Dkt. Hussein Mwinyi adai Mzee Mwinyi hakuagiza azikwe Mkuranga

Dada yangu wa kajunjumele,punguza uhana harakati,Mambo ya mwinyi hayo ni ya familia yake,wao ndo wana wosia wa mzee wao,pambana na ya kwako
 
Asicheze na watu mitandaoni. Watamtoa kwenye reli

Uki sawa sana.

Kuna binti mmoja wa Mwinyi nilisoma naye, huyo sijawahi kumuona kokote kwenye mtandao wa kijamii.

Mwanzo nilifikiri labda ni nyodo.

Lakini, nikakumbuka shule yule binti hakuwa na nyodo kabisa alikuwa mtu very humble.

Nikaja kuambiwa kwamba amekataa kuwa kwenye mitandao kwa kuepuka maneno ya watu.

Nikiangalia familia yao inavyoshambuliwa hapa, naweza kuelewa kabisa kwa nini ameamua kuishi hivyo.
 
Pia katika sentensi hiyo hakuna Mzee aliposema akifia Zanzibar basi azikwe hukohuko

Na wala huyo Mwinyi katu hawezi kusema Tulipewa wasia na Baba Tukamzike Mkuranga lakini tumeamua tumzike Zanzibar kwa sababu za kisiasa 😛😛😛
 
Mkuu hili liache tu tukichunguza sana itakuwa hatari

la kuchunguzwa ni hili


• Mke wa Mwl, Julius K. Nyerere, Maria Nyerere.
• Wake wa Ali H. Mwinyi, Sitti na Khadija Mwinyi.
• Mke wa Benjamin W. Mkapa, Anna Mkapa
• Mke wa Jakaya M. Kikwete, Salma Kikwete
• Mke wa John P. Magufuli, Janeth Magufuli
• Mume wa Samia S. Hassan, Hafidh Ameir

Kwa mujibu wa The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225] kila mwezi hawa watalipwa 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani.

Kama Rais aliyepo madarakani anapokea TZS 50,000,000 kwa mwezi, mwenza wa Rais atalipwa malipo/mafao ya TZS 30,000,000 kila mwezi.

Rais akistaafu, mwenza/wenza wake atapokea/watapokea (kwa mkupuo) 25% ya mshahara wa Rais alioupokea wakati wote akiwa madarakani.

Mfano, kama Rais alikaa madarakani kwa kipindi cha miaka 10, akalipwa TZS 4,000,000,000, mwenza wake atalipwa TZS 1,000,000,000 kwa mkupuo.

Pamoja na malipo hayo ya fedha, pia wenza hawa sita (6) wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapata mafao mengine kama ilivyoelekezwa;

1. Nyumba ambayo Rais alipewa na alikuwa akiitumia kama makazi baada ya kustaafu itakuwa mali yake halali baada ya mume/mke wake (Rais) kufariki.

2. Atapokea posho ya matengenezo ya kila mwezi katika maisha yake yote akiwa hai kiasi ambacho ni sawa na 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani.

3. Mke/mume wa Rais atatibiwa ndani na nje ya Tanzania, na matibabu yake yatagharamiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

4. Mjane wa Rais mstaafu atapata huduma ya magari mawili, na dereva wawili kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali inalipia gharama za mafuta.

5. Magari anayopewa mjane wa Rais yatabadilishwa baada ya miaka 5. Kuna maintenance allowance. 60% ya mshahara wa Rais aliye madarakani kila mwezi

6. Malipo ya fedha kulipa mishahara kwa kiwango cha kima cha chini cha mishahara ya watumishi kwa; dereva, mpishi, mfua nguo na mtunza bustani

7. Mke/mume wa Rais atapata huduma ya usafiri kwa gharama za serikali hadi mahali pa kuishi kwa maisha yake yote hadi pale ambapo kifo kitawatenganisha.

8. Mke/mume na watoto wanapata ulinzi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Usalama wa Taifa.

9. Gharama za mazishi ya mke/mume wa Rais yatakuwa chini ya serikali. Serikali ya Tanzania itagharamia kwa 100% msiba wa mwenza wa Rais

10. Mjane wa Makamu wa Rais, anapata stahiki kama za mjane wa Rais isipokuwa tofauti yake ni moja, atapata gari moja la Serikali na dereva mmoja.

Martin Maranja Masese, MMM.
 
Hata rais Mwinyi angesema yeye mwanamazingira hataki kuharibu ardhi anataka kuzikwa baharini, akakubaliana na famikia yake, ni sawa tu, ni maamuzi yake na familia yake.

Kwa nini tunaona ni sawa kuiingilia familia ya watu kwenye uamuzi wa kumzika baba yao?

Yani sisi wananchi tunaodai uhuru, tunaodai katiba mpya, tunainyima familia ya Mwinyi uhuru wa kumzika baba yao inavyotaka, bila kusengenywa?

Hivi, tukianza kupangia familia za watu wengine pa kuzika, hata huo uhuru wenyewe tutakuwa tunauelewa kweli?
 
Acha uwongo- Hussein mwinyi ana miaka 57 sasa. Akiwa na miaka minne ni 1970, nchi gani hiyo unayosema ilikuwa haijapata uhuru 1970?
 
Wazazi wake wamezaliwa wapi?
Wazazi wake wamezikwa wapi?
Na yeye Mwinyi amezaliwa wapi?
Mtu kupelekwa mahali nje ya nyumbani iwe ndani nchini au nje ya nchi kwa ajili ya masomo na kutafuta maisha, hata akae muda gani, haihalalishi kuwa ndio nyumbani kweao!
 
Mwinyi namkubali sana!hasa ukimya wake na kufikiri Cha kusema!!
Angeendelea kukaa kimya!kwani lazima ujibu!!?unaamsha popo lazima watakunyea tu!!

Kwanini asijifunze Kwa dada yake!!?
Gazeti la uhuru lilimtoa relini baada ya kujibu vile!Hadi Leo anasaidiwa kampeni akishindana na hewa coz hakuna aliechukua fomu Wala kumpinga!!

Jifunze wakati wa jk awamu ya nne,rafiki take alipoanza harakati alikaa kimya na yeye akafanya kimya kimya uwaziri mkuu ukaota mbawa!!

Kimya kimya ndio mpango mzima!
 

Uko sahihi.
Mwinyi hajawahi kuomba uraia wa nchi ya Jamhuri ya Tanganyika
Sheria ya mapinduzi ya Zanzibar inasema kuwa yeyote aliyekuweko Zanzibar siku ya mapinduzi anaqualify kuwa mzanzibari
 
Punguza emotions zako. Unalalamika nini mtu aliyekuwa mwanasiasa kufikiriwa kisiasa? siasa haifi kwenye misiba, Mwinyi atazungumzwa tu popote pale.

By the way, nani aliyekwambia Mzee Mwinyi anasemwa kwa ubaya? hebu wacha hisia zako potofu.

Kama sisi tusiofahamika na yeyote huko nje misiba yetu huwa haikosi maneno, ndio itakuwa msiba wa Mzee Mwinyi - Rais mstaafu?!

Nakwambia tena ondoa emotions zako kwenye hili jambo, wacha bongo za watu zifanye kazi yake.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…