Una uhuru wa kusema hivyo, lakini hilo halifanyi unalosema kuwa kweli.
Masuala ya nia, kitu cha ndani kabisa katika fikra za mtu, ni magumu sana kwa mtu mwingine kuyajua.
Wewe unaweza kurahisisha mambo hayo kwa sababu hujaishi maisha yake, hujajua ana connection gani na Zanzibar.
Familia ya Mwinyi imeamua kuhamia Zanzibar. Kuna mtoto wa pili wa Ali Hassan Mwinyi anaitwa Hassan hakuwa mwanadiasa, alifariki mwaka 2022. Alizikwa Zanzibar.
Huyo naye utasema kazijwa Zanzibar kisiasa?
Hawa wakina Mwinyi hata wakija kuzikwa Mkuranga nako kuna kitu kitakuzuia kusema wanazikwa Mkuranga kisiasa kwa sababu wanataka urais wa bara?
Ukitaka Mwinyi azikwe wapi iki usione kazikwa kisiasa? Cairo Misri?
Na huyu Hassan baba yake kazikwa hapo hapo, pembeni ya kaburi la mtoto wake wa pili aliyeitwa Hassan.
Sasa Mzee Ali Hassan Mwinyi akikwambia anataka kuzikwa Zanzibar walipohamia, alipoanzia elimu na maisha, alipianzia siasa, alipoolea na kuoata familia, ambapo mtoto wake kazikwa, na ndugu zake wengine watazikwa, utataka kumnyanyapaa kwamba kaamua kuzikwa hapo kisiasa?
Mbona mnamkosea heshima sana huyu Mzee wakati yeye alikuwa mtu mstaarabu sana kwenye ku deal na watu?