriamali.

Hivyo basi uchumi umelalia kwenye kitu chaitwa private property ownership ambapo waweza kutafsiri kuwa ni state capitalism.

Yaani hapa zile nyanja kuu za uchumi zinakuwa chini ya serikali lakini private enterprise zinashamiri.

Kwenye hii ya "private enterprise" ndipo serikali imeshindwa kwa kuwa wengi waliomo humo ni mafisadi na wako kuitumbua serikali kwa kukwepa kulipa kodi stahidi.

Hawa wakiwa well structured basi wataweza kufanya biashat zao katika uhuru kamili bila kuona kwamba kulipa kodi ni kama kwenda kituo cha polisi.
Unamaanisha nini unaposema " State Capitalism "?
 
Good, angalau unakubali kama hakuna nchi inaweza kuachia market iwe na kauli ya mwisho kwenye masuala ya uchumi. Ila mifano uliotoa ya Uingereza na Marekani kwamba zinafuata Keynesian Economic Model si za kweli, some elements za hiyo theory walizibwaga siku nyingi only applying them when there is need like economic shock 2008 or current pandemic.

Unaendelea kutengeneza Straw-Men na kuzidi kuniwekea maneno ambayo siyo yangu. Ninaposema kudhibiti Uchumi na Masoko it's by the virtue of regulating and controlling how goods and services flow within the markets, & ensuring compliance to monetary and fiscal policies which are pivotal for controlling the inflation. Hili ni tofauti kabisa na uchumi wa kupangwa "This is different from Economic Planning". Nadhani dhana hii ya Economic Planning imekuwa ngumu kwako kung'amua.

Pili, unajikanganya mwenyewe unaposema Marekani wameacha kutumia Keynesian Economic Model siku nyingi (Bila kutaja ni lini), lakini wanatumia tu pale ambapo panakuwa na uhitaji. Huu uchambuzi wako unashida kwasababu kama maraisi wa Marekani kuanzia Ronald Reagan hadi Donald Trump wametumia baadhi ya kanuni za Keynesian Economic Model: Massive Government Spending especially in the military & Infrastructure, Massive Tax Cuts & Tax Rebates, and Stimulus Packages.

Labda ulikuwa unamaanisha nini uliposema Marekani ameacha muda mrefu kutumia Keynesian Economic Model wakati mifano hai mbali na utoaji wa Stimulus Packages ipo mingi ???
Na sidhani kama China wana lipa kodi kubwa kuliko nchi za West, mfano nchi ya Uingereza mwenye kipato cha £45,000 na zaidi ana nalipa kodi 45% kulinganisha na mtu wa uchina anyepata kipato hicho hicho analipa 30%. Nchi za West ndio zinaongoza kusaidia wanachi wao kupitia ruzuku (subsidies), and nyongeza kwenye vipato vya chini (tax credit). Sasa kwa mtazamo wako sijuwi nani anayeendesha nchi kijamaa kati ya China na western countries.
Mosi, hizi takwimu zako hazina ukweli wowote kwasababu Uchina siku hizi nao wana Progressive Taxes, ambayo huanzia asilimia 3% hadi kufika 45% kwa wenye kipato kikubwa. Hilo la asilimia 30% wewe umelitoa wapi ???

Pili, Uchina mwaka 2018 amevunja rekodi kwa kutoa ruzuku ya dola za kimarekani bilioni 22 (Ambazo ni zaidi ya trilioni arobaini za kitanzania) kwa makampuni yake. Sasa unaposema mataifa ya Magharibi ndiyo yanaongoza kutoa ruzuku kuliko Uchina halafu hujaniwekea ushahidi nadhani hoja yako inakuwa iko mufilisi kabisa. Huu ndiyo umekuwa ugomvi mkubwa baina ya Uchina na Marekani kule WTO.

Mtazamo wako wa Tanzania uko nje ya reli, huwezi kusema Tanznia hatuna dira ya kiuchumi huku uchumi unapanda kwa wastani wa 6%.
Hebu niambie wewe: Tanzania inafuata dira gani ya kiuchumi inayofanya nchi ikue kwa asilimia 6%

SME in North Korea inatoa ajira kwa nusu ya wananchi, sekta ya mawasiliano, IT, viwanda hata madini zimeingia ubia na kampuni za nje mainly Chinese and Europian. kampumi kama VEON kwenye simu, au Nosotek kwenye IT, Kuna kampuni za South korea na China wamefunguwa indutries kwenye SEZ
Hayo makampuni ya Korea Kaskazini yaliyoingia kwenye ubia na mashirika ya nje yanamilikiwa na nani ???
 
Back
Top Bottom