Dkt. Leonard Chamuriho atajwa na Rais kuwa ni mtaalam wa kufanya mazungumzo - "Negotiation Expert". Je, hawa watu tunao wangapi?

Kwanini wanapenda kufichaficha mikataba ?

Ova

Sidhani kama wanaficha nafikiri ni suala la serikali ikikuwakilisha wewe mwananchi wa kawaida.

Hivyo serikali ikiharibu basi ni watanzania wote wameharibu.

Sidhani kama raisi John Mafuguli amekosea kwenye hii mikataba mipya hadi sasa.

Hivyo tumwamini kwani yeye anatuwakilisha.
 
Ni kweli kwa kabudi tunasubiri kishika uchumba stigler tunaolewa kabisa

Matatizo yalianzaia kwa akina chifu Mangungo wa Msovero ambao hawakuwa wnafahamu kusoma na kuandika.

Sidhani kama serikali ya sasa inakubali mambo hayo ya kizamani ya kusaini mambo usoyafahamu.
 
huo mkataba wewe umeuona? au kwa vile magu kasifia basi unaamini ni kweli?

Raisi amemsifia mtaalam wa kufanya mazungumzo.

Hatukuwahi kusikia kuwa Tanzania inaweza kuwa na watu ambao wanaweza kukaa meza moja na wazungu na wakazungumza na kikaeleweka.

Au ndugu umewahi kusikia huko nyuma, hebu tupatie ushuhuda.
 
HATA PROF KABUDI TULIAMINISHWA HIVYO NA MPAKA LEO HAKUNA HELA, SENTI WALA PESA
 
Tumia akili japo hata kwa siku moja badala ya kukurupuka na majibu ya Lumumba!!! Umekuwaje siku hizi weye? 😳😳😳

Zamani ulikuwa ukiandika posts zilizoenda shule sana siku hizi umeunga tela kwa mamburula!!!!

Kama zipo sababu za msingi za kujitoa kwanini haziwekwi hadharani!? Unajitoa vipi katika mpango ambao Wananchi wako walio wengi wanauunga mkono!? Si ndiyo UDIKTETA wenyewe huo?

Kama mpango huo unahusu UN basi kuna sababu za kujitoa.
 
tuione mikataba hio aliyoingia

Sasa akionyeshwa kila mtu si itachukua mwaka.

Pili unapaswa kuiamini serikalki yako inayokuwakilisha kwenye masuala mazito yanayohusu nchi kama haya ya miradi mikubwa.
 

🙂

Dah! mkuu, haya ngoja niangalie wapi nakosea.

Ila taarifa hiyo ni kwamba kila kiongozi anaengia akikuta mambo fulanifulani huwa wana uwezo wa kukubali mambo hayo yaendelee au kuamua vingine.

Huyu wa sasa amepangua mambo mengi tu,

Nafikiri ndivyo ilivyokuwa.
 

Nakushukuru mkuu kwa kuliona hilo.

Ila nasikitika hadi sasa sijapata post yoyote inayoongelea kwamba hawa wataalaam wa kufanya haya mazungumzo nchi yetu inao wangapi.

Kama nilivyoleza kuhusu Negotiation ni kazi na ni kipaji na pia kinalipa pesa sana.

Halafu kuna mtu amesema huyu Dr Chamuriho pia ni mshauri elekezi yaani ni consultant.

Ni vigumu sana kuamini kwamba tunao watu kama hawa.
 
Sekunde 60 (Sixty Seconds) za Dkt. Leonard M. Chamuriho ktk video clip:

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt .Leornard Chamuriho imetoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Fidia kwa wakazi wa maeneo yanayopitiwa na mradi wa reli ya kisasa (SGR), ambapo amesema Chuo cha Ardhi kinaendelea na uthamini
Zinaonesha Dkt. huyu wa structural engineering hana ubobezi ktk masuala ya mazito aliyotaja mwanzisha uzi kuhusu Dkt. Chamuriho

Dkt. Chamuriho akielezea ushoroba :
Source : BMG online
 

That's him, the expert.

Thanks.
 
That's him, the expert.

Thanks.

Hii tabia ya viongozi wetu kugeuka kuwa wakalimani kila wanapotembelewa na wageni wanaoongea lugha ya kigeni kama ktk video clip ya pili huwa inakera.

Huu siyo utaalamu wa negotiation skills bali ni kitu kingine kabisa (ukalimani), viongozi wetu wakitoka kwenye vikao na wageni watumie muda mwingi kuelezea msimamo sahihi wa serikali baada ya mazungumzo.

Maana mara nyingi utasikia wageni wetu wakitoa ufafanuzi baada ya viongozi wetu kupotosha umma!

Hivyo naungana na wachangiaji wengine makini JamiiForums kuwa na wasiwasi na sifa hizo za ziada anazobebeshwa Daktari huyu wa masuala ya ujenzi.
 
Raisi amemsifia mtaalam wa kufanya mazungumzo.

Hatukuwahi kusikia kuwa Tanzania inaweza kuwa na watu ambao wanaweza kukaa meza moja na wazungu na wakazungumza na kikaeleweka.

Au ndugu umewahi kusikia huko nyuma, hebu tupatie ushuhuda.
hatujawahi kusikia kwa sababu hatujawahi kusaini mikataba ya akili...



hata magufuli nae mwongo, anamsifia huyo kwavile katii maagizo yake, aweke mkataba tuuone km kweli una maslahi na sisi........

labda ni maslahi ya magu na watu wake
 
Sasa akionyeshwa kila mtu si itachukua mwaka.

Pili unapaswa kuiamini serikalki yako inayokuwakilisha kwenye masuala mazito yanayohusu nchi kama haya ya miradi mikubwa.
ubongo wako una shida..... bye
 
hatujawahi kusikia kwa sababu hatujawahi kusaini mikataba ya akili...



hata magufuli nae mwongo, anamsifia huyo kwavile katii maagizo yake, aweke mkataba tuuone km kweli una maslahi na sisi........

labda ni maslahi ya magu na watu wake

Nchi gani umeona wanaweka mikataba wazi kwa wananchi wake iwe Ulaya, Marekani au kwingine?

Ukinijibu hili suali utakuwa umewasaidia wengi.
 
Jamaa he is the Best Alikua lecturer kilaka kila course alikua anafundisha pale coet civil Engineering wakati lectures wenzie walikua wanashindwa
 

Yaani unabisha kwamba Dr Chamuriho si mtaalam wa kufanya mazungumzo kwa niaba ya serikali, yaani hana negotiation skills?

Hufahamu kwamba negotiation skills zaenda sambamba na communication skills yaani umakini kwenye kutumia lugha khasa ya kiingereza na kujenga hoja na ikakubalika?

Pia unabisha na unasema kwamba hata kwenye ununuzi wa ndege yeye alikuwa ni mkalimani?

Ni kweli kwamba hufahamu wapo wakalimani wa serikali ambapo ukalimani nayo ni taaluma?
 

Hizi sifa za ziada yaani kuwa nguli / uzoefu kazini ktk kushawishi / kuendesha mazungumzo kwa hoja kuhusu mikataba ya kikanda au kimataifa inayoambatana makubaliano ya kimataifa, treaties, sheria kibao n.k hana.

Ila la eneo lake la kufundisha course /degree za structural / civil engineering sifa / uzoefu anazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…