Dkt. Janabi na Wanaharakati wa Afya tuache upotoshaji. Nchi ina tatizo kubwa la Utapiamlo na sio uzito wala unene

Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.

Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.

Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.

Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.

Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU

Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.
LEO UMEONGEA POINT SANA. JANABI AMESHAKUWA MSANII NA ANATAKA MU TREND KAMA AKINA MWIJAKI TU. SIKU HIZI NIMEONA HANA JIPYA. ANAACHA MATATIZO YA MSINGI ANASHIKILIA VITU AMBAVYO SI MATATIZO KWA TAIFA.
 
Janab inaelekea huwa anatibu familia za madon maana inaelekea hana habari na kinachoendelea kwenye familia nyingi za kiswahili.

Kiukweli kuna familia nyingi sana hapa zinapata mlo mmoja kwa siku. lakini kama unaishi ushuani mboga 7 huwezi kujua.

Kuna wachache waliojipata kimaisha wanakula ovoovo. Unakuta mtu boonge lakini bado anafakamia mabia na misosi yenye mafuta tele.
 
Mchawi huyu dokta uchwara, usimuone na koti lake lile la maigizo, he is a manipulative liar, a propagandist and a pawn of the powers that be.

Sauti yake ni ya maigizo. Hasemi ukweli.

Anarembua rembua tu na kutupiga fix za hapa na pale. A WITCH IN HOSPITAL UNIFORMS.
Komwe kama komwe! 😂
 
Inasikitisha sana.

1. Ili ule vizuri, huhitaji kuwa na fedha nyingi ama ukwasi.

2. Unahitaji ule vyakula vya makundi yote vitamin, protin, mafuta na wanga (hapa sukari hamna, maana utaipata kwenye matunda)

3. Mboga za majani ikiwemo karoti ni moja ya vyanzo vikuu vya vitamini.

4. Mtanzania yupo tayari kupanda maua badala ya kuotesha mboga za majani.

5. Watanzia wengi wanakula kushiba na siyo kupata afya.

6. Watu wanaliogopa hata jua la saa mbili; utasikia "huoni jua wewe". Jua la asubuhi hadi saa nne lina vitamin D.

7. Mbeya na Iringa zinaongoza kwa utapiamlo japo ni miongoni mwa mikoa inayozalisha vyakula kwa wingi.

8. Watu hawapendi mazoezi wala kazi ngumu.

Kwa hiyo, utapiamlo hauna uhusiano na kipato kidogo bali uwezo mdogo wa kufikiri
 
Leo ninaandika nikiwa na hasira zilizochanganyikana na huzuni kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na huyu daktari pamoja na madaktari wengine uchwara wanaolazimisha ionekane kuwa nchi ipo kwenye tatizo kubwa la unene uliopitiliza wakati ni kinyume chake.

Tumekuwa tukiwasikia msile wanga mara usikun kuleni tu matunda na maji mengi wakati wananchi wengi wanakula tu ili kuzuia msiba na sio kuzingatia mlo kamili kwasababu ya umaskini.

Hizo nguvu mnazotumia kwa ajili ya kikundi cha watu wachache mngetumia kuonyesha ukubwa wa tatizo la lishe kwa wananchi mngepata thawabu. Dr Janabi huna tofauti na mke wa mfalme wa Ufaransa aliyesema watu kama hawana mikate wale keki.

Kwa mujibu wa mtandao wa STATISTA hadi kufikia November 2021 kulikuwa na 31.8% ya watoto wa chini ya miaka miatno wenye utapiamlo uliokithiri (Chronic Malnutrition). Ni 4% tu ya watoto huzaliwa wakiwa overweight.

Kimsingi hivyo vyakula anavyosema Janabi watu wasile ni ndoto za watanzania wengi kuvipata angalau mara moja kwa siku. Mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo la lishe. Ninachoona ni ndugu Janabi kudhani maisha anayoishi yeye ndo wanayoishi watanzania wote. ASIJISAHAU

Ninatoa wito kwa serikali za mitaa kupambana ili mashuleni watoto wawe wanapata chakula. Wale wazazi/ walezi wapumbavu wanaokataa kuchangia vyakula kwa kisingizio cha ELIMU BURE wakamatwe watupwe tu ndani maana wanaturudisha nyuma. Haihitaji utafiti kujua kama kuna tatizo kubwa la lishe karibu maeneo yote nchini.
Nini maana ya unene??

Usije kuwa unatumia macho Yako kufanya hitimisho wa kuwa huyu mnene na huyo si mnene.

All in all datari yupo sawa 100%

Kwa sasa Kuna changamoto kubwa ya magonjwa ya mfumo wa maisha na tatizo kubwa ni vyakula vya wanga (processed carbohydrates), sukari, mafuta, chumvi nyingi, pamoja na kutofanya mazoezi /kazi zinazoshabihana na mazoezi.

