Siasa zinafundisha mambo mengi sana. Baada ya JPM kutangazwa kuwa ameshalala usingizi wa milele, ukawa ndio mwanzo wa maisha mapya kwa watu wengi.
Wale waliokuwa wakiishi kiungwana bila kutaka kunyenyekewa waliendelea kupeta ndani ya mioyo yao wakiwa hawana sababu ya kuishi wakitegemea fadhila za Rais Samia.
Wale waliokuwa miungu watu maofisini mwao wakibebwa na jeuri waliyopewa na Hayati wakaanza kuwa wanyonge na wadogo sana mawazoni mwao.
Nilikuwa namwangalia Bashiru Ally mle ukumbini namna anavyojaribu kuwa sehemu ya furaha iliyokuwepo muda ule na mahali pale, alikuwa mnyonge sana nikakumbuka siku ile alipotukana wazee akitumia neno mpumbavu zaidi ya mara mbili kwa kujiamini kabisa.
Polepole kama kawaida anaongea kwa hamasa kubwa akisema ng'ara Samia ng'ara halafu baadae kidogo kwa unyonge analitaja jina la Saka Hamdu. Maisha yamejaa mafundisho.
Na Mungu kwa ufundi wake wa uumbaji hatupi hata dalili ya kutuonyesha ni lini itakuwa siku ya kuanza kupata funzo jipya, unaweza kulipata ukiwa kijana wa miaka 25 unaweza kulipata ukiwa mzee unayekaribia miaka 65.