Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Naona mwamba karudi tena kitini baada ya kuharibiwa CV yake na wapika majungu wa CCM, JK alimtoa USA huyu jamaa akamleta TPDC kabla ya kuzinguliwa na JPM kisa mshahara wa 35m.

Tanesco ni fupa gumu sana linahitaji uchizi kudeal nalo, ukileta theory linakuaibisha mchana kweupe.
Mbona alikuwa TPDC hadi Samia mwenyewe ndio akamuondoa?
 
Ina maana Biteko hamuoni kama kapwaya?
CCM na serikali yake hakuna aliye nafuu. Ni total system collapse! Huwezi kujua ni yupi nafuu au ni yupi mbaya. Haya ni matokeo ya chama kimoja kukaa madarakani kwa muda mrefu na kujisahau. Hii ni kama kanuni ya asili na tusitegemee tena kuwa CCM itakuja kuwa afadhali bali itaendelea kuwa mbovu. The only way is to neutralize it.
 
Wizara imejaa watu wajinga zaidi kwenye shirika la umeme Tanesco .
.Wataalamu wengi ni kunguru hata fikra zao ni za kizamani sana, shirika lipo na Wahandisi zaidi ya 300 lakini bado wanalipatia hasara Kwa mgao sugu wa umeme , Mh Raisi hapa amekosa mshauri Sahihi.
 
Mtaalamu wa kimataifa karudi mara ya tatu.

Toka maktaba :

RAIS AMTEUA Dkt. James P. Mataragio kuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC
MICHUZI BLOG AT THURSDAY, DECEMBER 18, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-

ELIMU:-
· Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
· PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
· MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
· BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WA KAZI:-
· Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
· 2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
· 2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
· 1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
· 1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014
 
View attachment 2911327
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Huyo kwa elimu yake kutegemea ajira za ccm atakua popoma...heri arudi zake nje kufanya kazi,level yake sio kua naibu katibu mkuu.
 
View attachment 2911327
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Yaan mi nikajua anafukuzwa kabsa kumbe anatolewa kwenye ugali anapelekwa kwenye mboga... Anyway I love my country
 
Daaaah kwake KIZIMKAZI anaona kafanya bonge moja la KAZI.
Akuna
1.Maji Kwa DAR
2.Sukari
3.Umeme.

Anacho weza yy pale magogoni ndio icho tu.

Kutengua na kuteua
Na Bado hatujasema n mpaka dj suluhu aamue mwenyew kuzima mziki Atupumzishe kdg Wana daslam
 
Ina maana Biteko hamuoni kama kapwaya?
Hamuoni yeye anaona kukwatwa umeme fresh TU yaan TANESCO wakikata umeme wiki 1 mfululizo asubuhi mchana na usiku bila kuwasha mwanga km wanavyofanyaga DAWASA kukata maji hata wiki 3 mpaka Mwezi watu wanaishi bila maji hapo ndio wataelewa watanzania ni watu wa aina gani, tutaenda kuwachomoa kwenye Ofisi zao mmoja mmoja
 
Wasira aeanza kua mkuu wa mkoa wa Mara mwaka 1971, leo ni miaka 53 bado ni mtumishi wa umma.
This government n Kam inamfumo wa kinship watu wanazungula humo miaka nenda rud mpaka wafe then relatives zao ndio waje washke usukan Tena so nimulemule until death do them apart
 
View attachment 2911327
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine

Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Huyu mzee alipaswa afanye kazi za taaluma yake...
 
Yaan mi nikajua anafukuzwa kabsa kumbe anatolewa kwenye ugali anapelekwa kwenye mboga... Anyway I love my country

Alitolewa ukurugenzi TPDC akawekwa pembeni kupangiwa kazi nyingine miezi kadhaa iliyopita...
 
Huyu Seleman Mbutuka anatoewa kafara tu. Siyo yeye anayeleta mgawo wa umeme.

Ili umeme uwake masaa 24 siku 7 za wiki mwaka mzima, ccm lazima iondoke. Samia mwenyewe aondoke
 
Back
Top Bottom