Dkt. Bashiru piga moyo konde na usonge mbele

kwangu hadi achomolewe Ali hapi,chalamila,Sabaye,polepole na gambo asipite tena hapo ntavuta Pepsi bariidi huku nikichangia mijadala ya humu jamii forum,wamewakashifu sana wazee wa chama kuwaambia zama zao zimekwisha,sasa kumbe kibao kimewageukia,wao walimtegemea mwanadamu wazee wakamtegemea mungu,.
Kwa hiyo kosa kubwa la Bashiru ni lipi hapo? Kurudisha mali za CCM walizo kuwa wamejimilikisha mafisadi papa ndani ya CCM - mzizi wa fitina dhidi ya Bashiru unakuwa driven na hilo - wanamtafutia kila mbinu kumukomoa na kumwaribia sifa, bahati nzuri Rais S.S.Hassan unajua viziri ukweli huko wapi ndio maana kampa wadhifa wa kibalozi na Ubunge for a good reason - watu baki ndio wenye maneno chungu mzima ya kutunga tu as if Dk. Bashiru amekuwa involved kwenye treasonable crime!!
 
Wakati nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam enzi zile Hayati Dr.

Magufuli akimalizia masomo yake ya Shahada ya Uzamivu, nilimtambua Dkt Bashiru kama Msomi, Mzalendo, Mjamaa na mpenda mabadiliko ya dhati kwa maendeleo ya wananchi.

Kamwe sikutarajia kama IPO siku Dkt Bashiru atakuwa sehemu ya Chama tawala wala Serikali iliyopo madarakani maana viongozi wenzake wangempinga na kumtenga kutokana na imani na itikadi yake ya kuwakomboa watanzania kutoka katika umasikini, rushwa, maradhi na ujinga.

Naamini 100% kwamba Dkt Bashiru pia hakuwahi kufikiria kugombea vyeo vya kisiasa wala nafasi za uongozi.

Hulka yake, uzalendo wake na uchapa kazi wake ndizo tunu zilizomgusa JPM hadi kumuona kama msaada mkubwa katika kurudisha nidhamu ya chama na uwajibikaji wa chama kwa wananchi. Kazi hiyo aliifanya vyema na kurejesha nidhani, Hadji na sifa ya chama katika jamii.

Mafanikio ya Bashiru katika Chama, yalimuaminisha Mheshimiwa Hayati JPM kwamba Bashiru anafaa kuziba pengo LA katibu Mkuu Kiongozi
Hakika ni kwamba uteuzi wa Bashiru kushika Ukatibu Mkuu wa Chama, uliwashangaza wengi kama ambavyo pia uteuzi wa Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ulivyowashtua wengi.

Leo hii, mheshimiwa Rais Samia ametengua uteuzi huo kwa kumteua katibu Mkuu Mwingine na Kumteua Dkt Bashiru kuwa Mbunge.

Mheshimiwa Bashiru, hiki ni kipimo cha ukomavu na weledi ndani ya kipindi kifupi.

Kuwa na moyo thabiti na utulivu wa nafsi na kukubaliana na hali. Endelea kuchapa kazi kwa weledi, usithubutu kuungana na kundi lolote, simamia msimamo wako.

Tambua pia kwamba, mabadiliko makubwa uliyoanzisha katika chama yamekujengea chuki na uhasama mkubwa kwa mafisadi ndani na nje ya chama. Unapaswa kuchukua tahadhari zote za msingi.

Baada ya mtikisiko mfupi, utazidi kuwa imara zaidi na nyota yako itang'ara. Kila LA kheri katika Majukumu yako ya Kibunge, saidiana na Mh. Polepole kukiimarisha chama na kumuunga mkono kwa dhati Mama Yetu Samia Suluhu Hassan. Uamuzi wake usikurudishe nyuma, Songa Mbele

Ningeshangaa sana kama Kuondolewa Kwake hapo Kusingewagusa ( Wauma ) nyie Wanafiki wenzake ambao mlikuwa mnafaidika nae hasa Kipesa kwa Vyeo vya Upendeleo, Unafiki na Ushirikina alivyopewa.

Kwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ninayemjua nilijua tu kuwa ingekuwa Ngumu kufanya Kazi na Msomi ( Mwanazuoni ) Mnafiki kama huyu ambaye hivi sasa mnajifanya Kumtia Moyo. Hii inaonyesha ni jinsi gani Team JPM mlivyokuwa Wazandiki na Opportunists pia.

