Kujamba unajamba wewe, halafu unamlazimisha Mwinyi athibitishe hajajamba yeye.
Unamlazimisha mtu aweke wosia wa baba yake, kitu ambacho kashakuambia ni private matter ya ndani ya familia yao, hadharani?
Kwa sababu tu wewe umetunga uongo kuhusu huo wosia?
Nakwambia hivi, nyie Watanzania wa hivi hawa watawala watawaburuza sana.
Kwa sababu mnajichanganya sana.
Huku mnataka uhuru, mnataka katiba mpya.
Huku mnashindwa hata kuelewa uhuru ni nini, mnashindwa kuiachia familia ya Mwinyi kumzika mzee wao kwa uhuru.
Hapo ndipo mnawapa hawa watawala msemo kwamba hamuelewi uhuru ni nini.
Kwa mwendo huu, I can guarantee you hiyo katiba mpya mtaisikia redioni tu.
Yani nyie watu msioelewa basic human right of dying and being buried with dignity ndio nyie nyie mnadai katiba mpya pia?
Tanzania ni nchi yetu na tunaipenda sana sana
Watu tumeishi ulaya lakini nyumbani ni nyumbani tu.Hapa JF kuna watu wengi nimeishi nao ufaransa wao wakiwa watu wazima na bado wapo huko lakini wanakuambia watarudi nyumbani na wataishi hapa Tanzania
Wahindi ni matajiri sana na wana majumba canada lakini wanaipenda Tanzania na tunaishi nao hapa
Hakuna anayeburuzwa Tanzania wala kubaguliwa hapa Tanzania kama nje,Ulaya ndio kuna kuburuzwa vibaya sana ,Kuna sheria kali ambazo ukiweka hapa Tanzania hakuna atakayezifuata kwani zinaondoa uhuru wa watu
Huko ulaya watu wanabaguliwa sana sijawahi kuona kwenye maisha yangu
Mimi niliyeishi ufaransa nikiwa mtoto wa college huwezi nirudisha kuishi ufaransa,Unabaguliwa kuanzia darasani mpaka kwenye kupanga apartment tu ilikuwa shida kisa rangi yangu watu wakiona black sipangishi mpaka nawatumia baadhi wazungu wastaarabu
Marekani kwenyewe ambako nimeenda nikiwa mtu mzima kwenye mambo ya kamati za bunge ni hovyo kabisa,Na ni nchi yenye watu weusi kibao zaidi ya ufaransa lakini unakuta jitu jeusi tii kama mkaa bado linakubagua mtu toka Afrika ambao kwa Tanzania sisi wengi sio weusi sana kama wasudan
Kuna kumbi za muziki wakati huo unafika mlangoni ufaransa ,Unakuta mzungu mlangoni anatukatalia watu black
Upweke uliopo ulaya na hata Marekani ndio maana watu wengi wakirudi wanaonekana kama vichaa kichwani
Bora kuendelea kuburuzwa nyumbani lakini sio kuwa mtumwa kwenye Taifa la watu ambalo hata haki ya kuongoza nakosa
Kama ulienda ulaya ukiwa mtu mzima kutafuta maisha najua utakuwa unayavumilia niliyoyaishi mimi miaka hiyo
Hapa Tanzania tuna sheria lakini hazibagui sana wageni isipokuwa kwenye mambo ya ardhi na uongozi wa kisiasa,Huko kuna sheria mpaka za kumlinda paka na mbwa na wengine mpaka kugeuza mbwa na paka kuwa wapenzi wao kimahaba
Kwa sasa najua huko ufaransa sijaenda kitambo nadhani kutakuwa na ndoa za Paka kuolewa na binadamu au Mbwa kufunga ndoa na binadamu