Dkt. Jingu: Wanawake wapewe nafasi za Uongozi si kwa sababu ni wanawake ila kulingana na uwezo wao

Dkt. Jingu: Wanawake wapewe nafasi za Uongozi si kwa sababu ni wanawake ila kulingana na uwezo wao

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu, amewataka viongozi wanawake chipukizi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kuchukua hatua madhubuti na kuleta mabadiliko halisi katika safari zao za uongozi

‎
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa uongozi wa wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute), Dkt. Jingu amesisitiza umuhimu wa kutumia maarifa waliyonayo kuleta ushawishi na matokeo chanya katika jamii

‎Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Uongozi Institute, Kadari Singo, amesema taasisi hiyo imezindua mpango maalum wa wanawake katika uongozi, ambao umelenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za kisiasa, kiuchumi na kibiashara na kuongeza kuwa takwimu za Kimataifa zinaonesha ni asilimia 33 tu ya wanawake wanaoshikilia nafasi kubwa za maamuzi duniani


‎

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom