Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Awamu ile JMK alikuwa kila wiki yuko Marekani au Ulaya au Sauzi au Japani au ...... yaani kila safari zilitumika takriban DOLA MILIONI pamoja na ulaji humo humo..... mwenyewe alisema eti anasaka misaada - wananchi wakampachika lakabu ya MATONYA - kuomba msaada kwa Bush au Obama kila siku - Walitucheka !!! Yote hayo pamoja na mikataba mibovu na wafanyakazi hewa na wanachuo hewa .........basi yatosha
 
Hivi hawa wazee hawawezi kukaa kimya kujilindia heshima zao?
 
Hao wapiga kura wa ccm waliongezeka wamewajuaje? Ama ni matokeo ya uchafuzi wa serikali za mitaa?
 
January 19, 2020


Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa

WanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa.

Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.

Dkt. Bashiru katika kikao hicho na wanaCCM anasema wote tunaona Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana.

Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano.

Bashiru anaendelea kujadili na kuwaomba rai wanaCCM tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Vitu na Maendeleo ya Watu hivyo tusikazanie ktk kitu 'matumaini', bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika na hayana uhalisia hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.

Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.

Source: Millard Ayo.

Ni nani aliyewafukuza akina Twaweza baada umaarufu kupungua kwa asilimia kutoka 90% hadi 40%? Je ni JK?
Ni nani akiona uchaguzi hata wa serikali za mitaa anaweka mpira kwapani na kuhujumu hovyo? Je ni JK?
Ni nani muoga aliyekunjia mkia matakoni asiyeruhusu wapinzani waongee na wapiga kura? lakini hajiamini? Je ni JK?
Ni nani anayezurura mitandaoni kutafuta watu wanaomsema vibaya ili awateke? Je ni JK?
Ni nani anahangaika kuteka teka hata ameunda kikosi cha watekaji wa wapinzani? Je ni JK?
Spare my breadth Bashiru soon you will become Bashir!!
 
Sasa nimejua msingi wa kejeli za Bashiru Ally. Kama siku kumi hivi zilizopita mama Salma Kikwete alikuwa na mkutano na wananchi wa Rondo kijijini kwa Membe,baada ya mkutano mama Salma Kikwete alijumuhika na Membe kupata chakula cha mchana nyumbani kwa membe huko kijijini Rondo.

Raisi wa muhula mmoja ameongezewa hofu hivyo amemtuma mmoja wa wazee wa jalalani kuja kumwaga povu. Hahahahaaa
 
Kwanini wanapenda kumangana-mangana,kama huyu anakubalika sana si wasonge mbele yanini kufufua makaburi daily!! Ukitoka familia maskini kilasiku utakuwa unadhihaki wazazi!! Kwanini wasijifananishe na viongozi wanchi nyingine waliofanya makubwa. Kilasiku kiku kiku mbona hamumsifu kwakubadili maisha ya wafanyakazi baada ya njaa Kali ya mkapa!!
 
Naomba kujua, hivi Dr Bashiru alikuwa ccm au Dr magufuli alimuita kwa kuwa yeye Bashiru ni non partisan?? Ninavyojua Dr Magufuli sio mjinga wa kuokotezaokoteza makapi.
 
Back
Top Bottom