Dkt. Hassan Abassi: Agizo la Rais Samia kufungulia vyombo vya habari linahusu televisheni za mitandaoni pekee

Dkt. Hassan Abassi: Agizo la Rais Samia kufungulia vyombo vya habari linahusu televisheni za mitandaoni pekee

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abassi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee na siyo pamoja na magazeti.

Amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.

---
Huyu ni kichwa ngumu bado amelala, tunaomba mama yetu umuache huyu mtu aendelee kulala, hakufai.

Amelipuuza agizo lako...anajifanya mjuaji...anakujua sana kuliko unavyojielewa...
Huyu mtu anaziamini sana tunguli na mzimu wa jiwe bado hajasoma alama s nyakati anamlisha raisi wa nchi maneno
 
Atazame big picture...mama anataka kua achieve nini. Hizo TV alitolea kama mifano kuchagiza hoja yake. Lakini kwa ujumla anataka kurejesha Uhuru wa habari ....hataki Tz ionekane inaminya uhuru wa habari.
 
Mama alisisitiza kuwa wavifungulie ili kuondoa minong'ono kuwa vyombo vya habari vinakandamizwa.

Mimi naona ameamua kwa makusudi kuzingua
Si kuzengua tu, bali na ujeuri wa kutaka ku-undermine authority ya mama Samia kiaina ili Serikali yake ionekane bado inaendelea ku-muzzle vyombo vya habari NCHINI.

Abas sio mbumbumbu kivile anapo jifanya ku-gross misinterpret kauli ya Rais S. S Hassan aliyo sema kwamba Taifa/Serikali hisi eleweke vibaya huko nje kwamba bado inaendelea inanyanyasa vyombo vya habari nchini - hapa Abbas anajifanya magazeti si vyombo vya habari!!
 
Serikali inafanya kazi kwa maandishi lazima atakuwa amepewa maelekezo kuwa ni tv za mitandaoni ndio maana kasema atawajuza kama kuna maelekezo mengine

Alichokisema rais ndicho hicho. Kila mtu alisikia hivyo. Kwa kuwa kwa kawaida serikali huendeshwa kwa maandishi au nyaraka na kwa sababu rais katika hotuba ile alitaja tu vi online tv vidogo vidogo vilivyokuwa vimefungiwa, Dr Abbas yuko sahihi. Kama rais aliimanisha na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa Dr Abbas atapaswa kwanza kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata uhakika. Halafu kwani ni magazeti yapi yalifungiwa? Si ni lile la Mbowe (Tanzania Daima), la Kubenea (Mwanahalisi) na lile la Tundu Lissu (jina nimelisahau) tu? Haya hata yakiruhusiwa wamiliki wake hawana uwezo tena wa kifedha kuyaendesha.
Kabla ya kuyafungulia unawataarifu wahusika nia yako ili kujua kama wapo tayari, maana ukiyafungulia watalazimika kulipia leseni na kodi nyinginezo, unawataarifu kujua kama wapo tayari au la.

Ila sasa,huyu Abass kwa cheo chake cha Katibu Mkuu wa Wizara ndiye anayehusika na kufunga na kufungulia magazeti? Na usemaji wa Serikali kwa sasa si ni post ya Gerson Msigwa? Sijaelewa huyu daktari ameyasema hayo kwa nafasi ipi inayompa jukwaa la kusema hayo.
 
Majamaa mengine bado yanawaza yapo enzi za kujimwambafai... Bado yanatamani zama za giza ziendelee... Roho zinawauma wanapoona minyororo yaliyotufunga inakatwa taratibu...

Bi Mkubwa anza na hizi takataka asee chaaaaaap kabla hazijaharibu asee.
 
Kabla ya kuyafungulia unawataarifu wahusika nia yako ili kujua kama wapo tayari, maana ukiyafungulia watalazimika kulipia leseni na kodi nyinginezo, unawataarifu kujua kama wapo tayari au la.

Ila sasa,huyu Abass kwa cheo chake cha Katibu Mkuu wa Wizara ndiye anayehusika na kufunga na kufungulia magazeti? Na usemaji wa Serikali kwa sasa si ni post ya Gerson Msigwa? Sijaelewa huyu daktari ameyasema hayo kwa nafasi ipi inayompa jukwaa la kusema hayo.
Kama kweli huyu Katibu Mkuu katafsiri hotuba ya Mhe. Raisi namna hii nachoweza kusema kwanza ni aibu kwa msomi kama yule kushindwa kujua lengo la maelekezo ya Mhe Rais kuhusu vyombo vya habari. Mhe. Rais hataki kusikia vyombo vya habari vilivyofungiwa, anataka uhuru wa vyombo vya habari Tanzania. Huyu hasitahiri kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa wizara hata kwa dakika moja, ni vema Rais amfukuze kazi mara moja! Nina wasiwasi, inawezekana KM huyu ana matatizo ya usikivu katika masikio yake! Haiwezekani KM akaquestion maagizo ya Rais na bado akabaki katika nafasi yake, HAIWEZEKANI!
 
