Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Wote hawa ndio sampuli ya jalalani binafsi katika Phd niliowahi kuwasikia wanaongelea siasa ninaye mkubali ni Lwaitama pekee.

Ukitaka kujua huyu Bashiru ni bogus kesho anaweza kweli mpigia simu JK na kumwambia tunaomba ushiriki kwenye campaign za uchaguzi au watu wengine wanao watukana kila siku.

Inawezekana kwenye kichwa chake; yeye, Polepole, Jerry Murro, Happi, Chalamila na Makonda wanaushawishi mkubwa sana peke yao kuweza kufanya campaign Tanzania nzima.
Kwa mtazamo wako unafikili wanahitaji kampeni? Wangekuwa wanajua kuna uchaguzi huru na wa haki wasingekuwa wanatoa kauli za aina hii!
 
‘...Bunge limekuwa na Demokrasia zaid kipindi hiki kuliko kipindi cha Kikwete...’-Dr Bashiru


Hapa Bashiru alikuwa anawatukana wanaomsikiliza sio Kikwete.
 
Kwa mtazamo wako unafikili wanahitaji kampeni? Wangekuwa wanajua kuna uchaguzi huru na wa haki wasingekuwa wanatoa kauli za aina hii!
Either way ni kauli ya mtu ambae ajawahi fanya kazi za kitaasisi ya chama ata ngazi ya mtaa wala kushiriki katika harakati za uchaguzi.

Kauli kama hizo hao watu wanao wakebehi wangekuwa wana kinyongo au immature kama yeye zina madhara.

Huu ni mwaka wa uchaguzi imagine JK na yeye atoke aanze kuwa defensive tu publicly kuhusu hizo kebehi au atoe maoni yake kuhusu negativity za mwenendo wa serikari na kazi za Bashiru. Si tayari wanaingia kwenye uchaguzi wakiwa sio wamoja na ni kwa faida ya nani.

Bashiru and Kabudi ni watu ambao wasioweza chunga kauli zao, awajui diplomatic language. Maneno yao sio mazuri kabisa kwa morale ya institution wanazoongoza na very demoralising.

Bahati nzuri hao wanaokejeliwa ni waelewa wa madhara ya kujibu kwa mustakabali wa chama chao haswa mwaka huu wa uchaguzi.
 
Kwa mtu yeyote aliyesomea elementary economics na Basic Financial management atakubaliana na haya.
1. Rais Kikwete alitengeneza matajiri wengi sana ambao nao walisababisa watu wa chini kunufaika kwa sababu labor (nguvu kazi) as a commodity (bidhaa) ilipanda bei kwa sababu ilikuwa na uhitaji. Pia nyumba zipanda bei sana hasa za mjini.
Thamani ya ardhi ikipanda sana, na kwa sababu asilimia kubwa ya ardhi ya Inchi hii inamilikiwa na maskini, walionufaika na mfumuko huu wa bei ya ardhi ni maskini.
2. Rais Makufuli ameifanya Serikali kuwa na uwezo mkubwa na kifedha na kusababisha lobor kushuka bei na pia estates kama ardhi na nyumba kushuka bei sana.
Mifumo yote miwili ya Ma Ris wetu wapendwa ina faida zake na hasara zake. Lakini kubwa ni kwamba mifumo yote miwili haijaharibu Amani ya inchi.
Mfumo wa Rais Kikwete kuwafanya watu wawe matajiri sana na Serikali kuwa maskini si mfumo wa Kisayansi na haukubaliki Kitaaluma.
Rais Kikwete ni Mchumi na alijua alichokuwa anakakifanya na alikifanya makusudi ili Watanzania kama mtu moja moja wapate manufaa. Alijua kuwa atakuja kiongozi mwingine ambaye atarekebisha.
Wakati anatafuta mtu wa kumrithi alisema "itabidi tuwatafutie kiongozi mkali kidogo"
Alipokwenda kumsalimu Rais Makufuli alisema. " Nilikwenda kumpongeza Rais Makufuli, Rais wangu kwa sababu amewanyoosha"
 
Sioni vibaya sana kwa kuwa hili zimwi waliliunda wenyewe! wakalipa power ya kufanya litakavyo! walitarajia yatatukuta wapinzani peke yetu? Hapana! wacha tugawane maumivu!
Jamani CCM kuyumba wakati wa Kikwete ni kwasababu demokrasia iliruhusiwa bila vikwazo vingi. Wakati KM analalamika kudhoofika kwa CCM anashau kuwa opposition ilikuwa inastawi
 
Naona Bashiru ameamua kumkejeli na kumtusi JK waziwazi. Au labda anaongea kinyume.
 
UDSM inatakiwa wampe PHD nyingine huyu bwana, au awe Profesa kabisa. Inapendeza tukimuita Prop Bashiru.
Kwa kazi nzuri iliyotukuka anayotufanyia wanyonge wa Tanzania na chama chetu CCM ni vyema UDSM wakamtunuku kuwa PROFESA au wamuongezea PHD nyingine.
 
Back
Top Bottom