Dkt. Kimei: Serikali ikakope kwenye soko la nje ili ikamilishe miradi ya kimkakati SGR na Bwawa la umeme

Dkt. Kimei: Serikali ikakope kwenye soko la nje ili ikamilishe miradi ya kimkakati SGR na Bwawa la umeme

Kwani kodi alikuwa anachukua za kazi gani? kwani Nyerere,Mkapa,Mwinyi,Kikwete hawakujenga vituo vya Afya kwenye awamu zao?
Narudia tena tembea vijijini uone maboresho ya vituo vya afya na miundo mbinu...
alafu tafuta kazi ufanye mm nipo bize job....
nikipata chansi nitakujibu kwa mapana badae
 
Kwani Mwendazake alikuwa anafanyaje hadi mambo yanaenda?
Daah ilikuwa balaa madai ya walimu.. Kupanda madaraja watumishi, wastaafu kucheleweshewa malipo.. Wengi hawakupata. Kodi za kubambika, faini kubwa.. Aisee acha mkuu Mwendazake tutamkumbuka
 
Narudia tena tembea vijijini uone maboresho ya vituo vya afya na miundo mbinu...
alafu tafuta kazi ufanye mm nipo bize job....
nikipata chansi nitakujibu kwa mapana badae

Acha kukariri dunia ni kijiji hata hapa nilipo ninaweza kuiona New york city ,weka taarifa ya hivyo vituo vilivyojengwa na sio kusikiliza taarifa za uongo alizokuwa anatoa MEKO.

Hapa nilipo nauza mkaa nasubiri wateja ,pia ni dalali ,pia ni fundi ujenzi.
 
Wapambe wameanza kujipigia chapuo kama zama za jiwe!

Jiwe alituambia tunajenga kwa pesa zetu za ndani kwani imekuaje tena?
 
Tunajenga kwa fedha za ndani mkuu
Kwani ukikopa unakuja kulipa kwa kutumia nini? Au unalipa kwa fedha zinazotoka wapi? Unajua vigezo vya mtu, taasisi au nchi kukopesheka? Au unadhani kujenga kwa pesa za ndani maana yake ni kujenga kwa cash (fedha taslimu)?

"Fursa hujitokeza na huenda na wakati, ili kujinufaisha na fursa hizi tunahitaji uwekezaji warasilimali kwa wakati muafaka. Wakati mwingi rasilimali alizonazo mtu au taasisi hua hazitoshelezi kutokana na uchache wake au wingi wa fursa zilizopo. Hapa ndipo haswa uhitaji wa nyongeza (mkopo) ya rasilimali toka kwa ndugu, jamaa, jirani, rafiki au taasisi huja. Na hii kwa kiasi kikubwa hutokana na fursa zinaendana na wakati, hivyo ili kujinufaisha nazo tunahitaji kupata rasilimali za uwekezaji kwa wakati muafaka na zinazotosheleza. Na ndio maana watu husema "muda ni mali" ukiupoteza na fursa hupotea. Fursa zinawezakua za kijamii ,kiuchumi nakadhalika. Mkopo unapata rasilimali (mfano fedha) yote kwa mkupuo kisha unaurejesha kidogokidogo."
 
SGR fedha za ujenzi jpm slizitoa wapi? Baada ya yeye kufariki mnaanza kuibuka na kwenda kukopa nje?
...hata mwezi haujaisha wameisha anza kuwaza kukopa kumalizia miradi kwani Pesa zilizokuwa hapo hazina wamezipeleka wapi🙄🙄 hii awamu Tembo atabanda ndege sio twiga tuu
 
Back
Top Bottom