Zanzibar 2020 Dkt. Hussein Mwinyi ashinda kiti cha Urais Zanzibar kwa asilimia 76.27

Zanzibar 2020 Dkt. Hussein Mwinyi ashinda kiti cha Urais Zanzibar kwa asilimia 76.27

Hongera sana Hussein Mwinyi kwa kushinda kwa kishindo, ni wakati sasa wa kuinua maendeleo ya Zanzibar. Wazanzibari waache kulialia waendelezi visiwa hivi kwa nguvu zote na bara tupo kuwasaidia kama wanakwama.

Kero zote/nyingi za Muungano zimetatuliwa sasa lazima muwe kitu kimoja tumia nafasi yako kuleta maendeleo kama unakwama JPM yupo kukusaidia.
 
Mambo yanayoendelea Zanzibar CCM wanayafurahia sasa hivi ila ndio tunaenda kuzika sekta ya utalii nchini kwetu kwa upumbavu wa watu wachache
 
Hongera sana hussein mwinyi, wazanzibar wapo pamoja nawe, kuwaletea maendeleo ya kweli.
 
Haijawahi kutokea mgombea urais wa Zanzibar kupata asilimia hizo kubwa katika mfumo wa vyama vingi. Ngoja nirudie kusoma makabrasha ya tangu 1995 kuhusu siasa za Zanzibar

2010
Huko Visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein wa chama cha mapinduzi CCM alishinda kwa asilia mia 50.1 ya kura dhidi ya mpinzani wake Seif Sharrif Hamad wa chama cha upinzani CUF aliyefanikiwa kupata asilia mia 49.1 ya kura.

Maafisa wa tume ya uchaguzi wanatarajiwa kutoa matokeo zaidi hii leo. Katika matokeo yaliyotangazwa hadi katika maeneo bunge 10, kutoka 239, Kikwete anaongoza kwa asilia mia 66.94 ya kura ilhali Slaa amepata asilia mia 17.36.

2005
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibaŕ ilitangaza kwamba mgombea wa uŕais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amani Kaŕume, alipata asilimia 53.2 ya kuŕa wakati mpinzani wake mkuu Chama Cha Wananchi (CUF), Seif Shaŕif Hamad, alipata asilimia 46.1.
 
Maalim Seif kugombea nafasi hiyo. Historia ya kugombea kwake urais wa Zanzibar ni kama ifuatavyo:

  • Aligombea mwaka 1995 katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi dhidi ya mgombea wa CCM Dkt Salmin Amour, alieshinda kwa asilimia 50.2 ilhali Maalim Seif alipata asilimia 49.8
  • Akagombea tena mwaka 2000 akichuana na mgombea wa CCM Amani Karume aliyeshinda kwa asilimia 67.04 huku Maalim Seif akipata asilimia 32.96
    Dr salmin amour katika ubora wake - YouTube
  • Alijaribu tena bahati yake mwaka 2005 dhidi ya mgombea wa CCM Amani Karume aliyeshinda kwa asilimia 53.2 huku Maalim Seif akifuatia kwa karibu kwa asilimia 46.1
    35th General Conference: Visit of Mr Amani Abeid Karume, President ...
  • Katika uchaguzi wa mwaka 2010 Maalim Seif alianguka tena akipata asilimia 49.14 huku mgombea wa CCM Ali Mohammed Shein ashinda kwa asilimia 50.11
    Dr Ali Mohamed Shein - Alumni and Supporters - Newcastle University
  • Na uchaguzi mkuu wa mwisho kabla ya huu wa mwaka huu ulifanyika mwaka 2015 ambapo katika kinachoweza kutafsiriwa kuwa hujuma za waziwazi dhidi ya Maalim Seif, Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar ilifuta matokeo ya uchaguzi, na kuamuru urudiwe ambapo Maalim Seif alisusa, na Dkt Shein akatangazwa mshindi kwa asilimia 91.4 matokeo ambayo hadi leo Maalim Seif hayatambui.
Danni Mzena on Twitter: KATUNI POLITIKS 3 @seifkabelele @bmachumu ...
Hata hivyo, uamuzi wa Maalim Seif kutangaza kuwania tena urais kwa mara ya sita mfululizo kumezua maswali ambapo baadhi ya watu wanadhani ingekuwa mwafaka apishe wanasiasa wengine kuwania nafasi hiyo, hasa kwa vile amekuwa akishindwa chaguzi zote alizoshiriki.
Source : Urais Zanzibar: Kwa Kurejea Hujuma Dhidi Yake 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, Maalim Seif Ana Haki Kugombea Tena Kwa Mara ya Sita
 
Hii ni nchi huru,
Jidanganyeni hivyo hivyo wakati moto unakuja.
Hii ni dunia jomba! Kuna kanuni za pamoja lazima zifuatwe ndio maana kina Gabgo walijikuta The Hague. Au unadhani nchi zao sio huru? Wapi Albashiri? Wako wapi kina Taylor?
 
Jidanganyeni hivyo hivyo wakati moto unakuja.
Hii ni dunia jomba! Kuna kanuni za pamoja lazima zifuatwe ndio maana kina Gabgo walijikuta The Hague. Au unadhani nchi zao sio huru? Wapi Albashiri? Wako wapi kina Taylor?
Maneno ya mkosaji
 
Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
😁😂😀😅😄😄
Akaulinde Huo Muungano
Unafki Ccm Wanauweza Yaani!!
Tunangoja Wajukuu Nao Watawale Zanzibar
 
Hakuna uchaguzi wowote ambapo CCM itaiachia Zanzibar as long as muundo wa ZEC na NEC unaendelea kuwa hivi. Piga, vunja miguu, funga, mwaga damu etc: CCM lazima itawale kule.

Upinzani unapaswa kujipanga upya na kuplan kuanza maisha baada ya Seif. Huku Bara nako kuna haja ya kujiangalia upya. Akina Lipumba, Mbowe na wenzao wanapaswa kujitafakari kama wanatosha kuendelea kuongoza haya mapambano
 
Back
Top Bottom