Uchaguzi 2020 Dkt. Kavishe: Wawakilishi wa CHADEMA waliomba Tundu Lissu apunguziwe adhabu, maana yake walikiri kosa

Uchaguzi 2020 Dkt. Kavishe: Wawakilishi wa CHADEMA waliomba Tundu Lissu apunguziwe adhabu, maana yake walikiri kosa

Mkuu, kwa kukusaidia tu kuna uandishi (au mpangilio wa maneno) wa kwenye vitabu vya kitaaluma, articles, magazeti, vitabu vya stori n.k. Na kila sehemu waweza kuta mpangilio wa maneno tofauti na uliozoea ktk sehemu nyingine. Lakini kutokuujua kwako hakufanyi kuwa huo mpangilio mgeni kwako sio sahihi.

Jijengee mazoea ya kutowashambulia watu ktk lugha ya kiingereza. Hii lugha ina wenyewe. Na yawezekana kabisa huyo Robert Amsterdam akikuzungumzisha hicho kiingereza usielewe kabisaa anachoongea kutokana na udhaifu wetu waTz ktk lugha hiyo ya malkia.

Si watanzania wote wana udhaifu katika lugha ya kiingereza.

Ipo sehemu ya watanzania wanaweza kukaa meza moja na huyo Robert Amsterdam wenu na wakajadili masuala yote kwa upana wake.
 
Huyu sidhani kama ni PhD holder. Jina lake halisi ni Kawishe.
 
Upo sahihi Mkuu, ila wengi wao wana udhaifu mkubwa tu ktk lugha hiyo, hadi waliofika level za juu madigirii.

Labda uamue kuvaa miwani ya mbao.

Ndo nakufahamisha mkuu kwamba wapo watanzania ambao wana uwezo wa kuongea na huyo jamaa kiingereza kizuri na chenye grammar nzuri na wakaelewana uzuri tu.
 
Katibu wa kamati ya maadili ya tume ya uchaguzi Dr Kavishe amesema wawakilishi wa Chadema waliomwakilisha Tundu Lisu waliomba adhabu ipunguzwe na hii maana yake ni kuwa wamekiri kosa.

Kavishe amesema wajumbe wa kamati walibishana sana na hatimaye busara ilitumika kwa maslahi mapana ya taifa adhabu ilipunguzwa na kuwa kifungo cha kutofanya kampeni kwa siku saba (7)

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Mfumo wa vyama vingi ni mwiba kwa watawala wa nchi za ki Africa. Mawazo ya wananchi wengi yapo enzi za ujima, hata kwenye kura ya kuingia siasa ya vyama vingi 80% walikataa. Kuingia vyama vingi ni baada kusoma nyakati na ile 20% ilikuwa ni wenye upeo mkubwa. Kwa yanayo tokea sasa ufumbuzi wake ni dola kukubali mfumo wa democracy na nchi itulie au mfumo inao uusudu wa mwenye nguvu atawale na vurugu iwe sehemu ya maisha.
 
Ndo nakufahamisha mkuu kwamba wapo watanzania ambao wana uwezo wa kuongea na huyo jamaa kiingereza kizuri na chenye grammar nzuri na wakaelewana uzuri tu.
Uko sahihi kabisa wachache hawawezi kukosekana.

Pia inategemeana na exposure ya mtu husika. Kadiri unavyokutana na watu wa sehemu tofauti tofauti na kuishi nao au hata ukiwa mfatiliaji mzuri wa vipindi vyao vya television unajifunza namna zao wanavyoongea kiingereza na hivyo unakuwa na uwezo wa kuwasikiliza na kuelewa waongeacho.
 
Acha kukimbia hoja, elezea makosa yake ya kilugha na kisha useme usahihi alitakiwa aandike vipi (kama kweli wewe umeiva English kihivyo kama unavyotaka kutuaminisha hapa jamvini)

Huyu ndiye Robert; amezaliwa New York (US), kakulia na kusomea Canada na anaishi London (Uingereza). Nchi zote hizo wanatafuna kiingereza, hakuna kiswahili wala lugha za kkkabila.