Nikikuuliza ( Nikiwaulizeni ) tu Swali huyu Dkt. Bashiru Ali Kakurwa mnamtia Moyo hapa kwa lipi Jema alilofanya ndani ya CCM yenyewe na hata huko Serikalini alikokuwa kama Chief Secretary wa Hayati Dkt. Magufuli mtakuwa na Majibu ya kunipa?

Tena msiendelee Kutukera ( Kutuudhi ) zaidi tukaanza Kuanika Maovu yake hapa kisha mkajiona mlivyo Wapumbavu Waandamizi sawa? Na kama kuna Mtu ambaye alichochea Hayati Rais Dkt. Magufuli Kuchukiwa tena na hata CCM wenyewe ni huyu Dkt. Bashiru Ali Kakurwa alipokuwa Secretary General wa CCM na hata Kipindi Kifupi tu huko Serikalini kama Chief Secretary pia aliharibu vile vile kwa Kutengeneza Makundi ( Matabaka ) ya Kiutendaji.

Kama nyie ni Team JPM na Mimi sasa ni Team SSH na sasa tunawafyeka Mmoja Mmoja ndani ya Mfumo na Sisi tunaweka Watu wetu. Kutesa kwa Zamu na Hayati wenu atatusamehe tu na aendelee Kulala zake Salama huko aliko sasa ila Tanzania ya sasa ipo chini ya Mwanamama Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan basi.

Na ningemuona huyu Mtu Wenu Dkt. Bashiru Ali Kakurwa ana Akili kama baada ya Kutolewa kama CS Jana na Kuteuliwa Ubunge angekataa tu na afanye Mambo yake mengine ila alivyo wa hovyo Kakubali wakati Kiitifaki hapo Mama Kamtukana Bonge la Tusi ila Yeye hajajua tu. Unatolewa kuwa CS na kuwa Mbunge tena wa Kuteuliwa tu hili siyo Tusi?

Wapuuzi wakubwa nyie tumewachoka.
 
Hivi Ubunge si anatengeneza hela nyingi kuliko huo ukatibu mkuu kiongozi?

kuweni serious jamani
katbu mkuu ana pesa mingi kuliko mbunge. halaf job security ni kubwa wkt wabunge after 5 yrs hawana uhakika
 
Nidhamu kwenye chama iliyoleta ushindi wa asilimia 99% kwenye uchafuzi mkuu!
Hili ndilo lililomuangusha mchapakazi, mzalendo Bashiru.

Tuna safari ndefu mno!

Mh. Raisi wa awamu ya 6, ukishapokea kijiti cha uenyekiti wa chama, nanukuu kutoka kwa member mmoja humu, kila mwenye jimbo akalipiganie kivyake, waambie mamluki ya wabunge wa kupewa, 2025, kila mtu atakufa kivyake. Biashara za wewe kuwafanyia kazi, nileteeni Askofu Rashiidii, fyekelea mbali.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Huyu Bashiru alikuwa na kauli za kuchochea chuki sana ni halali apumzikie huko bungeni akijibu maswali ya nyongeza
Yeye siyo waziri au naibu hana mamlaka ya kujibu maswali ya nyongeza sana sana akae akisinzia tu, na anywe kahawa na kina Musukuma naye apigishwe story za kina Wema Sepetu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sasa wale aliowanunua toka upinzani kwa gharama kubwa wamekuwa maboss wake. Yeye ana kwenda kukaa nyuma ajibiwe maswali yake na kina Waitara. Tamaa mbaya
Mchezo ule ulikuwa WA kitoto Sana mnachukua majimbo yote halafu mnashindwa kuunda Bunge kulingana na matakwa na Sheria halafu mnaanza kuhangaika kuwatafuta Covid-19. Mama Samia anaonyesha hakufurahiwa Ila hakuwa na namna. Wamelipaka matope Taifa bila sababu yoyote.
 
Wakati nasoma chuo kikuu cha Dar es salaam enzi zile Hayati Dr.

Magufuli akimalizia masomo yake ya Shahada ya Uzamivu, nilimtambua Dkt Bashiru kama Msomi, Mzalendo, Mjamaa na mpenda mabadiliko ya dhati kwa maendeleo ya wananchi.

