Dkt. Bashiru: Baada ya mzee Kikwete kuingia kura zetu (CCM) zilianza kuporomoka

Bashiru kaonyesha tabia za kihaya 100%.jk Na membe wakijibu utasikia wanaanza kuwaandama...
 
January 19, 2020

'BAADA YA MZEE KIKWETE KUINGIA KURA ZETU ZILIANZA KUPOROMOKA, CHAMA KILIPATA MSUKOSUKO'' BASHIRU

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa . wanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa. Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.

Dkt. Bashiru katika kikao hicho na wanaCCM anasema wote tunaona Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana.

Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano.

Bashiru anaendelea kujadili na kuwaomba rai wanaCCM tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Vitu na Maendeleo ya Watu hivyo tusikazanie ktk kitu 'matumaini', bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika na hayana uhalisia hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.

Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.

Source: Millard Ayo.

Nimepata wasiwasi huenda elimu yetu inapoingia chamani hugeuka na kuwa ujinga. Au niko ndotoni?
 
Hawa mashetani ni kuwagomea tu kwa kila kitu ambacho hakina ulazima ama chenye mbadala. Mimi mwenyewe kitambo tu sasa sinunui bidhaa kwa duka la mshabiki wa kijani wala sitoi ushirikiano kwa nzi yoyote wa kijani. Ukweli ni kwamba hawa nzi wa kijani ndio walio duni na dhaifu katika jamii na kama tutakuwa tuko serious na hili basi wao ndio waathirika wakubwa!
 
Siku nilipoona Mbowe kashinda kwa 93.5% dhidi ya mpinzani wake Cecil ndio nilijua maana halisi ya kucheza na sanduku la kura ambayo sikupata kuijua kabla

Hapo unaona umesawazisha? Mwambe angepewa kura na nani? Alikuja na upepo wa Lowassa, na Lowassa kasharudi ccm yeye alitegemea nini?
 
January 19, 2020

'BAADA YA MZEE KIKWETE KUINGIA KURA ZETU ZILIANZA KUPOROMOKA, CHAMA KILIPATA MSUKOSUKO'' BASHIRU

Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru anaichambua safari ya kisiasa ya CCM toka mwaka 2015, ambapo kura za CCM ziliporomoka na Magufuli alipata 58%. Fitna na misukosuko ikawa jadi ya chama. Wasemakweli wakawa maadui wa chama na kupelekea kuitwa na Halmashauri Kuu ya Chama NEC wakapewa adhabu na wengine kufukuzwa . wanaCCM wenye nia njema wakaanza kukaa kando na chama kikaanza kuendeshwa na wachache wababaishaji. Watu wanapata kazi ndani ya CCM bila ujuzi wanapata nafasi hizo kiushikaji. Miradi mingi inayohusu watu (Maendeleo ya Watu) ikafa. Hata idadi ya wapiga kura ikaanza kuporomoka kutokana na wananchi kukosa imani na CCM. Watu hawana imani na vyombo vya kusimamia uchaguzi chini ya serikali ya CCM.

Dkt. Bashiru katika kikao hicho na wanaCCM anasema wote tunaona Baada ya miaka minne ya Magufuli mambo yamebadilika, yale ya Kikwete niliyoyabainisha yamefutika. Sasa Watu wanaimani na uchaguzi, idadi ya wapiga kura imepanda na kupanda maradufu sana.

Mkazo ktk Maendeleo ya Watu umezidi kusisitizwa sambamba na Maendeleo ya Vitu chini ya Awamu ya Tano.

Bashiru anaendelea kujadili na kuwaomba rai wanaCCM tusibishanie ndege, flyovers, madaraja na SGR reli Mpya maana sote tunaona Maendeleo hayo ya Vitu na Maendeleo ya Watu hivyo tusikazanie ktk kitu 'matumaini', bali vitu halisi tunavyoviona na kuvishika. Matumaini ni matamanio kama mapenzi huwezi kuvipima au kuvishika na hayana uhalisia hivyo haya Maendeleo ya Vitu kama ndege ni maendeleo dhahiri tusiyabishanie.

Bunge limekuwa na heshima hakuna vurugu. Demokrasia na Haki za binadamu imezidi kuzingatiwa kama ilivyoainishwa na Katiba yetu ya nchi. Chaguzi kama za Serikali za Mitaa November 14, 2019 chini ya wizara ya TAMISEMI zimefanyika bila vurugu na CCM imeshinda kwa kishindo asilimia 98%.

Source: Millard Ayo.
We Bashiri vip bhna, kura zenu kwani CUF ndio ilikuwa madarakani wakati wa Mzee Kikwete?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom