Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Sijasema wote nimesema wengi,hivyo ndio walivyo hadi imefikia ukimkuta Daktari mpole na anakusikiliza unaona ni kitu cha tofauti na kawaida ilivyo. Inawezekana kweli wanakuwa na stress zao za kazi ila sio sababu ya kuhamishia hizo stress kwa wagonjwa na kutoa huduma mbovu lazima wakumbuke wana deal na afya za watu.
Kuna wagonjwa wanaongeaga vibaya sijui unapata wapi hamu ya kumuhudumia, swala la huduma linatakiwa liwe la kiushirikianao mgonjwa awe tayari kupata huduma na kwa upole sio kwa hasira
 
Wakuu habari za mchana.
Naomba walio karibu na huyu mama waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wampe semina ya ku-behave kama top government official. Naona hilo linamshinda. Mama atulize ubongo aje na solutions. Aache majungu na malalamiko kila kukicha.

Hizi clip tunazoziona hazimpi heshima kabisa. Anajiita Field Marshall wa wizara lkn mimi namuona bado sana.
Kama ana vinyongo na maumivu ya huko nyuma, asahau. Ajulishwe majukumu yake kama waziri. Aache kuleta viswahili kama vya vijiwe vya kina mama wakiwa peke yao.
Mama ana nyongo sana na atafeli mapema mno.
Hawajui wabongo vizuri, ukijifanya mnoko sana lazima wakufanyizie
 
Hiv jf huwa wanatuungia tu-MB twa bure nini, siku hizi tuvideo tunatorushwa Jf natucheki bila shida yoyote [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Dorothy ungekuwa mkulima wewe cjui, ila bora ww, ndalichako mhhh apana[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38].

Mi-five tenaaaaaaaa, understood??
Hao wanawake wawili ni takataka kabisa.
 
Sasa hapo anasafisha au anachamba!?
Kila clip anaonekana akichamba wenzie na kuwadharau
Watu wanamlalamikia kwa kujifanya anajua kuliko mtu yeyote kwenye hio wizara
Anamdharau mpaka mtangulizi wake ummy kana kwamba hakuna alichofanya mpaka anakuja yeye
Inaonekana amezoea kuchambana huko vijiweni
Shame!
Mkuu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nimesoma post yako hii nikamvutia picha anavyoongea dah mpaka mbavu zimeuma
 
Kuna wagonjwa wanaongeaga vibaya sijui unapata wapi hamu ya kumuhudumia, swala la huduma linatakiwa liwe la kiushirikianao mgonjwa awe tayari kupata huduma na kwa upole sio kwa hasira
Kwahiyo hao madktari nao wanashindana na hao wagonjwa kwa kuongea vibaya? ukiona mgonjwa anaongea vibaya ujue teyari ametibuliwa na Daktari,yani daktari anataka akupe maneno mabaya akukolomee halafu wewe uwe mpole tu kisa yeye daktari.
 
Watumishi wa afya mahospitalini ni miungu watu. Acha awanyooshe tu.

Tatizo lake analalamika tu, hachukui hatua.
 
Mama ana nyongo sana na atafeli mapema mno.
Hawajui wabongo vizuri, ukijifanya mnoko sana lazima wakufanyizie
Ndio maana basi Ummy mwalimu anasifiwa,pengine sio alikuwa anafanya kazi vizuri bali hakuwa mnoko.
 
Wakuu habari za mchana.
Naomba walio karibu na huyu mama waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wampe semina ya ku-behave kama top government official. Naona hilo linamshinda. Mama atulize ubongo aje na solutions. Aache majungu na malalamiko kila kukicha.

Hizi clip tunazoziona hazimpi heshima kabisa. Anajiita Field Marshall wa wizara lkn mimi namuona bado sana.
Kama ana vinyongo na maumivu ya huko nyuma, asahau. Ajulishwe majukumu yake kama waziri. Aache kuleta viswahili kama vya vijiwe vya kina mama wakiwa peke yao.
Ati anasema anafanya kazi afya miaka mingi halafu hajui kwamba dawa za serikali huwa hazitoshi?? Kama hazitoshi hizo za kuiba zinatoka wapi??? Naongea kwa experience yangu ya kuwa CHMT
 
Tahadhima kwenu wajumbe wa bodi huru!

KWA muda sasa nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu Waziri huyu toka alipoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Afya. Namzungumzia Dk. Dorothy Gwajima.

Kila ofisi zilizochini yake anapoingia huwadhalilisha sana madaktari wenzake. Dk. Gwajima anamtazama kila mtu kuwa ni mwizi na kujitapa kuwa hakuna anayejua kila kitu katika wizara hiyo kama yeye.

"Hivi mnajua mimi ni Field Marshal wa sekta ya afya?" anawafokea madaktari Bingwa zaidi yake na kuongeza, "kama ningekuwa Mwanasheria mngenidanganya sana" kuonesha kuwa mtangulizi wake Mwanasheria, Ummy Mwalimu alikuwa akidanganywa sana. Huku ni kumdharau Waziri mwenzie aliyeaminiwa na Rais Magufuli.