Kamwe sikutarajia kama IPO siku Dkt Bashiru atakuwa sehemu ya Chama tawala wala Serikali iliyopo madarakani maana viongozi wenzake wangempinga na kumtenga kutokana na imani na itikadi yake ya kuwakomboa watanzania kutoka katika umasikini, rushwa, maradhi na ujinga.

Naamini 100% kwamba Dkt Bashiru pia hakuwahi kufikiria kugombea vyeo vya kisiasa wala nafasi za uongozi.

Hulka yake, uzalendo wake na uchapa kazi wake ndizo tunu zilizomgusa JPM hadi kumuona kama msaada mkubwa katika kurudisha nidhamu ya chama na uwajibikaji wa chama kwa wananchi. Kazi hiyo aliifanya vyema na kurejesha nidhani, Hadji na sifa ya chama katika jamii.

Mafanikio ya Bashiru katika Chama, yalimuaminisha Mheshimiwa Hayati JPM kwamba Bashiru anafaa kuziba pengo LA katibu Mkuu Kiongozi
Hakika ni kwamba uteuzi wa Bashiru kushika Ukatibu Mkuu wa Chama, uliwashangaza wengi kama ambavyo pia uteuzi wa Bashiru kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ulivyowashtua wengi.

Leo hii, mheshimiwa Rais Samia ametengua uteuzi huo kwa kumteua katibu Mkuu Mwingine na Kumteua Dkt Bashiru kuwa Mbunge.

Mheshimiwa Bashiru, hiki ni kipimo cha ukomavu na weledi ndani ya kipindi kifupi.

Kuwa na moyo thabiti na utulivu wa nafsi na kukubaliana na hali. Endelea kuchapa kazi kwa weledi, usithubutu kuungana na kundi lolote, simamia msimamo wako.

Tambua pia kwamba, mabadiliko makubwa uliyoanzisha katika chama yamekujengea chuki na uhasama mkubwa kwa mafisadi ndani na nje ya chama. Unapaswa kuchukua tahadhari zote za msingi.

Baada ya mtikisiko mfupi, utazidi kuwa imara zaidi na nyota yako itang'ara. Kila LA kheri katika Majukumu yako ya Kibunge, saidiana na Mh. Polepole kukiimarisha chama na kumuunga mkono kwa dhati Mama Yetu Samia Suluhu Hassan. Uamuzi wake usikurudishe nyuma, Songa Mbele
Kwani BASHIRU ni Nani katika Nchi hii mpaka ASITENGULIWE? Alitenguliwa Waziri Mkuu Lowassa itakuwa Katibu Mkuu Acheni Ushamba
 
Mama ameanza kujaza wazanzibari wenzake kwenye serikali ya Tanganyika.

Ndio maana tunataka katiba mpya, kila mtu afanye yake.
Ni hatari sana. Chama tawala ukisifiwa na wapiinzani shtuka. Mama chonde chonde. Ila wananchi wa kawaida wanaona. Asihadaiwe na kushangiliwa mitandaoni.
 
Kwa hiyo kosa kubwa la Bashiru ni lipi hapo? Kurudisha mali za CCM walizo kuwa wamejimilikisha mafisadi papa ndani ya CCM - mzizi wa fitina dhidi ya Bashiru unakuwa driven na hilo - wanamtafutia kila mbinu kumukomoa na kumwaribia sifa, bahati nzuri Rais S.S.Hassan unajua viziri ukweli huko wapi ndio maana kampa wadhifa wa kibalozi na Ubunge for a good reason - watu baki ndio wenye maneno chungu mzima ya kutunga tu as if Dk. Bashiru amekuwa involved kwenye treasonable crime!!

Sio mali za ccm ni mali za wananchi zilizoporwa na ccm.
 
Kwa hiyo kosa kubwa la Bashiru ni lipi hapo? Kurudisha mali za CCM walizo kuwa wamejimilikisha mafisadi papa ndani ya CCM - mzizi wa fitina dhidi ya Bashiru unakuwa driven na hilo - wanamtafutia kila mbinu kumukomoa na kumwaribia sifa, bahati nzuri Rais S.S.Hassan unajua viziri ukweli huko wapi ndio maana kampa wadhifa wa kibalozi na Ubunge for a good reason - watu baki ndio wenye maneno chungu mzima ya kutunga tu as if Dk. Bashiru amekuwa involved kwenye treasonable crime!!
inamaana zile kauli zake we zikikunogea?
 
Akishindwa kusonga Mbele Asonge hata Ugali tuu!!

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom