Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Huyu mh anaweza kuwa ana nia nzuri lakini approach yake amefeli hata kabla hajaanza kazi vizuri. Kuna sehemu hazihitaji siasa na macamera camera. Zinahitaji ushirikiano baina ya wadau ili matatizo yatatuliwe.

Mwisho wa siku anayeumia ni mwananchi na sio Dr wala waziri.

Mfano hospital kalibia zote hakuna dawa lakini kwakua ni tatizo la serikali hutamsikia analiongelea atajikita na mambo yanayompa kiki tu.. watoto na wazee HAWATIBIWI BURE. Hilo k
Hutamkuta akiliongelea. Anaongelea mambo yanayompa kiki ili ashangiliwe na wananchi.
 
Yule Mama amejaa ulimbukeni na ushamba,binafsi nilikuwa sijawahi kumsikiliza speech zake.Majuzi kwenye speech ya kumpokea Rais wa Mozambique ndipo nilijua hamna kitu mule.
 
Nilidhani ni mie tu nimeliona hili.Huyu mama hayupo sawa,yani ni tafrani na kituko machoni pa watu.


Aibu aibuuu
 
Umesahau kuwa wanaoteuliwa ni vichaa kama baba yao aliyewateua?,na kwa mjibu ya aliyewateua bila kufanya kazi kama kichaa kazi imekushinda.
 
Katika nafasi ya uwaziri naungana nanyi kwamba amepanic na anajikuta hajui msaidizi yupi anaweza kumfaa na yupi ampatie majukumu gani, pia ana tatizo la kuamini vile anavyojua yeye ndio sahihi.

Kuhusu kuleta mabadiliko, aliweza alipokua TAMISEMI kwasababu baadhi ya mbinu zake zilihusisha kuimarisha mfumo mzima wa utendaji kazi vituoni, tofauti na sasa ambapo anatoa matamko yasiyokua na mbinu mbadala za utatuaji.

Kikubwa kinachomtesa ni ahadi ya chama chake kuhusu Bima ya Afya kwa wote iliyotolewa kwenye ilani, ukizingatia Bima hiyo anaifahamu vizuri utekelezaji wake katika kundi kubwa ni mgumu, maana ni yeye alieianzisha akiwa Iramba, ikaja kumsumbua akiwa RMO Singida baada ya kuhamisha makusanyo kutoka wilayani kuja mkoani. Kwahiyo anajaribu kuhamasisha wananchi wajiunge lakini anajua kabisa ile bima ni tatizo.

Kuhusu watu anaowatuhumu kuwa wezi na waongo (amemuambikiza na naibu wake), ni ngumu sana kuwa sahihi kwenye utunzaji wa rekodi za matumizi ya dawa, hasa kutokana na changamoto ya upungufu wa watumishi iliyopo nchini. Bahati mbaya sana Mama haamini kwenye uhaba wa watumishi, yeye anadai watumishi wapo wa kutosha lakini hawawajibiki.

Kujiita Field Marshal nadhani yupo sahihi kwenye sekta yake (tuzingatie kwamba hajasema yeye ni Field Marshal wa sekta ya afya, amesema yeye ni Field Marshal kwenye masuala ya uongozi wa sekta ya Afya).

Ni sahihi kabisa kwasababu ni mtu alietoka chini kabisa, japo kwenye CV yake haijaonesha lakini inasemekana alianza kuhudumu kama RMA ndipo akapanda hadi kufikia MO, kaongoza kuanzia Zahanati, Wodi, Kituo cha Afya, Kitengo cha hospitali, hospitali, Idara ya afya wilaya, Idara ya Afya mkoa, kurugenzi ya huduma za afya katika wizara ya afya, bodi mbalimbali za hospitali na huduma za afya, Ofisi ya raisi - Afya na sasa Waziri wa Afya. Hauwezi kukuta yeyote mwenye experience zinazokaribiana nae.
 
Nisaidie kuweka clip hiyo hapa uone anavyoshika kiuno.
Mbona wewe hujaweka clip ya Dorothy akidhalilisha hai madaktari?
Sasa iweje utake clip wakati wewe OP umeleta umbeya tuu bila picha?
 
Kwa hiyo ukiwa boss ndo unafanya tu unavyotaka? Wizara ya afya ni kampuni yake binafsi?
Mwache afanye anavyotaka, yenye si ndo boss au? Wewe umemwona huyo tu? Mbona Mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo, tutulie, tuifanye kazi kila mmoja atimize wajibu wake
 
Hapana wewe ndiye una upungufu wa uelewa. Pamoja na mapungufu yaliyopo ya eekta ya afya, ila kulikuwa na wizi sana na mlizooea kuiba mno na kutoa huduma mbovu bila kujua wajibu wenu. Acha awanyooshe kabisa mlijijaza uzembe. Kikubwa mfano wa kuacha kutumia GOT HOMIS sekta ya afya inaibiwa mno. Pia waziri huyu anayo dhamira ya kazi toka moyoni mwake. Labda lile tukio la mkunga ndiyo linahitaji busara juu yake.
Mleta uzi akili yake haiko sawa, nadhani niishie hapa.
 
