Mama kaahidiwa cheoMama Tibaijuka wape heshima wahaya wenzako
Umeahidiwa cheo unakenua
Bwana mahera njoo huku kuna rushwa inatangazwa wazi wazi
Magu bana anaongea kama si Rais wa nchi, CCM mlibugi big timeRais Magufuli leo yupo mkoani Kagera akitokea Chato kuendelea na kampeni za kuwania Urais kwa muhula wa pili, akiwa njiani amesimama Muleba, lililokuwa jimbo la mama Anna Tibaijuka upande wa Muleba Kusini. Hii ni sehemu ya yaliyojiri huko...
Magu yupo kila TV na kila media kinachoshangaza Lissu kazimwa kila kona lakini bado sindano zake zinamfikia na kumchomaVipi na Lisu nae si anafuatilia sana kampeni za Magu?
Hizo ni dalili za kifilisika Sera kichwani..nakwambia mtanzania wa Leo huwezi mdanganya hiviMkoa wa Kagera huyu mzee anakwenda kupoteza muda wake tu, hawajasahau kauli zake za hovyo wakati wa tetemeko.
Ni vizuri akitumia mkutano huu kuwaeleza rambirambi zao za tetemeko zimekwenda wapi?
Mwaka 2015 mlijipaga moyo hivihiviiiii..mlichoambulia Mungu mwenyewe ndie anayejua...Sasa naona mnakuja na wimbo uleulee..subirini rungu la wananchiMagu yupo kila TV na kila media kinachoshangaza Lissu kazimwa kila kona lakini bado sindano zake zinamfikia na kumchoma
Una uhakika? Mkoa wa Kagera mwaka huu tunaenda kuvunja rekodi, kuanzia madiwani, waving mpaka Raisi! Ni mafiga matatu kwelikweli! Chadema na lissu wenu mtakuwa na raisi wa twita! Kichinjio ninacho hapa kituo cha kupigia kura ni hapa Kitendaguro ofisi ya kata! Wewe na wenzako hata huku Kagera hamjawahi kufikaMkoa wa Kagera huyu mzee anakwenda kupoteza muda wake tu, hawajasahau kauli zake za hovyo wakati wa tetemeko.
Ni vizuri akitumia mkutano huu kuwaeleza rambirambi zao za tetemeko zimekwenda wapi?
Kumbeee wasubiri vipimoRais Magufuli leo yupo mkoani Kagera akitokea Chato kuendelea na kampeni za kuwania Urais kwa muhula wa pili, akiwa njiani amesimama Muleba, lililokuwa jimbo la mama Anna Tibaijuka upande wa Muleba Kusini. Hii ni sehemu ya yaliyojiri huko.
===========
Anna Tibaijuka: Nashukuru sana mheshimiwa Rais kuniruhusu na mimi nikapumzike. Ninapopumzika, hapa tunaacha ni mahali salama. Kuna mtu mwenye mashaka na baba huyu? Kuna mtu mwenye wasiwasi? (Wananchi: Hamna).
Nyinyi wanangu wa Muleba, walio wengi hapa ni wanangu na wewe mheshimiwa Rais ukiwa mdogo wangu. Hapa Muleba, jirani yetu ni Chato, wembe ni uleule. Wazungu wanasema kama huyu Rais Magufuli ana mshikaji wake, wanasema natural allie ni Muleba Kusini, Muleba kwa ujumla.
Kwa hio kura hapa zitaendelea kuwa za heshima mheshimiwa Rais kama ilivyokuwa 2015. Hapa usiwe na shaka na mimi hapa mstaafu na dada yako, nashukuru sana.
BASHIRU: Hapa mimi ndiko ulikonitoa jalalani(Bukoba) maana kuna lugha ya jalalani, ukiwa Kagera sisi wasaidizi wako umetutoa jalalani na mimi niko kwenye jalala langu na jana nimekuona ukiwa kwenye jalala lako Chato, sasa ni zamu yangu, acha nijidai kwenye jalala langu la Kagera.