Tunavyozungumzia unene lazima ipimwe BMI na watu wengi Wana uzito mkubwa japo wenyewe wanaona ni kawaida tu na mayokeo yake ndio magonjwa kama kisukari, presha, moyo, kufeli figo, upungufu wa ngubu za kiume nk

Hivi ushangai kukuta vijana wengi chini ya miaka 35 kuboost nguvu za kiume?? Shida ni ulaji tu
 
Hata kwa macho tu ukiangalia utagundua watanzania wengi wamedumaa kwa kukosa mlo kamili na kwasasa ndo kabisaa familia nyingi ni milo miwili kwa siku.

Sema asilimia kubwa ya waTz hawana uzalendo ndo maana sishangai kuona upotoshaji ukishamiri hasa kipindi hiki.
Shida siyo kula milo miwili

Hata ukila mara 5 Kwa siku, Kwa ulaji wetu wa vyakula vya sukari, wanga na mafuta/fat nyingi ni sio lishe

Halafu mwili wako unahitaji chakula kidogo sana tofauti na unavyojua.

Mwili hauhitaji tule kama tunavyokula ni mazoea tu ya hovyo

Halafu pia unaweza kula vizuri Kwa pesa ndogo tu
 
Janabi anadhani nchi yote ni Dasilamu.

Another professorial rubbish, nonsense.
Tanzania nzima mfumo wa ulaji ndio ule ule tu

Wanga /sukari na mafuta Kwa wingi; vyakula ambavyo ni hatari kwa afya
 
Janab inaelekea huwa anatibu familia za madon maana inaelekea hana habari na kinachoendelea kwenye familia nyingi za kiswahili.

Kiukweli kuna familia nyingi sana hapa zinapata mlo mmoja kwa siku. lakini kama unaishi ushuani mboga 7 huwezi kujua.

Kuna wachache waliojipata kimaisha wanakula ovoovo. Unakuta mtu boonge lakini bado anafakamia mabia na misosi yenye mafuta tele.
Tatizo la wabongo,

Ushajiuliza Kwa nini zamani magonjwa kama ya kisukari na presha walikuwa wanaumwa matajiri ila sasa maskini wengi wanaumwa?

Lishe yetu ni mbovu, watu wengi wanakula milo mitatu ila vyakula vya hovyo

Sukari sana/chumvi sana/ wanga sana/ mafuta sana
 
Tatizo linaanzia pale mbuzi nyeusi zinakwambia zinajifanya zinaenda kiasili na huku zikifakamia matakataka yenye mifuta kama kitimoto pamoja kulalamika sukari imekuwa bei ghali
Halafu mwili ukishazima data na likitambi lake ndio anajua kuna Muhimbili
 
Ubishi wenu ndio maana presha, kisukari, figo kufeli, matatizo ya moyo, bawasiri nk hayawaishi
Kuna siku nchi yetu itampata kiongozi dikteta mwenye kuamini na kusimamia sayansi. Bado hatujawahi kupata kiongozi huyo.

Tukimpata, Tanzania itakuwa moja ya nchi Bora Africa kama siyo duniani kwa sababu tuna nguzo zote kasoro hiyo.

Huyo dikteta awe ni muuaji.
 
Janabi aambiwe kuwa asilimia kubwa ya waTz wanakula ili wasife.
Sio kweli, kula kiafya hakuhitaji gharama kubwa kama mnavyofikiri

Watu mnadhani kula kiafya ni kula kuku, samaki nk Kila siku

Kwa gharama hizo hizo unazotumia unaweza ukala kiafya na ukajiepusha ma magonjwa ya kizembe huko mbeleni
 
Tatizo linaanzia pale mbuzi nyeusi zinakwambia zinajifanya zinaenda kiasili na huku zikifakamia matakataka yenye mifuta kama kitimoto pamoja kulalamika sukari imekuwa bei ghali
Halafu mwili ukishazima data na likitambi lake ndio anajua kuna Muhimbili
Wanakimbilia Kwa Dr Janabi hiyo huyo

Watu wanashindwa kujua kuwa magonjwa mengi tunayaita sisi wenyewe

Huwezi ukawa unakula kiafya ukapata kisukari (type 2), presha , kufeli figo nk
 
Nini maana ya unene??

Usije kuwa unatumia macho Yako kufanya hitimisho wa kuwa huyu mnene na huyo si mnene.

All in all datari yupo sawa 100%

Kwa sasa Kuna changamoto kubwa ya magonjwa ya mfumo wa maisha na tatizo kubwa ni vyakula vya wanga (processed carbohydrates), sukari, mafuta, chumvi nyingi, pamoja na kutofanya mazoezi /kazi zinazoshabihana na mazoezi.

Tunavyozungumzia unene lazima ipimwe BMI na watu wengi Wana uzito mkubwa japo wenyewe wanaona ni kawaida tu na mayokeo yake ndio magonjwa kama kisukari, presha, moyo, kufeli figo, upungufu wa ngubu za kiume nk

Hivi ushangai kukuta vijana wengi chini ya miaka 35 kuboost nguvu za kiume?? Shida ni ulaji tu
Huu upumbavu ulioandika ndo ninaoukemea. Nchi ina tatizo la utapiamlo nyie mnaongea kama vile watu wote wanapata hata hizo Carbohydrates kirahisi. Mnazua taharuki kipumbavu
 
Back
Top Bottom