mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Wapenzi wa JPM hatupo kama nyie, tukiona ovu tunasema wazi kama alivyofanya muungwana Jane Lowassa hata Na mama D ni muungwana.
Ni kweli kila anapopita Waziri anakutana na madudu yanayofanywa na watendaji wake, kuongea au kukaa kimya na kwenda kuyafanyia kazi ni hulka ya mtu, lakini pia kama kiongozi kuwaambia watendaji ukweli wa anachokijua haswa pale wanapomdanganya ni sawa.
Na kwa mambo anayokutana nayo waziri ni wazi kuwa wizara imekosa controls; ni kama vile hakuna process flows sahihi na manuals.... kitu kinachotoa mwanya kwa watendaji kufanya ubadhirifu wa mali na muda. Na kama zipo basi zina gap au hakuna monitoring
Ni bahati kwamba Waziri ni mtaalam wa sekta anayosimamia na naamini atakapokaa chini na wasaidizi wake akafanya review atakuja na suluhu
Maendeleo hayana vyama kolola 😍😍