Dkt. Bashiru piga moyo konde na usonge mbele

Dkt. Bashiru piga moyo konde na usonge mbele

Huyu Bashiru alikuwa na kauli za kuchochea chuki sana ni halali apumzikie huko bungeni akijibu maswali ya nyongeza
Akiuliza bana....ajibu kama nani?
Na pia atauliza ya jimbo gani?

Napataga hasira sana msomi akijitakia matatizo.
Usimdharau mtu.
Usimcheke mtu.
Usimdhanie mtu.
Usimsimange mtu.
Usimsengenye mtu.

Usimuone hawezi jambo fulani kwa sababu zako. Angeyajuwa haya.....asingeporomoka kiasi hicho.
 
Asante sana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan. Hakika kazi kubwa ya kumtoa Bashiru hapo Ikulu imekuongezea heshima kubwa mno. Nimefurahi mno unaepuka watu walioshiriki kwa kiasi kikubwa kuharibu Amani na Demokrasia Tanzania, kutesa watu na mambo mengi makubwa. Walioshirili kikubwa mno katika udikteta na ukandamizaji wa demokrasia. Walioshiriki na kutoa mbinu chafu za kugawa Tanzania kwa ukanda na ukabila. Mama yetu mpendwa RAIS leo umeliheshimisha Taifa la TANZANIA.
Mungu aendelee kukupa utulivu na umakini uendelee kusafisha na kupanga safu yako vizuri mno. Chanda chema huonekana Asubuhi. Hakika wewe ni chanda chema. Ninaiona Tanzania mpya ya Amani na FURAHA tena kwa watu wote na si kwa kikundi au kanda au kabila fulani. Mh. Rais wekeza pia juhudi katika kurejesha amani na Mshikamano bila kukali huyu katoka kanda ipi, kabila lipi na dini ipi.
Nimefurahi na Diplomasia umeitendea haki kabisa kwa kuangalia weledi. Tanzania mpya ndani na nje ya nchi.

I salute you Her Excellency, Samia Suluhu Hassan. May you be protected by Allah.
Hongera Mku sina maneno mengi kwa leo
Hongera
 
Kitu ambacho kinakiuma Mimi, katika wale Wabunge wa3 aliowateua Mama Samy, Wabunge wa2 wamekuwa mawaziri, Ila Mwalimu Bashiru Wala Hajateuliwa Kama Waziri. Naendelea Kusikitika Kwenye Hili.... #Silent Demotion [emoji19][emoji19][emoji19]
Mwalimu wako ni mjeuri sana hatunzi kauli zake hafai kuwa kiongozi wa kitaifa 'He does not keep his words and that he thinks he is more knwledgeable than others'
 
Amelaaniwa mtu yule anayemtegemea mwanadamu, na moyoni mwake amemuacha Mwenyezi Mungu.
Binadamu na project zetu hizi sio za milele
 
Ya Bashiru was so obvious atatemwa. SSH alikuwa very predictable kwenye hili. Na mhusika obviously alijua. Wanacheza chess wanaelewa sometimes kiongozi unapaswa kufanya unpredictable moves - keep your friends close BUT your enemies much closer.
 
Mimi sitaki Kuwa Muongo, Nimejikuta Nakuwa na Chuki Na Rais Kwa Sasa, Anisamehe Ila Moyo Wangu Umejaa Gadhabu Sana Juu Yake [emoji19][emoji19][emoji19]
 
Hivi wakati mh Rais aliyefariki anaomuondoa Ombeni Sefue kumuweka Kijazi mbona hukuja na utetezi wa aina hii?
Sefue alikuwa mwizi?
Wakati marehemu anatimua timua mlikuwa mnaruka ruka kwa furaha. Lakini leo anatimuliwa mjombako unaliia.
Machungu ambayo leo unayapitia ndiyo hayo waliyopitia wale mliowaita mafisadi.
Zamu yenu tulieni.
 
