Dkt. Bashiru Ally, Mjamaa aliyeshindwa kutuonesha ujamaa kwenye Uchaguzi

Bado upo kwenye State Control kwa kiwango kikubwa sana: Japo kinachofanya uchumi wake uwe ni wa tofauti na wa kipekee ni kuanzisha baadhi ya nyenzo za soko huria. Hapa tutazungumzia mambo kama umiliki binafsi wa baadhi ya nyenzo za uzalishaji na uwekezaji mkubwa wa kimataifa.
Wamewezaje kuintergrate hii mifumo wakati huku kwetu state run enterprises haziwezi kushindana sokoni na zinaishia kuzalisha Corrupt CEOs ?
 
Waweza kusema hivyo lakini tafsiri halisi ni kama alivyoeleza mkuu Lumumba.

Yaani pia uchumi wa China waweza kuitwa ni ujamaa wenye tabia za kichina yaani Socialism with Chinese Characteristics.

Ni "mixed Socialist market economy" ambapo enterprises zinamilikiwa na serikali na biashara zote za ndani na nje zote watumia mpango wa kiuchumi kutoka kwenye chama cha kikomunisti cha China.

Ndo maana nikasema somasoma kitabu cha hawa mazee Karl na Friedrich upate madini mchanganyiko.

Ukipata wasaa.
Ukipewa dhamana ya uongozi China na ufanye ubadhirifu wa mali ya umma, adhabu yake ni kifo.
 
Ila benki zao zinazokuja huku Afrika hawaleti Capital ya kutosha.

Kuna benki yao moja imetiwa kapuni na BOT juzijuzi.
Mkuu Richard mazingira ya uwekezaji nchini kwetu na sehemu nyingi barani Afrika ni mazuri sana lakini hayatabiriki.
Bado hatujakomaa na tunakuwa na kawoga fulani kakuhisi kwamba kila mtu anataka kutuibia. This neurosis is justified, considering Africa's background with foreigners who came as missionaries and traders later turned masters. Sisi tuliopewa neema na Mungu ya kuzaliwa hiki kizazi hatutakiwi kuogopa na kuwa na mawazo kama wale wazee wa miaka ya 70 na 80. Ifike mahali tubadilike.......
 
Ni kweli mazingira hayatabiriki kwa sababu mbili kuu.

1. Wawekezaji si wawekezaji halisi na wapo kwa ajili ya kupata faida za harakaharaka na kutaka tax break za miaka mingi.

2. Baadhi ya viongozi wa Afrika au wale walo chini yao kuwa ndumilakuliwi khasa pale wanapofanya negotiations na wawekezaji.

Ni hapo Mchina anapotushinda, yeye kaweka sera za kiuchumi na ni lazima zifuatwe ila ni sera rafiki tu.

Sasa sisi ni kodi inasumbua sana wawekezaji tukifanikiwa hili la kodi tutakuwa sawa.

Kwa mfano serikali ingewaruhusu watanzania wenye uwezo kufanya joint venture na wawekezaji wa kigeni kwenye maeneo kama migahawa kama McDonald's, KFCs na Nandos.

Hivyo hawa wawaweka kwenye kundi maalum lenye kodi maalum.

Si lazima wawe ni wahindi tu kwenye kila kitu.

Hata wabantu nao wajitahidi ili waajiri wabantu wenzao na hapo soko la ajira linakuwa linapanuka.

Ndo maana naona watu kama Charles Kimei wanafaa kwenye biashara kwamba wana maono ya mbali kwenye masuala kama kuboresha micro economies.

Hata hizi reli zinazojengwa ni fursa kubwa sana ya kibiashara kwa mtu anaefahamu kupanga uchumi na sera.
 
Wamewezaje kuintergrate hii mifumo wakati huku kwetu state run enterprises haziwezi kushindana sokoni na zinaishia kuzalisha Corrupt CEOs ?
Mkuu tatizo letu liko kimfumo zaidi na tumegoma kubadilika: Tunapenda kuendesha kila kitu kisiasa. Uarabuni wana State Run Enterprises lakini wamefanikiwa sana kuziendesha kwasababu waliamua kuruhusu ujuzi na mitaji kutoka nje ya mipaka. Makampuni mengi ya mafuta ya uarabuni yanaongozwa na wataalamu kutoka nje au yanakuwa kwenye Joint Venture Agreements na makampuni ya nje.

Saudi Aramco kabla ya kufanya IPO lilikuwa lina mikataba ya JV na makampuni makubwa ya mafuta kutoka nje kama Exxon Mobil, BP na Royal Dutch Shell, ambapo yeye mwarabu anatoa pesa na eneo la uchimbaji huku mzungu akitoa ujuzi na kutafuta soko. Hivi ndivyo biashara inatakiwa ifanywe ndugu yangu, mnashirikiana.

