Dkt. Hussein Mwinyi adai Mzee Mwinyi hakuagiza azikwe Mkuranga

Dkt. Hussein Mwinyi adai Mzee Mwinyi hakuagiza azikwe Mkuranga

Mzee mwinyi kuzikwa zanzabar ipo kisiasa zaidi
Una uhuru wa kusema hivyo, lakini hilo halifanyi unalosema kuwa kweli.

Masuala ya nia, kitu cha ndani kabisa katika fikra za mtu, ni magumu sana kwa mtu mwingine kuyajua.

Wewe unaweza kurahisisha mambo hayo kwa sababu hujaishi maisha yake, hujajua ana connection gani na Zanzibar.

Familia ya Mwinyi imeamua kuhamia Zanzibar. Kuna mtoto wa pili wa Ali Hassan Mwinyi anaitwa Hassan hakuwa mwanasiasa, alifariki mwaka 2022. Alizikwa Zanzibar.

Huyo naye utasema kazikwa Zanzibar kisiasa?

Hawa wakina Mwinyi hata wakija kuzikwa Mkuranga nako kuna kitu kitakuzuia kusema wanazikwa Mkuranga kisiasa kwa sababu wanataka urais wa bara?

Ukitaka Mwinyi azikwe wapi ili usione kazikwa kisiasa? Cairo Misri?

Na huyu Hassan baba yake kazikwa hapo hapo, pembeni ya kaburi la mtoto wake wa pili.

Sasa Mzee Ali Hassan Mwinyi akikwambia anataka kuzikwa Zanzibar walipohamia, alipoanzia elimu na maisha, alipianzia siasa, alipoolea na kupata familia, ambapo mtoto wake kazikwa, na ndugu zake wengine watazikwa, utataka kumnyanyapaa kwamba kaamua kuzikwa hapo kisiasa?

Mbona mnamkosea heshima sana huyu Mzee wakati yeye alikuwa mtu mstaarabu sana kwenye ku deal na watu?
 
Back
Top Bottom