Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli aomba kura mtandaoni

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli aomba kura mtandaoni

Kinachowatesa nyie ni kufikiria mambo yataendeshwa kwa mazoea tena. Inajulikana wako maadui wa ndani na nje ya Taifa la Tanzania. Maadui wa ndani wanao mamluki wao kwenye mifumo ya uendeshaji nchi bila kwenda kwa chenga za mwili huwezi fika. Vita ya ndani ndivyo inavopiganwa hivyo.

JPM aliye kwenda kumzika Mkapa wakati wa kurudi akatembea kwa Miguu kuvuka daraja la Mkapa na akapokea zawadi ya jogoo Mkiru, akatumbua wakutumbuliwa. Ndio unaleta propoganda zako za kilaghai hapa eti anaogopa.

Kwani mlipanga kufanya nini akiwa anafanya kampeni huko Kusini apaka ikuume hivi kwa yeye kutoenda mikoa ya kusini?

Wezi na Mafisadi waliozalishwa Tanzania awamu hasa za 3 na 4 mmegeuka kuwa maadui wa Taifa hili kwa kujitahidi kukwamisha serikali ya awamu ya 5. Nyie ni wajinga kabisa hamna hata akili kama nyie kipindi chenu mlisimama hamkukwama pamoja na kupinduliwa kwa pambio la chama. Vipi sasa mfikiri hawa wa awamu ya 5 watawaangalia tu ili muwafanye waonekane mbele ya macho ya Watanzania wameshindwa?

Mambo katika Taifa hili hayaendeshwi kwa mazoea tena, jueni hivyo na mkae mtulie. Unaweza kumuita JPM muoga, Rais aliye thubutu kuing'oa accasia london stock exchange? Licha ya vitisho mlivyokuwa mwaviendeleza kwa propoganda zenu uchwara?

Akaikoa nchi ya Tanzania kutoka kubadilishana dhahabu na misaada ya vyandarua vya mbu. Eti, eti, eti, katumwa na Bahima, huna hata aibu wala soni wewe, hujishtukii kutumika kama tambara la kufutia shombo. Umelipwa nini kinachokufanya kudhalilisha utu wako na heshima yako kiasi hiki? Mtu aliyetumwa na Bahima angezuia madini yetu yasiishie Rwanda na kwengineko? Angejenga ukuta Mererani.?Angehangaika na Bwawa lilolomshinda Nyerere ubunifu wa kulijenga na huku nchi iikiwa na raslimali tele za kuwanufaisha Amiri Jamal na wakina Sabudu? Waliomfuatia Nyerere nao wakajibaraguza kulijenga ili wachote raslimali zilizojaa selous wakishirikina na mabwana zao wazungu na waarabu, sijui wahindi wanao waamini na kuwanyenyekea kama miungu -idols.
Usipanik Bro..
Hata Gobershov alijenga viwanda , lakini huku akizorotesha nguvu za USSR Kijeshi, Usalama na Umoja kama taifa ....so hivyo vitu sio substitute ya uhai na uimara wetu kama taifa hasa UMOJA ...sasa ukishapanda ubaguzi kwenye nchi hivyo vitu ..vina msaada gani .
ALAFU BRO UMEJIBU MOJA TU...Hayo muhimu ya kuzembea makusudi kugharamia utunzaji wa mifumo yetu ...nadhani pia umeona lakini kwakua unajua nini kinaendelea umeamua hilo usiongelee kwakua ndio ukweli .
MSICHEZE NA HUKO BRO , WAZALENDO WANA UCHUNGU .....
kweli sisi ni wa kuchinjwa kama kuku na watoto wadogo ....wakati vifaa vipo lakini havina msaada kwakua havina matunzo ......
BRO utapata wapi uweledi na utimamu kama vijana wakienda KOZI wanalipishwa 'ADA" hakuna nchi inafanya hivyo hata wakati mgumu sana kwenye nchi yetu baada ya mwalimu kutoka akaingia mwinyi haijawaji kutokea Askari wanalipishwa kwenda mafunzoni ...tena sana wanalipwa ..
Mnategemea hao ndio mtakaowaamini kukabiliana na jambo lolote .....hamasa iko chini sana ....umeona lini uchaguzi unafanyika hawana vifaa na magari mapya ....msicheze na usalama wa nchi .
 