Lakini upande mwingine kukwepa rushwa ni lazima serikali ifanye Forcible IPO's na kuyaweka makampuni yake kwenye soko la hisa. Ukishawekwa pale DSE na watu wakanunua hisa sidhani kama kutakuwa na ujinga wa kufanyia vitu chini ya kivuli cha chama tawala. Hakuna mwanahisa atakubali kufanyiwa ujinga ujinga kirahisi....
 
Mkuu Richard mazingira ya uwekezaji nchini kwetu na sehemu nyingi barani Afrika ni mazuri sana lakini hayatabiriki.
Bado hatujakomaa na tunakuwa na kawoga fulani kakuhisi kwamba kila mtu anataka kutuibia. This neurosis is justified, considering Africa's background with foreigners who came as missionaries and traders later turned masters. Sisi tuliopewa neema na Mungu ya kuzaliwa hiki kizazi hatutakiwi kuogopa na kuwa na mawazo kama wale wazee wa miaka ya 70 na 80. Ifike mahali tubadilike.......
Nafikri pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini kwetu na barani Afrika, uwekezaji wa wageni umejikita kwenye raslimali, changamoto tunayoipitia ni uwekezaji husika kunufaisha kundi dogo sana la watu wetu.

Lakini pia tulifungua milango ya uwekezaji hasa kwenye raslimali without an eye on resource nationalism matokeo yake tumepigwa vya kutosha hasa kwenye madini.

Lakini pia nchi zetu bado hazijawa na technolijia na mitaji itakayotupa bargaining power kwenye hizi investment agreements.

Kingine hatujafanya jitihada kubwa za kuwezesha locals wetu ili waweze kuingia ubia na makampuni ya kigeni.

Badala ya wananchi kunufaika kupitia corporate social responsibility na royalty kwa nchi ni vyema tukaruhusu wamiliki hisa kwenye mashirika ya umma yanayoingia ubia na makampuni ya kigeni hii itaongeza wanufaika lakini pia itaongeza public oversight kwenye uwekezaji husika.

How can we get of corrupt CEOs kwenye State run enterprises ni mtihani mwingine
 
Asante sana hope nikisoma policies za China nitapata mwanga zaidi hivi vitabu vya Karl Max nimevisoma Mara nyingi sana.

Hope nitafanya research kwenye economic laws za China nione namna gani zimeweza kuintergrate market economy vs socialist principles.
Tafuta kitabu kinaitwa The Third Way: A Renewal of Social Democracy by Professor Anthony Giddens.
Naamini utapata jawabu la hiki unachokitaka hapa mkuu, amefanya tafiti nzuri sana na amegusa pande zote.
 
Mkuu tatizo letu liko kimfumo zaidi na tumegoma kubadilika: Tunapenda kuendesha kila kitu kisiasa. Uarabuni wana State Run Enterprises lakini wamefanikiwa sana kuziendesha kwasababu waliamua kuruhusu ujuzi na mitaji kutoka nje ya mipaka. Makampuni mengi ya mafuta ya uarabuni yanaongozwa na wataalamu kutoka nje au yanakuwa kwenye Joint Venture Agreements na makampuni ya nje.

Saudi Aramco kabla ya kufanya IPO lilikuwa lina mikataba ya JV na makampuni makubwa ya mafuta kutoka nje kama Exxon Mobil, BP na Royal Dutch Shell, ambapo yeye mwarabu anatoa pesa na eneo la uchimbaji huku mzungu akitoa ujuzi na kutafuta soko. Hivi ndivyo biashara inatakiwa ifanywe ndugu yangu, mnashirikiana.

Lakini upande mwingine kukwepa rushwa ni lazima serikali ifanye Forcible IPO's na kuyaweka makampuni yake kwenye soko la hisa. Ukishawekwa pale DSE na watu wakanunua hisa sidhani kama kutakuwa na ujinga wa kufanyia vitu chini ya kivuli cha chama tawala. Hakuna mwanahisa atakubali kufanyiwa ujinga ujinga kirahisi....
Nilikuwa nafikri hili la public Corporations kuwa kwenye IPO lingekuwa na faida mbili.
1. Litawezesha wananchi kiuchumi kwa wao kumiliki hisa kwenye hizo Corporations

2. Nafikri tutadhibiti pia hao Corrupt CEOs kwenye mashirika kwani itaongeza transparency na yatalazimika kushindana kibiashara.

Lakini naona serikali bado iko reluctant juu ya hili la kuruhusu wananchi kumiliki uchumi wao kwenye public Corporations
 
Ni kweli mazingira hayatabiriki kwa sababu mbili kuu.

