Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei Mbunge mtarajiwa Vunjo

Uchaguzi 2020 Dkt. Charles Kimei Mbunge mtarajiwa Vunjo


Habari za asubuhi wadau. Hapa Marangu Mamba Komakundi kibaridi ni kikali 12 centigrade.

Wapambe ni wengi nyumbani kwa Dokta Kimei hapa baada ya kujua Dokta atachukua fomu ya Ubunge Jimbo hili la Vunjo kupitia CCM.

Wapinzani wake wengi bado ni wachovu kama DC wa Zamani Chonjo.
Kila la heri Dokta Kimei.

Mwakeye
huyo mzee nae apumzike doohh hatari atapeleka wapi ela zote hizo jamani
 
Mama Samia Makamu wa Rais alisema akiwa Kilimanjaro na hasa akiwa Machame. "Mnataka watu wenu wawepo kwenye Serikali lakini hamtupi watu wa kufanya nao kazi, Tutafutieni watu wa kufanya nao kazi na muone sisi tunafanya nini".

Tukiwa kwenye maamuzi hatuna mtu wa kutuambia habari za Kilimanjaro. Naona sasa hivi watu wanajipanga kupata watu wa kwenda kusema kwenye vikao vya maamuzi. Wachaga sio wajinga Meli ndio inaondoka hivyo, lazima watu wajisogeze jikoni wakikosa kukomba basi waonjee tuu mboga. Na kutakuwa na mabadiliko sana uchaguzi huu. Tusubiri tuone.
 

Habari za asubuhi wadau. Hapa Marangu Mamba Komakundi kibaridi ni kikali 12 centigrade.

Wapambe ni wengi nyumbani kwa Dokta Kimei hapa baada ya kujua Dokta atachukua fomu ya Ubunge Jimbo hili la Vunjo kupitia CCM.

Wapinzani wake wengi bado ni wachovu kama DC wa Zamani Chonjo.
Kila la heri Dokta Kimei.

Mwakeye
Bora wampe huyu kuliko Mbatia ndumila kuwili
 
Huyu aingii ubunge kutafuta hela
Mara 100 watu kama Hawa kuliko Hawa njaa kali

Ova
Nani kakuambia kuwa utamu wa pesa huwa una kikomo.Kadiri mtu anavyokuwa nazo nyingi,ndo tamaa ya kupata zaidi inavyoongezeka.Mtu hasemi KWAMBA anataka ubunge kwa sababu Kuna pesa nyingi,Huwa wanaficha hizo tamaa na maslahi yao binafsi kwa kusema ati anataka kuwatumikia wananchi..Tazama Jinsi ambavyo wakuu wa mikoa wanavyotamani ubunge(ati akawatumikie wananchi).Kwani katika nafasi ya ukuu wa mkoa,so kila cku unawatumikia wananchi? HATUDANGANYIKI ! We kama unataka ubunge,we gombea TU ki-vyako.Sio ati unagombea kwa kuwa unataka kututumikia.NOOO !
 
Wewe ndo umesema ukweli..Akishapata ubunge,na au pia uwaziri,Utashangaa huyu jamaa aliyekuwa anasifiwa Ana akili,AKILI ZOTE ZINAPIGWA "Lock-down".
Tatizo kubwa si kupata Ubunge bali ni pale atakapoupata tu uwezo wake na akili zake atalazimika kuziacha pale kwenye ofisi ndogo ya ccm Marangu na kuvalishwa zile za kiccm.

Kwa maana hiyo hata akishinda tusitarajie mabadiliko.
 
Huyu mzee kwa pesa zote za crdb ajaridhika Hadi apate na za ubunge
 
Hiyo ofisi hapewi mchaga hata wakimroga Magu.

Magu anakwambia, hapendwi mtu, inapendwa pesa kwake. Magu amefanya kazi kubwa sana kuwatoa wachaga Hazina na TRA hawezi fanya ujinga huo. Kimei amejaza wachaga kila tawi la CRDB, Magu hawezi ruhusu warudi sehemu nyeti za pesa ya nchi hii akiwa madarakani.
KAMA MTU ANA UWEZO NI HAKI YAKE KUPEWA NAFASI
HIYO HABARI YA KUPENDELEA WACHAGA NI KUENEZA TU CHUKI ZA KIKABILA
 
13 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Polepole : Mabango au Vipeperushi viwe vya ktk nguzo au mtandaoni haviruhusiwi na CCM Mpya

Watia nia ktk kutaka kuteuliwa kugombea uongozi wa nafasi vyombo vya dola kupitia CCM Mpya wasomewa makatazo ikiwemo vipeperushi ktk mitandao ya kijamii
 
KAMA MTU ANA UWEZO NI HAKI YAKE KUPEWA NAFASI
HIYO HABARI YA KUPENDELEA WACHAGA NI KUENEZA TU CHUKI ZA KIKABILA
Ni kusema ukweli ulio wazi. Kuwawezesha kabila moja kiuchumu kwa kuwapa ajira, kunawapa purchasing power ambao wasio na hizo ajira hawana, na unawapa nguvu ktk jamii kuliko wasionacho.

Uwezo alio nao wako wengi wenye nao pia. Nakumbuka kabla ya Magu, kama jamii tuliamishwa miaka nenda rudi, wasomi wa nchi hii ni wa sehemu fulani tu. Ombaomba ni wa sehemu fulani. Kumbe kila jamii inavichwa, walikuwa hawpati fursa tu.
 
Siwakubali watia nia/wagombea wengi kwa ticketi ya CCM kwa sababu wengi ni wanafiki na wachumia tumbo . Lakini Dr. Charles Kimei namkubali kwa asilimia 101 na kwa vyovyote ni "Potential Minister" kwenye baraza lijalo. Hivyo nawaomba wana vunjo wamchague fasta ili tumpate waziri asieangaishwa na njaa.
 
Back
Top Bottom