Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

View attachment 2911327
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Disemba 2014, Dkt. James Mataragio aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC

August 2016 alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC

Julai 2019 Rais Magufuli Aliagiza arejeshwe kazini

Aprili 4 2021 alitolewa TPDC nafasi ikachukuliwa na Thobias Mwesiga.

Aprili 5 2021 aliteuliwa tena kuwa Mkurugenzi TPDC.

Februari 2023 alitolewa TPDC nafasi yake ikachukuliwa na Mohamed Makame na taarifa ilisema atapangiwa kazi nyingine.

Februari 2024 ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Wizara ya Nishati.
Aliwakosea nini ikulu?
 
Huyu mzee atupeleke alipozika kizizi maana wanamuondoa anakaa kidogo wao wenyewe wanamrudisha. Sometimes shule inalipa na ukiwa smart kwamukichwa.
 
Yaan mi nikajua anafukuzwa kabsa kumbe anatolewa kwenye ugali anapelekwa kwenye mboga... Anyway I love my country
Dr. Mataragio ame"survive" TPDC kwa bahati, kwa vile alipoenda pale waliyokuwepo walimwekea chuki, kwa nini atoke mtu nje wakati wao wapo. Hii ilifanya asukiwe kesi, alipopona na kurudishwa alioondolewa na mama kwa siku mbili na nafasi yake akapewa kada wa CCM alieduma siku moja kazini na Mataragio kurudishwa tea. Baadaye aliondolewa na mama na kua,biwa atapangiwa kazi ngingine. Nchi yetu ina pesa za kupoteza Kum,buka safari zote huyu bwana amekaa kando alikuwa analipwa au alilipwa mshahara. Sasa amerudi tena, hopefully atastaafia hapo.
 
Huyu mzee atupeleke alipozika kizizi maana wanamuondoa anakaa kidogo wao wenyewe wanamrudisha. Sometimes shule inalipa na ukiwa smart kwamukichwa.
Uliwahi kuusikia msemo "una bahati kama mtende"? Huyu Bwana ni Mtende (Watende kwa kawaida ni watu wa Mara yakijumuishwa makabila ya Wakurya, Waikizu, Wazanaki, Wangoreme, Wanatta, Waisenye, Waikoma....) Basi hii ndiyo aliyonayo bahati huyu Mtende (Mongoreme).
 
Back
Top Bottom