1. Wawekezaji si wawekezaji halisi na wapo kwa ajili ya kupata faida za harakaharaka na kutaka tax break za miaka mingi.

2. Baadhi ya viongozi wa Afrika au wale walo chini yao kuwa ndumilakuliwi khasa pale wanapofanya negotiations na wawekezaji.

Ni hapo Mchina anapotushinda, yeye kaweka sera za kiuchumi na ni lazima zifuatwe ila ni sera rafiki tu.

Sasa sisi ni kodi inasumbua sana wawekezaji tukifanikiwa hili la kodi tutakuwa sawa.

Kwa mfano serikali ingewaruhusu watanzania wenye uwezo kufanya joint venture na wawekezaji wa kigeni kwenye maeneo kama migahawa kama McDonald's, KFCs na Nandos.

Hivyo hawa wawaweka kwenye kundi maalum lenye kodi maalum.

Si lazima wawe ni wahindi tu kwenye kila kitu.

Hata wabantu nao wajitahidi ili waajiri wabantu wenzao na hapo soko la ajira linakuwa linapanuka.

Ndo maana naona watu kama Charles Kimei wanafaa kwenye biashara kwamba wana maono ya mbali kwenye masuala kama kuboresha micro economies.

Hata hizi reli zinazojengwa ni fursa kubwa sana ya kibiashara kwa mtu anaefahamu kupanga uchumi na sera.
Hilo la joint venture ni la msingi sana kwenye gas walifurukuta lakini haikufanikiwa hope with time tutajua namna gani ya kuongeza wanufaika kwenye hizi investment badala ya kutazama royalty na kodi tu.
 
Unaendelea kutengeneza Straw-Men na kuzidi kuniwekea maneno ambayo siyo yangu. Ninaposema kudhibiti Uchumi na Masoko it's by the virtue of regulating and controlling how goods and services flow within the markets, & ensuring compliance to monetary and fiscal policies which are pivotal for controlling the inflation. Hili ni tofauti kabisa na uchumi wa kupangwa "This is different from Economic Planning". Nadhani dhana hii ya Economic Planning imekuwa ngumu kwako kung'amua.

Pili, unajikanganya mwenyewe unaposema Marekani wameacha kutumia Keynesian Economic Model siku nyingi (Bila kutaja ni lini), lakini wanatumia tu pale ambapo panakuwa na uhitaji. Huu uchambuzi wako unashida kwasababu kama maraisi wa Marekani kuanzia Ronald Reagan hadi Donald Trump wametumia baadhi ya kanuni za Keynesian Economic Model: Massive Government Spending especially in the military & Infrastructure, Massive Tax Cuts & Tax Rebates, and Stimulus Packages.

Labda ulikuwa unamaanisha nini uliposema Marekani ameacha muda mrefu kutumia Keynesian Economic Model wakati mifano hai mbali na utoaji wa Stimulus Packages ipo mingi ???

Mosi, hizi takwimu zako hazina ukweli wowote kwasababu Uchina siku hizi nao wana Progressive Taxes, ambayo huanzia asilimia 3% hadi kufika 45% kwa wenye kipato kikubwa. Hilo la asilimia 30% wewe umelitoa wapi ???

Pili, Uchina mwaka 2018 amevunja rekodi kwa kutoa ruzuku ya dola za kimarekani bilioni 22 (Ambazo ni zaidi ya trilioni arobaini za kitanzania) kwa makampuni yake. Sasa unaposema mataifa ya Magharibi ndiyo yanaongoza kutoa ruzuku kuliko Uchina halafu hujaniwekea ushahidi nadhani hoja yako inakuwa iko mufilisi kabisa. Huu ndiyo umekuwa ugomvi mkubwa baina ya Uchina na Marekani kule WTO.

Hebu niambie wewe: Tanzania inafuata dira gani ya kiuchumi inayofanya nchi ikue kwa asilimia 6%

Hayo makampuni ya Korea Kaskazini yaliyoingia kwenye ubia na mashirika ya nje yanamilikiwa na nani ???
Japo umekuwa mtaalamu wa Chinese economy lakini unatupa picha China unayoijuwa wewe ni kwenye makaratasi.

Nashindwa hata kupata logic ya paragraph one, virtue of regulating and controlling how goods and services flow within the markets, & ensuring compliance to monetary and fiscal policies which are pivotal for controlling the inflation. Hili ni tofauti kabisa na uchumi wa kupangwa "This is different from Economic Planning". Sasa economic plan ya miaka mitano au kumi ijayo inahusiana nini control of goods and services of today. Labda ufafanuzi kidogo kwa ngumbalu kama sisi.

