Nsoji go Nvaa
JF-Expert Member
- Oct 15, 2019
- 999
- 1,948
Ummy mmoja ni sawa na gwaji girl buku.Kumbe bora hata ka dada Ummy "mtoa matangazo ya corona"kwanza Ummy Ni karembo katoto ka kitanga kale ila huyu mwehu Dr Gwajima ovyo kabisa
Lile ni empty jar😂Yule Mama amejaa ulimbukeni na ushamba,binafsi nilikuwa sijawahi kumsikiliza speech zake.Majuzi kwenye speech ya kumpokea Rais wa Mozambique ndipo nilijua hamna kitu mule.
Mbona wewe hujaweka clip ya Dorothy akidhalilisha hai madaktari?Nisaidie kuweka clip hiyo hapa uone anavyoshika kiuno.
Mwache afanye anavyotaka, yenye si ndo boss au? Wewe umemwona huyo tu? Mbona Mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo, tutulie, tuifanye kazi kila mmoja atimize wajibu wake
Mleta uzi akili yake haiko sawa, nadhani niishie hapa.Hapana wewe ndiye una upungufu wa uelewa. Pamoja na mapungufu yaliyopo ya eekta ya afya, ila kulikuwa na wizi sana na mlizooea kuiba mno na kutoa huduma mbovu bila kujua wajibu wenu. Acha awanyooshe kabisa mlijijaza uzembe. Kikubwa mfano wa kuacha kutumia GOT HOMIS sekta ya afya inaibiwa mno. Pia waziri huyu anayo dhamira ya kazi toka moyoni mwake. Labda lile tukio la mkunga ndiyo linahitaji busara juu yake.
Tatizo ni jiwe ndio anataka mawaziri wake wawe,unakumbuka aliwahi kumwambia waziri mmoja avute bangi ili awe mkali sana?Wizara ya afya ni nyeti sana kama ilivyo ya ulinzi, inahitaji utulivu na umakini sana kuiongoza.
Huyu mama ana nia njema ila njia anayotumia ya kupayuka hadharani ndio mbovu.
Asipokuwa makini ataishia njiani.
KaribuSawa mpenzi.
Kwani Dr Dorothy ndo kasema maneno hayo? Aliyesema hayo maneno ni mchangiaji Kama wewe.Aliyemwambia kuwa watu wanaitaka nafas yake ni nani?
Ye afanye kazi kistaarabu, aache kudhalilisha watumishi wake...
Ila nadhan "ndoa" yake ina walakini...ama kuna shida kichwan hayuko sawa
watanzania mmejaaliwa kwa kupigana majungu na fitina,Tahadhima kwenu wajumbe wa bodi huru!
KWA muda sasa nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu Waziri huyu toka alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Afya. Namzungumzia Dk. Dorothy Gwajima.
Kila ofisi zilizochini yake anapoingia huwadhalilisha sana madaktari wenzake. Dk. Gwajima anamtazama kila mtu kuwa ni mwizi na kujitapa kuwa hakuna anayejua kila kitu katika wizara hiyo kama yeye.
"Hivi mnajua mimi ni Field Marshal wa sekta ya afya?" anawafokea madaktari Bingwa zaidi yake na kuongeza, "kama ningekuwa Mwanasheria mngenidanganya sana" kuonesha kuwa mtangulizi wake Mwanasheria, Ummy Mwalimu alikuwa akidanganywa sana. Huku ni kumdharau Waziri mwenzie aliyeaminiwa na Rais Magufuli.
Lakini hata "body language" ya mama huyu inaonesha kuhemka mno kiasi Cha kufanana na kina mama "ndala ndefu" wa huko Tandale wanaochambana bombani huku ameshika kiuno.
Cha ajabu, kama alivyowahi kufanya Dk. Hamisi Kigwangala "mzee wa kukurupuka" naye kila anapotaka kuwadhalilisha wahudumu wa sekta hiyo ni lazima awe mbele ya kamera ili aonekane. Huyu mama ameenda mbali kiasi Cha kutorokwa hata na haiba na staha ya mwanamke wa Kitanzania mbele ya wanaume.
"Field Marshal" ni cheo Cha juu na Cha mwisho jeshini. Hivi, Dk. Gwajima anadhani ni Bingwa wa afya kuliko maprofesa wote wa tiba nchini? Kwani kuongoza ni lazima kudhalilisha wenzako hadharani?
Wakati yule "mkata viuno" aliyetembea na Ilani ya CCM akijiita "ninja" huyu kaja na skafu ya bendera akijiita "Field Marshal". Mwendo uleule wa kukurupuka na kujipendekeza.
My Take: Napendekeza madaktari wafuatilie faili lake la matibabu anakotibiwa kuona anasumbuliwa na ugonjwa gani? Yapo baadhi ya magonjwa ambayo humfanya mtu ku-react ukichaa kama mama huyu.
Lakini pia wadadisi wachunguze mahusiano yake ya ndoa. Je, ana familia au ni mtalikiwa? Maana mahusiano ya ndoa na familia yakiwa salama pia huleta utulivu katika uongozi wenye staha, hekima, busara na maarifa. Huwezi kukufanya kuwa wizara hiyo imeoza kiasi kwamba waliopita kabla yake hawakufanya chochote. By the way, si tunaambiwa utawala wa Magufuli umeondoa ufisadi na uzembe kazini?
Nawasilisha.