Mabaya mawili yanaweza kufuta kumi mazuri
 
JPM umeshapata mitano tena.
Eenh, imekuwa hivi tena?

Naona mioyo inazidi kuwa mizito!

Hapa hakuna msaada tena mkuu.

Safari hii hata wenye njaa ya siku moja watakikataa chakula ili kesho yao iwe nzuri.
 
Kufungua account Twitter ni dakika tatu tu au chini ya hapo.

SIKO TWITTER JE UNAWEZA NILETEA UPDATE MPAKA SASA ANA 'LIKE NGAPI'? maana hizo 3,317 sikutegemea zitoke twitter kwa wanaojielewa labda istagram
 
Jeshi lituondolee hili balaa liachanae na siasa.

Video ya huko mtwara
 
Amini msiamini mnaomchukia JPM kwa sasa mnajitahidi kutafuta faraja japo muuburudishe moyo wenu hata kwa sekunde kadhaa. Lakini ukweli unaufahamu fika kubwa mh.JPM anapendwa na kukubalika na watanzania kuliko mgombea urais yoyote TZ. Poleni sana JPM kawakosea nini hadi mumchukie? Au ndio zile fasheni za ki Libya. Toeni tongotongo hakuna mtu ataekuletea pesa mfukoni.

MAGUFULI4LIFE.
Hujapatwa we we ndo mana unasema hivyo ungekua umekopwa korosho ungejua kwanini hawampendi ungebomolewa nyumba ungejua ,unge kua mfanyabiashara ungejua ungekua mfanyakazi ungejua hakuna kundi lililosalama kwa huyu MTU wako isipokua wanaokula meza moja nae
 
Wanapiga vita matumizi ya mitandao na vyombo huru vya habari alafu huku wanatumia vyombo hivyo-hivyo kuomba kura. Hawaeleweki, sipangiwi nani wa kumchagua, tumenyanyaswa vya kutosha tunataka uhuru, haki na maendeleo ya watu .
The best response I have seen today!
 
Ndiyo sababu Twitter inazidi kuwa maarufu sana kwa Watanzania kwani uhuru wa kule hakuna tena. Yule kigogo serikali ilimchomea afungiwe na akafungiwa lakini wabongo hawakukubali wakaiandikia Twitter kwa wingi kwamba hajatenda kosa lolote na Twitter wakawaelewa Wabongo hivyo Kigogo akafunguliwa. Sikuwa kufikiria kwamba kuna mtandao utakuwa kipenzi cha Watanzania kama JamiiForums lakini kwa uhuru uliokuwepo kule Twitter nadhani kwa kasi hii Twitter inaweza kuwa maarufu zaidi kuliko JamiiForums.
Kule twita watu wana majibu ya hovyo sana.

Hawajawahi kumuacha mtu salama.
 
Eti wanashindana na vyama dhaifu lakini wakati huo huo maccm yanahofia uchaguzi huru na wa haki na pia kura kuhesabiwa hadharani! Akili ni Nywele hata maccm wana zao!

Atapita Tena kwa kishindo kikubwa mno
 
Ikifika tarehe 27 nalala usingizi mzito niamke tarehe 29 niendelee na mishe zangu . Ifike mahali kila
mtu awe na uhuru wa kweli wa kufanya maamuzi yake binafsi bila kuombwa wala kulazimishwa. Siwapendi wagombea wote wa awamu hii 🙅🏽🙅🏽🙅🏽🙅🏽🙅🏽🙅🏽
Hapa sio swala la"kupenda au kutopenda wagombea."

Hapa ni swala la Tanzania yenyewe.
 
Back
Top Bottom