Ukija kwenye Keynesian Economic Model, nimesema US waliacha kutumia huu mfumo miaka mingi iliyo pita, to be precise 70's Nixon era. Sidhani kama umesikia katika miaka 10 au 15 iliyopita serikali ya US ilijihusisha na major infrastructure projects to stimulate the economy. Sio New railways, new airport, new ports au hata new highways. Investment in military doesn't count as economic stimulus. Economic stimulation ya mwisho Wamarekani walichofanya ni kuwawekea pesa mifukoni kwa watu (direct credit) baada ya 2008 crush. Sasa ukisema Regan na viongozi wengine walitumia Keynesian Economic Model, walitumia kufanyia nini.

China ina kodi kuanzia 3% mpaka 45%. Ndugu, kuna nchi duniani haina tax base tofauti kulingania na kipato cha mlipa kodi? Mfano niokupa mwanzoni kulinganisha mlipa kodi wa China wa UK ni kwa watu wenye kipato cha juu. Hata Tanzania tunakuwago cha chini cha ulipaji kodi ambacho ni kitambulisho cha machinga Tshs20,000/-pa

Swala la China kutumia $22 billion kusaidia makampuni yake, ni drop in ocean kulinganisha na sehemu kama EU wanaotumia €187 billion kwa mwaka kuhakikisha kazi na sekta mbali mbali hazikumbwi utatanishi wa soko. Marekani ndio ina bajeti kubwa ukija kwenye subsidies $1.1 trilioni kusaidia wakulima, mashirika ya ndege, maji, elimu, afya nk. Hii ni tofauti na Keynesian Economic Model maana hiyo keynesian ni ku-stimulate economy wakati uchumi unakufa, while subsidies ni kulinda uchumi ili uvuke kwenda mwaka wingine.

Tanzania tunafuata mixed economy, hatutegemei sekta moja au hata mwekezaji mmoja. Its mixed of public investment running parallel with private investment. Kuanzia kwenye kilimo, madini, mabenki, huduma, afya, ujenzi na vingine vingi. Mashirika yote yanashindana kwenye level playing field na hakuna upendeleo. Ikiwa kama wewe ni kijana wa kitanzania na unasema hujuwi Tanzania inafuata mfumo gani, you can only blame yourself.

Haya ya N.Korea nadhani unauwezo wa kufanya research na kujuwa yote. Is not a rocket science.
 
Alianza na kauli, kwa kusema chama chenye dola kushindwa kutetea dola yake ni uzembe!. Alishangaa iweje uwe na dola kisha upoteze dola.

Naam!. Kwenye uchaguzi huu tumeona alichomaanisha!. Bila shaka sote tuliona nini maana ya kutumia dola kubaki na dola, Tulishuhudia Kura kwenye vikapu vya akina mama, nyingine kwenye mabegi. Wapo waliozishika hizo kura na kuzipekeka polisi, polisi wakawajibu kwa mkato tu "Hatushughulikii masuala ya uchaguzi".

Maelfu kwa maelfu ya Mawakala wa vyama shindani wakapigwa zengwe, wakazuiwa kuingia, na wale walioningia wakapigwa zengwe wasipate nakala za matokeo.

Kule Zanzibar watu wakaonekana wanaopiga kura kwa lumbesa, mtu mmoja kura lundo.

Falsafa ya Bashiru Ally Kakurwa mtoto wa Kiislamu huyo aliyepitia madrasa!

Lakini huyu ni mwalimu wa chuo kikuu, msomi mkubwa, kafundisha wanafunzi wengi tu nadharia za demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi yao wenyewe. Kafundisha sana masuala ya class struggle, ni role model wa maelfu ya wanafunzi wake wa ndani ya darasa na nje ya darasa! Sijui ametuma ujumbe gani kwa watu ambao walikuwa inspired naye kabla ya kuingia kwenye siasa pale wanapoona amekuwa katibu mkuu wa chama ambacho leo kimenufaika kwa mchakato feki na haramu kabisa wa uchaguzi, uliogubikwa na wizi wa kura wa kutisha katika historia ya nchi hii toka uhuru!

Lakini cha kuchekesha zaidi, Sheikh Bashiru Ally Kakurwa eti ni mjamaa, mfuasi wa Nyerere. Eti naye alikuwa mdau mkubwa wa Kigoda cha mwalimu. Eti naye alikuwa akiimba kama kasuku kuhusu uadilifu na sense ya haki ya mwalimu Nyerere.

