Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

View attachment 2911327
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Disemba 2014, Dkt. James Mataragio aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC

August 2016 alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC

Julai 2019 Rais Magufuli Aliagiza arejeshwe kazini

Aprili 4 2021 alitolewa TPDC nafasi ikachukuliwa na Thobias Mwesiga.

Aprili 5 2021 aliteuliwa tena kuwa Mkurugenzi TPDC.

Februari 2023 alitolewa TPDC nafasi yake ikachukuliwa na Mohamed Makame na taarifa ilisema atapangiwa kazi nyingine.

Februari 2024 ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Wizara ya Nishati.
Jamaa yupo kwenye mfumo hatoki ni vijana wa Msoga na Rostam
 
Mwingine nani acheni utetezi wa kijinga enzi zile za mkono wa Chuma TANESCO walikua tumbo joto hawakua wakikata umeme hata KIDOGO hadi tukasahau suala la umeme kukatika yaan hawa wanahitaji mtu mwenye karba hio mtu wa kuwaendesha kibabe kibabe tu undava undava ukizingua unapigwa chini ndio wananyooka ukiondoa wa kwanza akiingia mwingine akazingua ukimuondoa akiingia mwingine akazingua ukimuondoa kuna mmoja ukimweka lazima atagundua wapi kuna tobo na kuliziba mara moja Ila hawa wahuni wame-relax kuna tobo alafu wame-relax tu hawalizibi sababu wanajua hawana mtu wa kuwatia tumbo joto
Kalemani aliwaweza sn hawa wajinga
 
Back
Top Bottom