MAGUFULI: Miaka mitano iliyopita tulipita hapa kuomba kura na tuliwaomba kwa heshima kubwa, mgombea ubunge wakati alikuwa Prof. Tibaijuka. Mimi Prof. Tibaijuka ni dada yangu na nataka niwaeleze hata marehemu mume wake alipokuwa balozi kule Sweden, mimi nikiwa naibu waziri wa ujenzi na mbunge kwenye miaka ya 95 nilienda mpaka huko kwa hio Prof. Tibaijuka ninamfahamu.
Baada ya wakati ule, mheshimiwa Masilingi, aliyekuwa mbunge wa hapa kabla ya mama Tibaijuka nae ni rafiki yangu, tulihangaika nae wote kwenye barabara ya kwenda mpaka Kyamyora mpaka kuelekea Kimwali. Ndio maana alipomaliza kumuachia Pro. Tibaijuka, Masilingi nikamteua kuwa balozi na hata mpaka leo ni balozi kule Marekani, ndiyo faida ya kumteua unayefahamu.
Hata mama Tibaijuka amesema amestaafu lakini kwangu mimi hajastaafu.
Huyu Bashiru, hakuna mtu alitegemea atakuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, alikuwa muuza ndizi pale Kemondo, baadae akaenda chuo kikuu akafundisha lakini leo ndio katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, Muleba Oyee.
Serikali hii ina mavyeo mengi na ndio maana nimemwambia hata Prof. Tibaijuka, ameniambia hapa, mdogo wangu nimestaafu. Mimi nakwambia hapa, Prof. hujastaafu. Hauwezi tukamuacha Profesa akakaa tu hapa wakati kuna maeneo mengi ya kwenda kufanya.
Muachane na propaganda ambazo zinafanyika, kwamba mkituchagua sisi tutafuta kodi. Utafutaje kodi wakati kwenye mikutano yako unachangisha kodi?
Unasema utafuta kodi, ukienda kwenye mkutano, naomba mtuchangie, sasa wakiingia zile tulizozikusanya si watazitumia vibaya, zile tulizopanga kununua meli ambayo inatengenezwa pale, zitapotea.
Msichagua watu wasiomanika, msichague watu watakaokuja kutawala kwa matakwa ya watu wengine. Na si ajabu zikarudishwa hapa lockdown wakati Mungu ameshaimaliza.
Mh. Wakili msomi! Au acha tu, siulizi tena! Kampeni ziendelee!Ni jambo jema. Kampeni na ziendelee. Tuna jambo letu Oktoba 28!
Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.
Alisema, namnukuu: "Kama Rais Magufuli hata yaachia hayo makontena ya mchanga na kuyaruhusu yaende kwa wazungu hakika tutapigwa kama Gadafi na tutachakazwa ndani ya masaa 48 tutakuwa tumekwisha"
Njombe hiyooooo
Moto chini, uuwi , Lissu namba nyingine aisee
Wewe si ulisema kaahirisha? Muda sio mrefu utashangaa watu mada zako hawasomi sababu wanakuona kuwa huko reliable
Baada ya kujidhalilisha kwa kauli ya jalalani wanajaribu kubadilisha maana yake ingawa wanazidi kujichanganya.
Wanajitapa uchumi wa kati na kuwa tunapata maendeleo kama Ulaya, ni kwa nini sasa wanaanza kuita kila sehemu ni jalalani?
Mkumbushe Tibaijuka barabara ya Muleba Rubya kaitelekeza miaka minne kilometa 100 na point hazijaisha watu wanateseka
Ujinga mtupu Kama kawaida ya maccmRais Magufuli leo yupo mkoani Kagera akitokea Chato kuendelea na kampeni za kuwania Urais kwa muhula wa pili, akiwa njiani amesimama Muleba, lililokuwa jimbo la mama Anna Tibaijuka upande wa Muleba Kusini. Hii ni sehemu ya yaliyojiri huko.
