Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Dkt. James Mataragio ateuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati

Wasira aeanza kua mkuu wa mkoa wa Mara mwaka 1971, leo ni miaka 53 bado ni mtumishi wa umma.
"Mwalimu akang,,
Anastahili kustaafu bwana tangu nimemsikia mimi nikiwa kijana mpaka nimezeeka jamaa yumo tu! Mh. Rais sasa ni zamu yangu uniteue sasa na mimi nile mema ya nchi hapo kwa muda mfupi!
Unashangaa ya Dr. Mteuliwa, ukiyasikia ya Mzee wa Makoti waweza kuzimia!
 
Naona mwamba karudi tena kitini baada ya kuharibiwa CV yake na wapika majungu wa CCM, JK alimtoa USA huyu jamaa akamleta TPDC kabla ya kuzinguliwa na JPM kisa mshahara wa 35m.

Tanesco ni fupa gumu sana linahitaji uchizi kudeal nalo, ukileta theory linakuaibisha mchana kweupe.
Huyu alikuwa kichwa cha Bell Geospace.

Tanzania tungeheshimu na kuthamini taaluma na uweledi wa watu wetu na kuwatumia sio kisiasa, tungepiga hatua sana.
 
Huo ndo ukweli. Mataragio alitumbuliwa miezi michhe tu baada ya JPM kuingia madarakani. Baadae nadhani JPM akafahamu kwamba yalikuwa majungu tu ndipo akamrudisha tena TPDC
Uzuriwa magufuri akigundua umeonewa anakurudisha Tena kwa lazima
 
Daaaah kwake KIZIMKAZI anaona kafanya bonge moja la KAZI.
Akuna
1.Maji Kwa DAR
2.Sukari
3.Umeme.

Anacho weza yy pale magogoni ndio icho tu.

Kutengua na kuteua
Kwanj asimfukuze wazir wa kilimo na wiwanda kwa kushindwa kufanya kazi yao ipasayo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mtaalamu wa kimataifa karudi mara ya tatu.

Toka maktaba :

RAIS AMTEUA Dkt. James P. Mataragio kuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC
MICHUZI BLOG AT THURSDAY, DECEMBER 18, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-

ELIMU:-
· Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)
· PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)
· MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)
· BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WA KAZI:-
· Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA
· 2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu
· 2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
· 1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)
· 1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.

Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
18 Desemba, 2014
Huyu ni mmoja wa wasukuma wasomi snaa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mtu anashindwa hapa anapelekwa pale hivi hii serikali hakuna watu wengine wa kufanya hizo kazi?
 
Back
Top Bottom