Haya hatukuhadithiwa, tumeona kwenye TV mihadhara ya kigoda cha Mwalimu, Tumemuona Bashiru Ally Channel ten akielezea falsafa za haki, uadilifu, demokrasia, uhuru, umoja, n. k lakini hatukujua kuwa miaka michache baadaye, Bashiru huyuhuyu atakuwa ni katibu mkuu wa chama kilichonufaika kwa kuhujumu wananchi kuwaweka madarakani watu wawatakao wao wenyewe kupitia sanduku la kura!

Nikiangalia miaka michache ijayo nini itakuwa Legacy ya Bashiru Ally kwenye utumishi wa CCM, Siioni zaidi ya kushiriki kuwanyima wananchi viongozi na wawakilishi wawatakao watokanao na ridhaa zao wenyewe!. Kiufupi naye ni mshiriki asiyeweza kujivua lawama kwa dhulma hii kubwa waliyotendewa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata kama ngazi ya urais wa Muungano mlikuwa mkiitaka kwa udi na uvumba lakini Bashiru, hivi kweli Hussein ni wa kumshinda Maalim Seif kwa zaidi ya 57%?

Bashiru hivi kweli Tulia ni wa kumshinda Sugu Mbeya?

Hivi kweli Zitto ni wa kushindwa na yule Jamaa pale Kigoma? na mifano ya ya namna hii ni mingi nchi nzima!

Msomi na Mjamaa Bashiru hongera sana kwa kushiriki ipasavyo kuithibiti demokrasia vilivyo!, Maana sasa demokrasia ni kama adui yenu mliyefanikiwa kumdhibiti asifurukute!, But ngoja nikwambie kitu kimoja mko myopic sana kwa hizi moves zenu, kwa sababu ili mfanikiwe katika lengo lenu hilo ovu itabidi muwe wanafiki zaidi, walaghai zaidi, waonevu zaidi, madhulumati zaidi, msiheshimu wananchi zaidi.

Mtafanya hivyo mpaka mtakapokutana na kigingi kutoka kule ambako hamkukudhania kabisa, kisha hapo common sense zitawarudia kuwa ni USELESS KUDHANI KIKUNDI KIDOGO KINA AKILI KULIKO UMMA, maana umma utasimama na nguvu yeyote itakayokema yaani itakayoweka kigingi cha kuzuia dhulma zenu, nguvu ya kuzuia uonevu wenu, nguvu ya kuzuia ulaghai wenu!. Nguvu hiyo Ama inaweza iwe ni nguvu yoyote ya ndani ya nchi au ya nje ya nchi au zote mbili kwa pamoja as long as wananchi wataona hii inasimama nao na inawatetea wataiunga mkono kwa maua, nderemo, vifijo, bashasha, kucheza, kusifu, n. k!.

Mwalimu Bashiru, Nikukumbushe tu kuwa mahali popote pale duniani uchaguzi hovyo na corrupt, huzaa serikali hovyo na corrupt na hutengeneza bunge hovyo na corrupt lisiloogopa wananchi bali wale waliowawezesha kuingia bungeni kwa njia corrupt!. Kamwe haiwezekani kupata maendeleo kwa bunge na serikali ya aina hiyo, maana hiyo si serikali na bunge la watu kwa ajili ya watu, bali ni kundi tu la watu wachche tu wenye "special interests" lenye kumiliki silaha na kwa silaha hizo huwatisha wananchi wasinyanyuke na kudai haki yao ya kuwa na viongozi watokanao na ridhaa yao, lakini ukweli ni kuwa serikali ya hivyo na bunge la hivyo havina legitimacy mbele ya watu hao!

Bashiru Umeshiriki dhambi ya kuwadhulumu haki wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, unajisikiaje, "umewaweza" wapinzani au "umeiweza" nchi?. Kwamba umeacha alama ya heshima au alama ya aibu?

Shame on you!
Huyo Bashiru, Polepole, Kheri, Musiba lao ni moja.
Hawa wanapaswa kufikishwa ICC. Na pia wanapaswa kupigwa marufuku kusafiri kwenye nchi zote za Ulaya wao na Familia zao.
Na wakikanyaga nchi yoyote ya Jumuiya ya madola wakamatwe.

Hawa watu hawana tofauti na majambazi. Jambazi anapoona upenyo wa pesa anatumia nguvu hata kuua alimradi azipate aendeshe maisha na familia yake.

Bashiru na Polepole wametuletea wabunge wengi waliokua na tuhuma za rushwa kwa muda mrefu na wengine walitafutwa muda mrefu na Takukuru.
Tutakua na Bunge la wapenda Madaraka watupu. Na wajue kabisa mwisho wa heshima kidogo waliyo nayo ni 2025 mana Makundi ndani ya CCM ndio yatakua na nguvu kuliko wakati wowote mana kila mtu atataka kumpata Rais wa kutoka eneo lake ili kupeleka maendeleo kijijini kwake bila kuhojiwa.
Ule woga wa enzi za mwalimu wa kuogopa kupendelea nyumbani kwa kodi za wote umekwisha sasa watu watapeleka mpaka Bahari kijijini kweo alimradi tu wapate ile nafasi ya kuwa kama mungu asiyeshindwa.