Sasa wale alio wanunua toka upinzani kwa gharama kubwa wamekuwa maboss wake. Yeye ana kwenda kukaa nyuma ajibiwe maswali yake na kina Waitara. Tamaa mbaya
Kitendo cha kununua wabunge wa upinzani, mleta mada ndiyo anakiita cha kizalendo kwa Bashiru.
Ile ni rushwa kama rushwa nyingine ambayo Bashiru aliisimamia
 
Sefue alikuwa mwizi?

SEFUE HAKUTIMULIWA KWA WIZI ILA KOSA LAKE LILIKUWA LOYALTY KWA VASCO DAGAMA!! JIWE ALIKUWA NA WASI WASI KUWA ANGEKUWA ANAVUJISHA SIRI YA MAMBO YAKE KWA MKWERE!!! JIWE ALIKUWA FISADI MITHILI YA DONALD TRUMP ,ANATAKA TOTAL LOYALTY TO HIM NA SIO KWA NCHI [ KATIBA]. NA HIYO NDIO HULKA YA MAFIA a.k.a DICTATORS!
 
Wakati nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam enzi zile Hayati Dr.

Magufuli akimalizia masomo yake ya Shahada ya Uzamivu, nilimtambua Dkt Bashiru kama Msomi, Mzalendo, Mjamaa na mpenda mabadiliko ya dhati kwa maendeleo ya wananchi.

Kamwe sikutarajia kama IPO siku Dkt Bashiru atakuwa sehemu ya Chama tawala wala Serikali iliyopo madarakani maana viongozi wenzake wangempinga na kumtenga kutokana na imani na itikadi yake ya kuwakomboa watanzania kutoka katika umasikini, rushwa, maradhi na ujinga.

Naamini 100% kwamba Dkt Bashiru pia hakuwahi kufikiria kugombea vyeo vya kisiasa wala nafasi za uongozi.

Hulka yake, uzalendo wake na uchapa kazi wake ndizo tunu zilizomgusa JPM hadi kumuona kama msaada mkubwa katika kurudisha nidhamu ya chama na uwajibikaji wa chama kwa wananchi. Kazi hiyo aliifanya vyema na kurejesha nidhani, Hadji na sifa ya chama katika jamii.

Mafanikio ya Bashiru katika Chama, yalimuaminisha Mheshimiwa Hayati JPM kwamba Bashiru anafaa kuziba pengo LA katibu Mkuu Kiongozi
Hakika ni kwamba uteuzi wa Bashiru kushika Ukatibu Mkuu wa Chama, uliwashangaza wengi kama ambavyo pia uteuzi wa Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ulivyowashtua wengi.

Leo hii, mheshimiwa Rais Samia ametengua uteuzi huo kwa kumteua katibu Mkuu Mwingine na Kumteua Dkt Bashiru kuwa Mbunge.

Mheshimiwa Bashiru, hiki ni kipimo cha ukomavu na weledi ndani ya kipindi kifupi.

Kuwa na moyo dhabiti na utulivu wa nafsi na kukubaliana na hali. Endelea kuchapa kazi kwa weledi, usithubutu kuungana na kundi lolote, simamia msimamo wako.

Tambua pia kwamba, mabadiliko makubwa uliyoanzisha katika chama yamekujengea chuki na uhasama mkubwa kwa mafisadi ndani na nje ya chama. Unapaswa kuchukua tahadhali zote za msingi.

Baada ya mtikisiko mfupi, utazidi kuwa imara zaidi na nyota yako itang'ara. Kila LA kheri katika Majukumu yako ya Kibunge, saidiana na Mh. Polepole kukiimarisha chama na kumuunga mkono kwa dhati Mama Yetu Samia Suluhu Hassan. Uamuzi wake usikurudishe nyuma, Songa Mbele
Kama ana ubavu si na ubunge apige chini tuone , mzalendo, uzalendo gani KWA BASHIRU tangu amepewa nafasi zile, BASHIRU uliemfaham kipindi kile hakua wa kipindi hichi,
 
Si ahame chama arudi chuo?

Back
Top Bottom