Halafu wewe mmakonde wa Ntwara (Uswahilini) wataka kujitia kumdogesha ktk lugha yake mama.
========
View attachment 1588557
Kingereza kimekosewa
 
Tatizo la wengi wanafikiria JF ndio inafuatwa na Watanzania wengi wapiga kura. Hapa watu wanaingia kuona nini kinasemwa, Je, kina ukweli wowote, nk. Tena sio hii JF ya sasa. Watu walimzuia rais kuingia humu na jina lake kamili enzi zile itakuwa sasa hivi wakati wamenunuliwa na Chadema? Propaganda tu siku hizi.


Nipo ofisini hapa chini napokea simu .... ... ..


1601667838980.png


Khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

1601667910126.png


?
 
Wala hamna haja ya kujikomba ,tunajua Mfumo mmbovu wa Nchi hii unampa nguvu Raisi alie Madarakani.Yeye hakosei ni malaika mkuu na mtakatifu sana .
Huo utakatifu wake feki feki lazima upigwe spana za kutosha
 
Na yule anayetumia police, nec na TISS ni kibaraka wa nani? Au matumizi ya vyombo vya umma kwa manufaa ya watu wachache ndo uzalendo?
Kutumia vyombo vya dola dhidi ya kibaraka ni baraka hata kwa Mungu
 
Mkuu tume inaweza kufanya hivyo,na je ikifanya hivyo what next, ? Je mafuriko ya watanzania kwake wakikataa mtaweza kuwazuia kwa njia gani!!!? lissu mpaka mda huu anajeshi kubwa la mafuriko ya watanzania ,unafikili ni chombo gani Cha ulinzi chaweza kukubali upuuzi Kama huu,watu hawalali juu ya nchi yao Leo eti tume ifanye mzaa wa kubet na amani ya nchi alafu waichekee,watakatalowa kweupe nakwambia , hao wanaviapo vyao juu ya nchi Wala sio chama chochote au mtu yoyote,japo kwa namna moja au nyingine wanaweza fanya fair tu kwa Mambo madogomadogo ila si maslahi mapana ya taifa
Acha ujinga hakuna watanzania wenye ujasiri wa kupambana na mtutu bado hawajazaliwa
 
Onesha hayo makosa unayodai kama kweli wewe mweledi wa lugha, unakwama wapi ndugu yangu?

Kiingereza ni lugha pana, haiko finyu kama hivyo unavyoisawiri.

Na hata kama angekuwa kaandikiwa, basi jambo la awali ingekuwa ni yeye kupitia maandishi na kusahihisha lugha (kama kuna makosa). Hiyo (umakini) ni kawaida kwa wazungu ambao wamesomea fani nyinginezo, si kwambii mtu aliyesomea law na mashuhuri duniani kama huyo Robert umakini wake utakuwa juu kwa kiwango gani.
Sasa hapo unatetea nini kwa mfano...unajidhalilisha tu
 
Lissu ana maagano gani na huyu jamaa na "wazungu"? Naanza kuwa na wasiwasi, ni hatari kama tutakubali kuchaguliwa kiongozi wa nchi na mataifa ya nje, haijalishi hata kama tuna hali mbaya kiuongozi kiasi gani.
Mkuu kama ume note lisu siku hizi hata akiandika kitu mtandaoni anaandika kwa lugha ya kingereza! Unajiuliza huyu ana agenda gani?

Huwa nasema kila siku hapa huyu Amsterdam anazidi kumaharibia Lisu ila wafuasi wa Lisu hawaelewi.
 
Hakuna haja ya kujieleza Kiasi hiki!!!!


Upendeleo unaonekana waziwazi!!!!
 
Wamtoe ndio watanzania wataonyesha rangi zao vizuri. Muda wa kuwaogopa polisi ulishapita, haki itendeke na siyo NEC kubeba watu mgongoni.
Nlifikiri sasa hivi uko barabarani umekinukisha, kumbe unasubiri uatolewe jumla?
 
Back
Top Bottom