Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Uchaguzi 2020 Dkt Bashiru: CCM haipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
880
Reaction score
971
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama, mashabiki na wakereketwa wa CCM kuwa Chama hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini kama ilivyofanyika miaka michache nyuma.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa kamati za siasa za wilaya ya Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijini mara baada ya kupokelewa akitokea Mkoani Dodoma.

"Ujumbe ninao utoa kwa vyama vya upinzani leo tarehe 17 Desemba, 2019 ni kuwa, nataka jimbo la Iringa mjini na Manispaa yake lirudi CCM, na Mkoa wa Iringa umekuwa ni ngome ya CCM miaka yote, hapa mjini yalifanyika makosa ambayo ndani ya uongozi huu hayatojirudia tena."

Aidha Katibu Mkuu ameongeza kuwa,
Jimbo hilo lilipotea kutokana na migawanyiko ndani ya CCM, na awamu hii, jimbo na manispaa yake inarudi CCM na Chama hakitarajii kufanya makosa tena.

Katika hatua nyingine, Dkt. Bashiru ameendeleea kuwaasa wanaCCM kuwa, heshima wanayopatiwa viongozi, ni heshima kwa Chama, ambapo ndani ya CCM hakuna mtu maarufu wala kiongozi maarufu kuliko chama, nje ya Chama, hakuna mtu maarufu hivyo ni lazima viongozi na wanachama wajue wanapata heshima kwa sababu ya Chama na ni lazima tukilinde ili kiendelee kubaki na heshima wakati wote.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kueleza msimamo wa CCM katika uongozi, ambapo ni mtu mmoja kofia moja na kiongozi yeyote hana sababu ya kujiuzulu nafasi aliyonayo kabla hajapata nafasi aliyoiomba, hivyo ameshauri nchi nzima wale waliojiuzulu nafasi zao kwa lengo la kugombea serikali za mitaa na hawakufanikiwa kuchaguliwa, warudi kwenye nafasi zao kwa kuwa wengi hawakuwa na sababu za msingi.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Iringa kwa siku mbili ambapo kesho atakuwa mgeni maalum katika uzinduzi wa chuo cha Mafunzo cha CCM Ihemi kitakachofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Japhet Mangula.

Imetolewa na:
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Iringa, amewahakikishia wanachama, mashabiki na wakereketwa wa CCM kuwa Chama hakipo tayari kupoteza jimbo la Iringa Mjini kama ilivyofanyika miaka michache nyuma.
Ndiyo CCM wamesha anza figisu figisu zao. Jimbo liko chini ya CDM wao wanasema hawako tayari kulipoteza. Swali wakiona wanalipoteza je unajua watafanya nini? Tusubiri mizengwe itakayofuata. Hizi ni dalili za ushenzi unaopikwa.
Zanzibar yule mama alituambia hushiki dola kwa vikaratasi tu, tukamcheka lakini alipotokea Jecha akiungwa mkono na JK na JPM tukamuelewa.
 
Hii ndio hizi trends tulizozingungumza humu
Na kwa Uchanguzi wa 2020
Formula hii itatumika kwa Majimbo yote yalichini ya upinzani, yatarejeshwa na Bunge la 2020-2025 litakuwa ni Bunge la chama kimoja CCM


P
 
Hawa ndo madaktari uchwara wanaopatikana bongo//tunapita kwenye wakati mgumu sana
Kupoteza au kutokupoteza jimbo ni maamuzi ya wananchi wala sio katibu mkuu wa chama, hawa ccm wana dharau sana wanaonaga wananchi kama mazombie/misukule isiyojitambua,isiyoweza kujua kiongozi gani anafaa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Egnecious,
Inaeleweka kuwa kwa kuwa CCM ni mabingwa wa kuiba kura, kwa kutumia Jeshi letu la Polisi, ndiyo maana anaongea kwa kiburi cha aina hiyo

Tukumbuke kauli iliyowahi tolewa na kada mwingine Humphrey Polepole, hapo siku za nyuma, nanukuu "uchaguzi ukifanyika kwa Uhuru na haki, CCM ijiandae kukabidhi Ikulu" mwisho wa kumnukuu
 
Wahehe mpo? Mnamsikia Mhaya huyo anayekuja kwenu kuwatukana kuwa maamuzi yenu hawezi kuyakubali lazima ya kwao ndio yawe?
Ana tofauti gani na gavana wa mjerumani aliyekataa maamuzi ya Mkwawa na watu wake kujipangia mambo yao akitaka ya kwao ndio yawe? Jee Mkwawa alikubali? La hasha, alionyesha ushujaa wake na ndio maana anakumbukwa mpaka Leo na wahehe wana heshimiwa.
Jee wahehe wa Leo CCM imewaona ni Mdebwedo hadi aje atambe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza,
Acha ukabila wewe jibu hoja ya msingi mpangaji anatakiwa kupisha mwenye nyumba yake anaitaka
 
Back
Top Bottom