Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli apangua hoja ya kujenga Uwanja wa Ndege wa Chato kwa ustadi mkubwa

Swali zuri sana. Huu uwanja utakuwa hauna kazi tena, tutaubadilisha utakuwa wa kuchezea mpira. Kawaida mtu aliyejenga uwanja wa ndege, akishamaliza muda wake wa urais, viwanja vya ndege vyote alivyojenga huwa vinabadilishwa na kuwa viwanja vya mpira!
Hizi ndizo zinaitwa akili za kimaskini. Viwanja vyote vya ndege vinakarabatiwa kwanini huo wa Chato ndio ufe baada ya rais kuondoka?.

Kwani akiondoka rais mahitaji ya viwanja vya ndege yatatoweka?.
 
Nimecheka sana hapo 'kwa ustadi mkubwa'.
 
Kuna upigaji
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Tunataka ripoti ya gharama za uendeshaji ndege kabla ya kipindi cha corona.

Zilitokaga mara moja tena zilikuwa leaked, ripoti ni kwamba zilikuwa na hasara nzuri tu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Hoja kama hizi zinawaondolea heshima makamanda wenzangu. Kipindi hiki cha Corona unategemea Atcl wapate faida?
Atcl kwa nini isikaguliwe na CAG wakati ni shirika la umma? Tunajiabisha tuwe makini kujibu hoja
Duhh.... Nimekustukia mzee baba
 
Huko Makambako sasa hivi, petroli zaidi imemwagwa motoni!!
 
Ndiyo maana wapambe hawataki atokee kwenye midahalo. Kumbe tatizo ni kuwa ana ufundi mkubwa wa kupangua hoja kuliko kaseja!
 
Nadhani kila mvuta kamba huivutia kwake, hivyo ubinafsi ni silka ya wanadamu wote.
faida ya kununua ndege itachukua muda mrefu kupata faida, tena na hii corona ndo kabisaa hasara inaongezeka
Magufuli sio rais wa Kwanza. Tuambie mwingine aliyevutia kwake kwa mtindo huu
 
Kama anajijua akiondoka hakuna ndege itatua huko kwa nini kaupeleka ujengwe huko? Huyu hana mpango wa kung’atuka. Kashajiwekea uwanja wake wa mpaka kifo, midege ya serikali iwe inatua huko.

Bashiru anajitahidi kumuelewesha kiaina mara kwa mara juu ya ukomo wa Urais ila wanampigia mbuzi gitaa. Jamaa yao hawatamuweza akirudi tena kwenye hii ngwee inayofata. Wakina Bashiru na wenzie wanatakiwa wajiandae kumtoa tu sasa hivi, la sivyo nchi itaingia kwenye ukurasa mbaya sana zaidi ya hapa.
 
KWANI KUNASHIDA GANI KUJENGA UWANJA CHATO?
KWANI CHATO SIO TANZANIA?
KWANI UWANJA WA NDEGE CHATO SI UWANJA WAWATANZANIA WOTE?
KWANI UWANJA WA CHATO NI MALI YA MAGUFULU NA FAMILIA YAKEEE??
Hoja si kujenga uwanja bali faidi ya huo uwanja maana ata Mabotu alifanya aya aya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…