Dkt. Hassan Abass: Pato la Tanzania limekua mara mbili zaidi katika miaka minne ya Rais Magufuli

Dkt. Hassan Abass: Pato la Tanzania limekua mara mbili zaidi katika miaka minne ya Rais Magufuli

Pato la Taifa mwaka 2015 lilikuwa dola za kimarekani bilion 47, sawa na shilingi Trillion 108 za kitanzania. Huyu msemaji aache maneno yake ya kubumbabumba!

Pia wingi wa watu mwaka 2015 ulikuwa mdogo kulinganisha na sasa

Huyu msemaji aache propaganda zisizo na kichwa wala miguu, ipo siku ataleta GDP ya wakati Nyerere anang'atuka halafu atasema Magufuli kakuza GDP ya Taifa mara 50 kuliko miaka 35 iliyopita!

Tatizo ni kuwa serikali hii inalazimisha kuonyesha mafanikio ya kiuchumi ambayo hayapo!
 
Uchumi wa kati katika viwango vya kati na juu huwa na viashiria vya uwezo wa serikali kulipa fao la kukosa ajira kwa wananchi wake wenye sifa za kuajiriwa lakini uchumi umeshindwa kutoa fursa ya ajira kwa sababu za msingi.

Wanachotofautiana madaktari hawa wawili mmoja wa Falsafa na mwingine wa heshima ni kitu kidogo sana, serikali ya Mkapa iliamini katika sekta binafsi kukuza uchumi.
Waliposema 2025 tutaingia uchumi wa kati kwa per capita ya $ 3000 walimaanisha hapo ndipo uchumi utaanza kufungua fursa kwa wote wanaostahili na sekta binafsi ikishindwa kutoa ajira kwa wote basi uchumi unaweza kuwafidia waliokosa ajira kwa kuwapa fao la kukosa ajira ambalo halitazidi per capita iliyokubalika ambayo ni $ 3000 yaani fao lisilozidi sh 500,000 kwa mwezi.

Yawezekana madaktari hawa wanazungumza kitu kile kile lakini katika mitazamo tofauti mmoja yuko kinadharia na mwingine kivitendo zaidi.

Nawatakia Sabato yenye baraka!

Maendeleo hayana vyama!
 
Hata US kuna ombaomba na wanalala nje kwenye corridors lakini Marekani ni Taifa tajiri na lenye nguvu kubwa Duniani.
 
uchumi kukua mara 2 kati ya 2015 - 2020 kimahesabu ni sawa na kusema umekua kwa 100%!

twende taratibu na hii hesabu maana mi naona nyota nyota tu hapa.

ili uchumi ukue kwa 100% kwa miaka 5 tafsiri ya haraka ni kwamba wastani wa ukuaji uchumi wetu kwa mwaka ni 20%.

sasa hii takwimu ya waziri Mpango ya uchumi kukua kwa wastani wa 7% kwa mwaka kaitoa wapi?

au tuna serekali 2 tofauti?
Mimi siyo mchumi lakini nahisi hapa unachanganya mambo.
 
weka sawa basi...
Niwe mkweli tu kama kawaida yangu, sina maelezo yoyote mkuu sababu mimi siyo mchumi hapo nimeongea kufuata hisia tu.
Naona kama hauko sawa kuibadili kauli ya mapato/pato kuwa uchumi moja kwa moja bila kuhusisha variable zingine au vigezo vingine kama idadi ya watu n.k.
 
Huyu mtu wa propaganda Dr. Abbas hajui maana ya ku rebasing uchumi na anatumia udhaifu wa waTanzania kuwa na elimu duni, kutofahamu lugha ya Kiingereza kuongea vitu ambavyo wengi hapa JamiiForums wametumia hekima kuhoji ukuaji wa kipato na uchumi mbona hauonekani ktk hali halisi mitaani na ktk familia za wananchi wa kawaida.

Geo-economic analyst William Gumede unpacks the concept of rebasing and what the process entails. He discusses the pros and cons.
 
Ulinganifu huu ungefaa zaidi na kuleta picha sahihi, kama thamani yake kwa US $ ndio ingetumika badala ya TZS ili kutilia maanani thamani halisi ilivyokuwa ikibadilika. Sasa hivi dola moja ni tsh 2360 wakati miaka kumi iliyopita ilikuwa tsh 1500.
Na hata dola yenyewe nayo ime-depreciate.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo sahihi.
Ni sawa kalinganish pato LA kipindi cha ujima na kipindi hiki.
Na haitasaidia ,JK alishapiga misumari kuwa wanatakiwa pato liwe $3k by 2025.
Sasa badala ya kuleta mikakati wanaanz kuwa waalimu wa history.
Viazi sana hawa
 
Kwa wale ambao mapato yenu yameongezea, tuwajue humu
Screenshot_20200808-103053.jpg
 
uchumi kukua mara 2 kati ya 2015 - 2020 kimahesabu ni sawa na kusema umekua kwa 100%!

twende taratibu na hii hesabu maana mi naona nyota nyota tu hapa.

ili uchumi ukue kwa 100% kwa miaka 5 tafsiri ya haraka ni kwamba wastani wa ukuaji uchumi wetu kwa mwaka ni 20%.

sasa hii takwimu ya waziri Mpango ya uchumi kukua kwa wastani wa 7% kwa mwaka kaitoa wapi?

au tuna serekali 2 tofauti?
Matatizo ya kutoshirikisha ubongo wote.Wa nyuma kazi hii na wa mbele kazi ile! Hivi Abass aliyekula "supp" za kutosha sheria anaweza zungumzia "Uchumi" ambao mwenye Phd yake hajafikiria kudanganya licha ya kujikomba komba??? Hapo ndo taaluma zinapogeuka vituko.
 
Back
Top Bottom