Alichokisema rais ndicho hicho. Kila mtu alisikia hivyo. Kwa kuwa kwa kawaida serikali huendeshwa kwa maandishi au nyaraka na kwa sababu rais katika hotuba ile alitaja tu vi online tv vidogo vidogo vilivyokuwa vimefungiwa, Dr Abbas yuko sahihi. Kama rais aliimanisha na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa Dr Abbas atapaswa kwanza kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata uhakika. Halafu kwani ni magazeti yapi yalifungiwa? Si ni lile la Mbowe (Tanzania Daima), la Kubenea (Mwanahalisi) na lile la Tundu Lissu (jina nimelisahau) tu? Haya hata yakiruhusiwa wamiliki wake hawana uwezo tena wa kifedha kuyaendesha.
Tulia dawa ikuingie mkuu, sukuma gang kwisha habari yake, Mataga mmekuwa watoto yatima baada ya Jiwe kutaka kutawala milele ila Mungu akaingilia kati kuliponya Taifa, pole sana mkuu
 
Bila kuwa ‘mkono wa chuma’ mama yenu hataiweza nchi hii, amuulize mkwere alishindwa wapi adi leo hii tunamwona ‘failure’
Tumia umoja ndugu Mataga, ok let's say uko sahihi, Mkwere alifeli kwenye nini?
 
Kinamentality za mwenda,imesemwa msifungie vyombo vya habari hovyohovyo,sasa yanini mpendelee online TV wengine muwaache wakati wote walikosea ndipo wakafungiwa!!
Huyu MTU wakati watu wanakimbia nchi kwa kutishiwa kuuwawa alitetea,alitetea maamuzi yote mabaya ya awamu yatano!! Alipaswa akawe ata Ras huko ruvuma mpaka akili zimrudi alishazoea rohokubwa!!
 
Dkt. Abbas angalia VAR isione hayo mabega utarudisha gari shauri yako.

Umeambiwa fungulia tuanze upya wewe unaleta sarakasi.
 
Abbas ni jeuri, bora afukuzwe. Miongozo hutolewa na mkuu wa nchi kwa maslahi ya wengi(wananchi), haipaswi kupuuwa wala kupingwa na Abbas. Mama mtoe huyu anakuchafulia uongozi wako kwa manufaa ya nchiyetu

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Alichokisema rais ndicho hicho. Kila mtu alisikia hivyo. Kwa kuwa kwa kawaida serikali huendeshwa kwa maandishi au nyaraka na kwa sababu rais katika hotuba ile alitaja tu vi online tv vidogo vidogo vilivyokuwa vimefungiwa, Dr Abbas yuko sahihi. Kama rais aliimanisha na magazeti yaliyokuwa yamefungiwa Dr Abbas atapaswa kwanza kumuuliza Katibu Mkuu Kiongozi ili kupata uhakika. Halafu kwani ni magazeti yapi yalifungiwa? Si ni lile la Mbowe (Tanzania Daima), la Kubenea (Mwanahalisi) na lile la Tundu Lissu (jina nimelisahau) tu? Haya hata yakiruhusiwa wamiliki wake hawana uwezo tena wa kifedha kuyaendesha.
Mkuu, naona mpaka sasa hujaelewa vizuri modus operandi ya Mh. Rais, anatumia diplomatic language ku drive point home - mama huyu kichwa sana siwakuchukulia poa hata kidogo.

Tatizo Dk. Abbas bado amegubikwa na remnant amri za kijeshi jeshi za awamu ya tano ambapo JPM used to scare a living daylights out of Govt leaders - woga kama nini, siku moja niliwahi kumsikia akiwatisha mawaziri kwamba "mkiendelea kunisema sema ntatafuta mbinu za kuwa-rekodi halafu wanao husika ntawashukia kama mwewe" something like that - niliposikia hivyo nilishikwa na butwaa!

FYI binadamu pekee kwenye baraza la mawaziri aliye kuwa jasiri kutomwogopa au kutishwa na JPM alikuwa ni Rais wetu wa awamu ya sita Mh. Samia Suluhu Hassan - ukimzengua hana simile kweli na atanii.

Now back to the main point, sasa ndugu yetu Dk. Abbas hivi Rais aliposema kwamba Mataifa ya nje yasije kuendeleza kelele kwamba bado tunavifungia vyombo vya habari - wewe ulimwelewaje? Kwamba anazungumzia TVonline tu kwa kuwa kazitaja? Alitaja hivyo kama mfano lakini the crux of the matter here ni kuhusu uhuru wa vyombo vya hahari namely Magazeti,TVonline,social media and what have you - wakati mwingine Dk.Abbas ni vema kujiongeza si kila kitu uwe spoon fed - eti hajapata maelekezo ya kufungulia magazeti as if magazeti sio vyombo vya habari, au anaogopa kufungulia magazeti kwa kuwa wamiliki ni members wa vyama vya upinzani, ni hicho tu wala sikitu kingine kinacho mtia woga.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abassi amesema agizo la kufungulia vyombo vya habari lililotolewa na Rais Samia Suluhu linahusu televisheni za mtandaoni pekee na siyo pamoja na magazeti.

Amesema endapo kukiwa na maagizo mengine yanayohusu magazeti, atatekeleza.

---
Huyu ni kichwa ngumu bado amelala, tunaomba mama yetu umuache huyu mtu aendelee kulala, hakufai.

Amelipuuza agizo lako...anajifanya mjuaji...anakujua sana kuliko unavyojielewa...
Neno Uhuru wa Habari Dr Abbas limemchenga na hawezi kuwa MTU sahihi hapo alipo,anamharibia Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza maagizo yake apendavyo yeye!
Hivi tuapoongelea vyombo vya habari Dr anadhani ni TV pekee?Yaani Mh.Rais aanze kumfundisha Dr Abbas majukumu yake?Atoe ufafanuzi kuhusu magazeti,majarida,Radio's ama Online TV separately?
 
Back
Top Bottom