===========
Anna Tibaijuka: Nashukuru sana mheshimiwa Rais kuniruhusu na mimi nikapumzike. Ninapopumzika, hapa tunaacha ni mahali salama. Kuna mtu mwenye mashaka na baba huyu? Kuna mtu mwenye wasiwasi? (Wananchi: Hamna).
Nyinyi wanangu wa Muleba, walio wengi hapa ni wanangu na wewe mheshimiwa Rais ukiwa mdogo wangu. Hapa Muleba, jirani yetu ni Chato, wembe ni uleule. Wazungu wanasema kama huyu Rais Magufuli ana mshikaji wake, wanasema natural allie ni Muleba Kusini, Muleba kwa ujumla.
Kwa hio kura hapa zitaendelea kuwa za heshima mheshimiwa Rais kama ilivyokuwa 2015. Hapa usiwe na shaka na mimi hapa mstaafu na dada yako, nashukuru sana.
BASHIRU: Hapa mimi ndiko ulikonitoa jalalani(Bukoba) maana kuna lugha ya jalalani, ukiwa Kagera sisi wasaidizi wako umetutoa jalalani na mimi niko kwenye jalala langu na jana nimekuona ukiwa kwenye jalala lako Chato, sasa ni zamu yangu, acha nijidai kwenye jalala langu la Kagera.
MAGUFULI: Miaka mitano iliyopita tulipita hapa kuomba kura na tuliwaomba kwa heshima kubwa, mgombea ubunge wakati alikuwa Prof. Tibaijuka. Mimi Prof. Tibaijuka ni dada yangu na nataka niwaeleze hata marehemu mume wake alipokuwa balozi kule Sweden, mimi nikiwa naibu waziri wa ujenzi na mbunge kwenye miaka ya 95 nilienda mpaka huko kwa hio Prof. Tibaijuka ninamfahamu.
Baada ya wakati ule, mheshimiwa Masilingi, aliyekuwa mbunge wa hapa kabla ya mama Tibaijuka nae ni rafiki yangu, tulihangaika nae wote kwenye barabara ya kwenda mpaka Kyamyora mpaka kuelekea Kimwali. Ndio maana alipomaliza kumuachia Pro. Tibaijuka, Masilingi nikamteua kuwa balozi na hata mpaka leo ni balozi kule Marekani, ndiyo faida ya kumteua unayefahamu.
Hata mama Tibaijuka amesema amestaafu lakini kwangu mimi hajastaafu.
Huyu Bashiru, hakuna mtu alitegemea atakuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, alikuwa muuza ndizi pale Kemondo, baadae akaenda chuo kikuu akafundisha lakini leo ndio katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Tanzania nzima, Muleba Oyee.
Serikali hii ina mavyeo mengi na ndio maana nimemwambia hata Prof. Tibaijuka, ameniambia hapa, mdogo wangu nimestaafu. Mimi nakwambia hapa, Prof. hujastaafu. Hauwezi tukamuacha Profesa akakaa tu hapa wakati kuna maeneo mengi ya kwenda kufanya.
Muachane na propaganda ambazo zinafanyika, kwamba mkituchagua sisi tutafuta kodi. Utafutaje kodi wakati kwenye mikutano yako unachangisha kodi?
Unasema utafuta kodi, ukienda kwenye mkutano, naomba mtuchangie, sasa wakiingia zile tulizozikusanya si watazitumia vibaya, zile tulizopanga kununua meli ambayo inatengenezwa pale, zitapotea.
Msichagua watu wasiomanika, msichague watu watakaokuja kutawala kwa matakwa ya watu wengine. Na si ajabu zikarudishwa hapa lockdown wakati Mungu ameshaimaliza.
Haya majamaa yamerugwa na aliyeyaroga kafa.Eti niko kwenye jalala langu!Nchi haiwezi ongozwa na watu hovyo namna hii, wenye roho za kimaskini ni,kukiri udhaifu kila wakati, mara sijui jalalani, wanyonge, etc, huu ni ushamba.
Ku renew contract sio uteuzi?Mbna anadanganya aliemteua Masilingi balozi marekani ni jk.