Bashiru na Polepole wameua Uhuru wa watoto wa maskini kujieleza na kujenga hoja kukuza uwezo wa kujieleza na kuona makosa na kuyakosoa .
Hata Bashiru , Polepole ,Kafulila,Mashinji,Katambi,Kabudi na wengine hawakupata umaarufu na kuonekaba kwa kusifia tu bali kwa Uhuru uliokuwa umeweka na Kikwete wa kutoa maoni.
Kama Kikwete angewapiga mabomu na kuwafungulia kesi za Uchochezi leo hii hao watu wangekua jalalani . Uhuru walioupata wakati wa ujana wao ndio uliowafanya wajulikane sasa wamekuja kuua Uhuru ili watoto wengine wa maskini wanaotegemea nguvu ya umma kuungwa mkono wasipate nafasi ya kujieleza bila woga.
Damu za Watu wote waliouawa ,walioteswa na kufungwa kwenye uchafu walioufanya wakati wa Uchaguzi Ziwe juu ya Polepole,Bashiru, Musiba ,Kheri ,Kabudi na Tume ya Taifa.
 
Japo umekuwa mtaalamu wa Chinese economy lakini unatupa picha China unayoijuwa wewe ni kwenye makaratasi.

Nashindwa hata kupata logic ya paragraph one, virtue of regulating and controlling how goods and services flow within the markets, & ensuring compliance to monetary and fiscal policies which are pivotal for controlling the inflation. Hili ni tofauti kabisa na uchumi wa kupangwa "This is different from Economic Planning". Sasa economic plan ya miaka mitano au kumi ijayo inahusiana nini control of goods and services of today. Labda ufafanuzi kidogo kwa ngumbalu kama sisi.

Ukija kwenye Keynesian Economic Model, nimesema US waliacha kutumia huu mfumo miaka mingi iliyo pita, to be precise 70's Nixon era. Sidhani kama umesikia katika miaka 10 au 15 iliyopita serikali ya US ilijihusisha na major infrastructure projects to stimulate the economy. Sio New railways, new airport, new ports au hata new highways. Investment in military doesn't count as economic stimulus. Economic stimulation ya mwisho Wamarekani walichofanya ni kuwawekea pesa mifukoni kwa watu (direct credit) baada ya 2008 crush. Sasa ukisema Regan na viongozi wengine walitumia Keynesian Economic Model, walitumia kufanyia nini.

China ina kodi kuanzia 3% mpaka 45%. Ndugu, kuna nchi duniani haina tax base tofauti kulingania na kipato cha mlipa kodi? Mfano niokupa mwanzoni kulinganisha mlipa kodi wa China wa UK ni kwa watu wenye kipato cha juu. Hata Tanzania tunakuwago cha chini cha ulipaji kodi ambacho ni kitambulisho cha machinga Tshs20,000/-pa

Swala la China kutumia $22 billion kusaidia makampuni yake, ni drop in ocean kulinganisha na sehemu kama EU wanaotumia €187 billion kwa mwaka kuhakikisha kazi na sekta mbali mbali hazikumbwi utatanishi wa soko. Marekani ndio ina bajeti kubwa ukija kwenye subsidies $1.1 trilioni kusaidia wakulima, mashirika ya ndege, maji, elimu, afya nk. Hii ni tofauti na Keynesian Economic Model maana hiyo keynesian ni ku-stimulate economy wakati uchumi unakufa, while subsidies ni kulinda uchumi ili uvuke kwenda mwaka wingine.

Tanzania tunafuata mixed economy, hatutegemei sekta moja au hata mwekezaji mmoja. Its mixed of public investment running parallel with private investment. Kuanzia kwenye kilimo, madini, mabenki, huduma, afya, ujenzi na vingine vingi. Mashirika yote yanashindana kwenye level playing field na hakuna upendeleo. Ikiwa kama wewe ni kijana wa kitanzania na unasema hujuwi Tanzania inafuata mfumo gani, you can only blame yourself.

Haya ya N.Korea nadhani unauwezo wa kufanya research na kujuwa yote. Is not a rocket science.
Kukurekebisha tu, kitambulisho cha wamachinga siyo kodi, wenyewe waliovitngeneza walidai eti hiyo ni "gharama za kuvichapisha tu", kiufupi ni mradi wenye maswali mengi kuliko majibu!
 