Lakini hata "body language" ya mama huyu inaonesha kuhemka mno kiasi Cha kufanana na kina mama "ndala ndefu" wa huko Tandale wanaochambana bombani huku ameshika kiuno.

Cha ajabu, kama alivyowahi kufanya Dk. Hamisi Kigwangala "mzee wa kukurupuka" naye kila anapotaka kuwadhalilisha wahudumu wa sekta hiyo ni lazima awe mbele ya kamera ili aonekane. Huyu mama ameenda mbali kiasi Cha kutorokwa hata na haiba na staha ya mwanamke wa Kitanzania mbele ya wanaume.

"Field Marshal" ni cheo Cha juu na Cha mwisho jeshini. Hivi, Dk. Gwajima anadhani ni Bingwa wa afya kuliko maprofesa wote wa tiba nchini? Kwani kuongoza ni lazima kudhalilisha wenzako hadharani?

Wakati yule "mkata viuno" aliyetembea na Ilani ya CCM akijiita "ninja" huyu kaja na skafu ya bendera akijiita "Field Marshal". Mwendo uleule wa kukurupuka na kujipendekeza.

My Take: Napendekeza madaktari wafuatilie faili lake la matibabu anakotibiwa kuona anasumbuliwa na ugonjwa gani? Yapo baadhi ya magonjwa ambayo humfanya mtu ku-react ukichaa kama mama huyu.

Lakini pia wadadisi wachunguze mahusiano yake ya ndoa. Je, ana familia au ni mtalikiwa? Maana mahusiano ya ndoa na familia yakiwa salama pia huleta utulivu katika uongozi wenye staha, hekima, busara na maarifa. Huwezi kukufanya kuwa wizara hiyo imeoza kiasi kwamba waliopita kabla yake hawakufanya chochote. By the way, si tunaambiwa utawala wa Magufuli umeondoa ufisadi na uzembe kazini?

Nawasilisha.
Mama yeye si alikuwa analima hadi alizeti singida Hapo maana mshahara ulikuwa hautoshi sasa anategemea mtu anayelipwa 300000 kwa miaka sita bila ongezeko lolote la maana asipokee rushwa
 
Kwahiyo hao madktari nao wanashindana na hao wagonjwa kwa kuongea vibaya? ukiona mgonjwa anaongea vibaya ujue teyari ametibuliwa na Daktari,yani daktari anataka akupe maneno mabaya akukolomee halafu wewe uwe mpole tu kisa yeye daktari.
Tuliache hilo, wewe elewa unavyoelewa
 
Ndio maana basi Ummy mwalimu anasifiwa,pengine sio alikuwa anafanya kazi vizuri bali hakuwa mnoko.
Tatizo kubwa nchi hii viongozi wetu hawatumii AKILI ZAO bali akili za mwenyekiti anataka nini.
Kila mtu anajitutumua ili kumbariki mwenyekiti...hawajui wanaumiza wengine.
Nchi hii ukiwa na hekima na busara ni rahisi mno kuongoza na kuwa na positive outcome.
Mfano mzuri ni mwl Nyerere aliongozwa na busara hekima na utu.
Hivyo Watanzania walimfuata kama mchungaji wa kondoo wa Kiisrael.
 
Huyu mama kiukweli anapiga kazi pia ni mfuatiliaji mzuri lakini apunguze sifa, majigambo na kujikweza. Hivi vitu vitatu ndivyo vinamharibia.....
Hivi kama kila mtumishi, DED, wakuu wa idara, wazoa taka, wachimbaji wa mitaro etc etc wakawa kila kazi wanayoenda kufanya wanaita waandishi wa habari ili irushwe hii nchi si itageuka kuwa nchi ya propaganda kama enzi za Soviet union?? Kwa nini kila mahala lazima waongizane na waandishi wa habari?? Hii ndiyo sababu kuuu ya kuishiwa hoja za kusema maana kila siku wewe uko kwenye media, sasa utazungumza mangapi kwa mwaka mzima maana key problems za sekta ya afya zinafanana na zinajulikana. Alianza vizuri but sasa amekuwa kama mipasho ya akina mzee Yusufu au Juma Lokole... Too much aisee...
 
Hapana wewe ndiye una upungufu wa uelewa. Pamoja na mapungufu yaliyopo ya eekta ya afya, ila kulikuwa na wizi sana na mlizooea kuiba mno na kutoa huduma mbovu bila kujua wajibu wenu. Acha awanyooshe kabisa mlijijaza uzembe. Kikubwa mfano wa kuacha kutumia GOT HOMIS sekta ya afya inaibiwa mno. Pia waziri huyu anayo dhamira ya kazi toka moyoni mwake. Labda lile tukio la mkunga ndiyo linahitaji busara juu yake.
GotTHoMis IPO ipo wala haipewi kipaumbele wala serikalini haijawezaka sana huko .dunia ya sasa ili kuzuia wizi huna budi kuwekeza Kwenye electronic system .maana ndo njia sahihi ya kufanya auditing na kurahisisha kazi .sasa leo hii unapamabana na issued voucher kitu ambscho kila mtu naweza kutempa nacho
 
Back
Top Bottom