Dkt. Kikwete: Ninaandika kitabu cha historia yangu ambacho ninaelezea mambo mengi hata yale msiyoyajua!

Dkt. Kikwete: Ninaandika kitabu cha historia yangu ambacho ninaelezea mambo mengi hata yale msiyoyajua!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
1610085103043.png

Rais mstaafu wa awamu ya 4, Mh. Mrisho Jakaya Kikwete amesema kwa sasa anaandika kitabu cha historia ya maisha yake ambacho kitaelezea mambo aliyoshiriki, aliyoyashuhudia na aliyoyaona katika maisha yake binafsi na yale ya siasa.

Kikwete amesema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi Salama Jabir katika kipindi cha Salama leo.

Chanzo: Eatv.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kikwete nae anataka kutubu
Vitabu ni urithi mzuri sana kwa vizazi vijavyo. Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amelifanyia mengi taifa hili. Mbali na kuwa rais kwa kipindi cha miaka10 amehudumu kwenye serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania tangu akiwa kijana.

Kwangu mimi JK anabaki kuwa shujaa aliyeweza kutegua mtego wa kumuingiza mtuhumiwa wa ufisadi ikulu na kutuletea Chuma JPM💪

Naamini kuna vingi tutajifunza kupitia kitabu chake

Mungu ampe maisha marefu yenye afya na furaha tele Jakaya Kikwete
 
Rais mstaafu wa awamu ya 4 mh Mrisho Jakaya Kikwete amesema kwa sasa anaandika kitabu cha historia ya maisha yake ambacho kitaelezea mambo aliyoshiriki, aliyoyashuhudia na aliyoyaona katika maisha yake binafsi na yale ya siasa...
Ni jambo jema, lakini atakumbushia kuhusu yule jamaa aliyetaka kumbwaga jukwaani 2005 pale Ccm kirumba?
 
Najua hatosahau kutueleza kilichomuua Dk. Omar Ally Juma na uhusiano wake na Rostam Aziz kuhusu like briefcase jeusi pale hoteli ya Kilimanjaro.

Na pia atatuambia kwa nini alishindwa kutamka jina la Dk. Alli Mohhamed Shein kwa mara ya kwanza hadi RA alipomtambulisha kwake bila kusahau lile shimo la tanzanite maarufu kama "Shimo la Mwarabu" pale Mererani sasa analichimba nani baada ya ya mzungu wa SA kufurushwa?
 
Back
Top Bottom