Huyo Bashiru, Polepole, Kheri, Musiba lao ni moja.
Hawa wanapaswa kufikishwa ICC. Na pia wanapaswa kupigwa marufuku kusafiri kwenye nchi zote za Ulaya wao na Familia zao.
Na wakikanyaga nchi yoyote ya Jumuiya ya madola wakamatwe.

Hawa watu hawana tofauti na majambazi. Jambazi anapoona upenyo wa pesa anatumia nguvu hata kuua alimradi azipate aendeshe maisha na familia yake.

Bashiru na Polepole wametuletea wabunge wengi waliokua na tuhuma za rushwa kwa muda mrefu na wengine walitafutwa muda mrefu na Takukuru.
Tutakua na Bunge la wapenda Madaraka watupu. Na wajue kabisa mwisho wa heshima kidogo waliyo nayo ni 2025 mana Makundi ndani ya CCM ndio yatakua na nguvu kuliko wakati wowote mana kila mtu atataka kumpata Rais wa kutoka eneo lake ili kupeleka maendeleo kijijini kwake bila kuhojiwa.
Ule woga wa enzi za mwalimu wa kuogopa kupendelea nyumbani kwa kodi za wote umekwisha sasa watu watapeleka mpaka Bahari kijijini kweo alimradi tu wapate ile nafasi ya kuwa kama mungu asiyeshindwa.

Bashiru na Polepole wameua Uhuru wa watoto wa maskini kujieleza na kujenga hoja kukuza uwezo wa kujieleza na kuona makosa na kuyakosoa .
Hata Bashiru , Polepole ,Kafulila,Mashinji,Katambi,Kabudi na wengine hawakupata umaarufu na kuonekaba kwa kusifia tu bali kwa Uhuru uliokuwa umeweka na Kikwete wa kutoa maoni.
Kama Kikwete angewapiga mabomu na kuwafungulia kesi za Uchochezi leo hii hao watu wangekua jalalani . Uhuru walioupata wakati wa ujana wao ndio uliowafanya wajulikane sasa wamekuja kuua Uhuru ili watoto wengine wa maskini wanaotegemea nguvu ya umma kuungwa mkono wasipate nafasi ya kujieleza bila woga.
Damu za Watu wote waliouawa ,walioteswa na kufungwa kwenye uchafu walioufanya wakati wa Uchaguzi Ziwe juu ya Polepole,Bashiru, Musiba ,Kheri ,Kabudi na Tume ya Taifa.
Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM ilikuwa ni rushwa tupu.
Leo wamepitisha watu corrupt kugombea ubunge na kisha wakawashindisha kinguvu bila ridhaa ya wananchi.
Kiufupi wametuletea bunge corrupt.
Bunge la namna hii haliwezi kuithibiti serikali katika issue za ubadhirifu wa pesa za wananchi au ufisadi, maana vitu hivyo ndiyo nature yao haswaa!
Umewahi kuona wapi shetani akimtoa shetani mwenzie?
 
Nashindwa hata kupata logic ya paragraph one, virtue of regulating and controlling how goods and services flow within the markets, & ensuring compliance to monetary and fiscal policies which are pivotal for controlling the inflation. Hili ni tofauti kabisa na uchumi wa kupangwa "This is different from Economic Planning". Sasa economic plan ya miaka mitano au kumi ijayo inahusiana nini control of goods and services of today. Labda ufafanuzi kidogo kwa ngumbalu kama sisi.
Nadhani kama hujanilewa nilivyoeleza kuhusu Economic Planning and Command Economy kwa nchi za kikomunisti sidhani kama hata nikitembea kichwa chini miguu juu utanielewa. Lakini kama ulivyosema It's not rocket science basi wafuate waliosomea uchumi wa ujamaa Shivji na Bashiru halafu waambie wakueleze dhana nzima za Base and / Superstructure/Economic Planning and Command Economy.

Ukija kwenye Keynesian Economic Model, nimesema US waliacha kutumia huu mfumo miaka mingi iliyo pita, to be precise 70's Nixon era. Sidhani kama umesikia katika miaka 10 au 15 iliyopita serikali ya US ilijihusisha na major infrastructure projects to stimulate the economy. Sio New railways, new airport, new ports au hata new highways. Investment in military doesn't count as economic stimulus. Economic stimulation ya mwisho Wamarekani walichofanya ni kuwawekea pesa mifukoni kwa watu (direct credit) baada ya 2008 crush. Sasa ukisema Regan na viongozi wengine walitumia Keynesian Economic Model, walitumia kufanyia nini.
Nilihisi unafahamu vizuri lakini kumbe na wewe una shida kubwa pahala kuhusu uelewa wa baadhi ya mambo. Ngoja nikuoneshe umufulisi wa hoja yako hii kitaalamu. Usiponielewa hapa basi hata malaika ashuke hutakaa unielewe na sintakuwa na muda wa kubishana na wewe:

Mosi, unapoiangalia Keynesian Economic Model kwa jicho la Economic Stimulus Packages bila kuangalia mambo mengine kama Tax Cuts & Tax Rebates na Government Spending nadhani utakuwa na parcohial understanding of the world. Unaponiambia kwamba tangu kipindi cha Nixon nchi ya Marekani hawajafanya matumizi yoyote kwenye miondombinu napata ukakasi sana na jinsi unavyoelewa mambo: Ronald Reagan alifanya massive Tax Cuts. Kuhusu miradi nakushauri fanya tafiti tena, kuna miradi mikubwa sana imefanyika nchini Marekani.

Pili, umenishangaza sana uliposema kwamba matumizi ya jeshi huwa hayahesabiki kwenye uchumi na kuendelea kukomaa kwamba Stimulus Packages pekee ndiyo kanuni pekee ya Keynesian Economic Model. Wachumi wakubwa duniani kama Professor Stanley Fischer wanasema matumizi ya jeshi ni muhimu sana katika kupima na kuangalia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mashirika makubwa kama Goldman Sachs na The Institute of Strategic Studies kwenye chapisho lao liitwalo The Military Balance wameenda mbali zaidi na kusema siku hizi wanatumia PPP (Purchasing Power Parity) kama ndiyo benchmark ya kupimia Uchumi wa taifa kuliko kutumia GNP na GDP: Ukitumia hii njia basi ni lazima uzingatiea matumizi ya kijeshi ambayo wewe ndugu yangu bwana Mwanzi umekanusha. Mchumi kwanini unashindwa kuelewa hili jambo rahisi kabisa ???

China ina kodi kuanzia 3% mpaka 45%. Ndugu, kuna nchi duniani haina tax base tofauti kulingania na kipato cha mlipa kodi? Mfano niokupa mwanzoni kulinganisha mlipa kodi wa China wa UK ni kwa watu wenye kipato cha juu. Hata Tanzania tunakuwago cha chini cha ulipaji kodi ambacho ni kitambulisho cha machinga Tshs20,000/-pa
Tatu, wewe siyo mtu mkweli au aidha huelewi nilichokisema: Tanzania hatuna Progressive Tax tuna Proportional Tax.
Makundi yote hulipa asilimia moja ya pesa katika vipato vyao, kama ipo hebu tupe mifano. Uchina ukiwa tajiri na kodi inaanza kuwa Progressive. Kafanye tafiti zaidi au kama unataka tuanze kuongelea kodi basi fungua uzi mwingine.

Mimi nikajua kwamba nazungumza na mtu mwenye elewa wa mambo kumbe I'm just laboring in futility. Hivi malipo ya Tsh 20,000 ya vitambulisho vya machinga nayo ni kodi ??? Kama ni kodi basi naomba unitajie basi ni kodi ya aina gani na iko kwa mijali ya sheria ipi.

Swala la China kutumia $22 billion kusaidia makampuni yake, ni drop in ocean kulinganisha na sehemu kama EU wanaotumia €187 billion kwa mwaka kuhakikisha kazi na sekta mbali mbali hazikumbwi utatanishi wa soko. Marekani ndio ina bajeti kubwa ukija kwenye subsidies $1.1 trilioni kusaidia wakulima, mashirika ya ndege, maji, elimu, afya nk. Hii ni tofauti na Keynesian Economic Model maana hiyo keynesian ni ku-stimulate economy wakati uchumi unakufa, while subsidies ni kulinda uchumi ili uvuke kwenda mwaka wingine.
Hiyo takwimu ya ruzuku ya dola za Kimarekani Trillioni moja umeitoa wapi na imetolewa lini na serikali ya Marekani ?
Hizo ruzuku za zinazotolewa na umoja wa Ulaya zinatolewa kwenye sekta zipi ???
Je, WTO Rules zinaruhusu utoaji wa ruzuku ???
Tanzania tunafuata mixed economy, hatutegemei sekta moja au hata mwekezaji mmoja. Ikiwa kama wewe ni kijana wa kitanzania na unasema hujuwi Tanzania inafuata mfumo gani, you can only blame yourself.
Basi kama hii ndiyo hoja yako, basi kila nchi duniani ni Mixed Economy na ulikuwa huna haja ya kuniuliza swali kama hili kwasababu It wouldn't have made any diffference, considering that aspects of private and public enterprise are in sync and prevalent in almost all global economies.
 
Back
Top Bottom