Dkt. Kigwangalla afungua duka la maziwa Kunduchi Mtongani, asema sasa anajikita kwenye ufugaji

Dkt. Kigwangalla afungua duka la maziwa Kunduchi Mtongani, asema sasa anajikita kwenye ufugaji

"ujasiriamali unalipa kuliko kitu chochote"[emoji848][emoji848][emoji848].
Huyu anampiga dongo magufuli
 
Maziwa na asali vitu vya kipekee kabisa Hongera Dr, kutusambazia kimoja wapo
 
Dkt. Kigwangalla ambaye ni waziri mstaafu wa Serikali ya awamu ya 5 amesema kwa sasa amejikita kwenye ufugaji kwa kuwa ujasiriamali unalipa kuliko kitu kingine chochote.

Kigwangalla amesema kwa sasa anamiliki shamba kubwa la mifugo huko Mvomero mkoani Morogoro ambako anazalisha ng'ombe wa kisasa akiwa amejikita kwenye uzalishaji wa madume ya mbegu na maziwa.

Jijini Dar es salaam amefungua duka la maziwa maeneo ya Kunduchi mtongani linalosimamiwa na mke wake.

Dkt. Kigwangalla amewataka vijana kujikita kwenye ujasiriamali wasisubiri ajira kwani ushindani wa ajira ni mkubwa.

Maendeleo hayana vyama!


!
!
wakati huo huo anaendelea kuwa mbunge au?
 
Mi namsifu kwa kuchagua location mtoni ni sehemu yenye biashara sana mpaka waje washituke kashatembea na gape
 
Mwambie tunawakumbuka Ng'ombe wa Wasukuma waliokamatwa pori la Lwafi mkoani Katavi, aliowapora na kujimilikisha baada ya kukamatwa hifadhini na kusafirishwa usiku kwenda kufichwa kwa rafiki yake Salum Sumry mmiliki wa zamani wa mabasi ya SUMRY ambaye kwa sasa ana shamba linaloitwa MSIPAZI FARM huko wilaya ya Nkasi Rukwa na kisha kusafirishwa kama Ng'ombe wanaopelekwa mnadani Pugu kumbe wanachepushwa kwenda kwenye shamba lake Mvomero. Viongozi wa CCM waendelee kudhulumu wananchi huku wakijifanya Watakatifu.
dunia hii kweli haina siri
 
Back
Top Bottom