Wizara ya afya ni nyeti sana kama ilivyo ya ulinzi, inahitaji utulivu na umakini sana kuiongoza.

Huyu mama ana nia njema ila njia anayotumia ya kupayuka hadharani ndio mbovu.

Asipokuwa makini ataishia njiani.
Tatizo ni jiwe ndio anataka mawaziri wake wawe,unakumbuka aliwahi kumwambia waziri mmoja avute bangi ili awe mkali sana?
 
Sawa daktari tumekusikia.
Kumbuka mwenzio mwisho wa siku anapokea mshahara wake
 
Aliyemwambia kuwa watu wanaitaka nafas yake ni nani?

Ye afanye kazi kistaarabu, aache kudhalilisha watumishi wake...


Ila nadhan "ndoa" yake ina walakini...ama kuna shida kichwan hayuko sawa
Kwani Dr Dorothy ndo kasema maneno hayo? Aliyesema hayo maneno ni mchangiaji Kama wewe.
 
Kama ilivyo desturi
Kila darasa kuna mtu mmoja mwenye vituko hivyo hivyo kwa familia....kijiji...ukoo...
Hata vikundi vya hisa.

Na kila awamu kuna waziri mmoja atakuwa na show off sana.
Ila naona awamu hii imetokea kwenye uhai wa mtu.
Mungu awape nguvu madaktari wasitekeleze kwa lengo la kumkomoa
 
Tahadhima kwenu wajumbe wa bodi huru!

KWA muda sasa nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu Waziri huyu toka alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Afya. Namzungumzia Dk. Dorothy Gwajima.

Kila ofisi zilizochini yake anapoingia huwadhalilisha sana madaktari wenzake. Dk. Gwajima anamtazama kila mtu kuwa ni mwizi na kujitapa kuwa hakuna anayejua kila kitu katika wizara hiyo kama yeye.

"Hivi mnajua mimi ni Field Marshal wa sekta ya afya?" anawafokea madaktari Bingwa zaidi yake na kuongeza, "kama ningekuwa Mwanasheria mngenidanganya sana" kuonesha kuwa mtangulizi wake Mwanasheria, Ummy Mwalimu alikuwa akidanganywa sana. Huku ni kumdharau Waziri mwenzie aliyeaminiwa na Rais Magufuli.

Lakini hata "body language" ya mama huyu inaonesha kuhemka mno kiasi Cha kufanana na kina mama "ndala ndefu" wa huko Tandale wanaochambana bombani huku ameshika kiuno.

Cha ajabu, kama alivyowahi kufanya Dk. Hamisi Kigwangala "mzee wa kukurupuka" naye kila anapotaka kuwadhalilisha wahudumu wa sekta hiyo ni lazima awe mbele ya kamera ili aonekane. Huyu mama ameenda mbali kiasi Cha kutorokwa hata na haiba na staha ya mwanamke wa Kitanzania mbele ya wanaume.

"Field Marshal" ni cheo Cha juu na Cha mwisho jeshini. Hivi, Dk. Gwajima anadhani ni Bingwa wa afya kuliko maprofesa wote wa tiba nchini? Kwani kuongoza ni lazima kudhalilisha wenzako hadharani?

Wakati yule "mkata viuno" aliyetembea na Ilani ya CCM akijiita "ninja" huyu kaja na skafu ya bendera akijiita "Field Marshal". Mwendo uleule wa kukurupuka na kujipendekeza.

My Take: Napendekeza madaktari wafuatilie faili lake la matibabu anakotibiwa kuona anasumbuliwa na ugonjwa gani? Yapo baadhi ya magonjwa ambayo humfanya mtu ku-react ukichaa kama mama huyu.

Lakini pia wadadisi wachunguze mahusiano yake ya ndoa. Je, ana familia au ni mtalikiwa? Maana mahusiano ya ndoa na familia yakiwa salama pia huleta utulivu katika uongozi wenye staha, hekima, busara na maarifa. Huwezi kukufanya kuwa wizara hiyo imeoza kiasi kwamba waliopita kabla yake hawakufanya chochote. By the way, si tunaambiwa utawala wa Magufuli umeondoa ufisadi na uzembe kazini?

Nawasilisha.
watanzania mmejaaliwa kwa kupigana majungu na fitina,
mkimuona kiongozi yuko makini na anabana ubadhirifu basi njia pekee ya kumchafua ni kuanzisha majungu na fitina.
nashauri viongozi wa juu kamwe wasisikilize na kufuata majungu na fitina maaana tabia hii imeshamiri sana.....isiachwe ipigwe vita. utafiti unaonyesha viongozi weledi huwa wana undiwa zegwe/jungu na kikundi cha watu wachache, Majungu na fitina ni mbinu pekee ya kuwaondoa viongozi wazuri na weledi, kamwe mamlaka za uteuzi msikubali kuendeshwa au kusikiliza majungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom