Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

Mgombea urais wa ccm amesema, hawezi kuongeza wafanyakazi mshahara na huku anajenga reli,elimu bure,miradi mikubwa kwa sababu na wafanyakazi watatumia hivyo vitu

Poleni wafanyakazi ,twende na Lissu

=====
View attachment 1559428
DKT MAGUFULI: MARA

> Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

> Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, ukatumia hiyo hela kupandisha mishahara

#Uchaguzi2020
Hivyo hivyo vitu mnavyopinga ndio ndio hivyo hivyo mnavifurahia kuvitumia, na mnajua ndio vitakavyo support mnavyotaka kufanya sasa , bali mnavitumia kisiasa ili mpate uongozi.
 
Na ndiyo maana hayupo mfanyakazi wa nchi hii mwenye akili zake timamu kichwani, anaweza kumfagilia huyo magufuli kwa chochote.

Kiufupi tu hana faida kwa wafanyakazi wa nchi hii. Amejawa tu na dharau, kiburi, roho mbaya na ya kikatili, ubinafsi, unafiki, ubaguzi, nk. Nachelea tu kumuombea mabaya kwa sababu na yeye ni binadamu kama mimi! ila kiukweli anatuzingua sana wafanyakazi.
Anawaonea washika chaki mbona washika smg kawaongeza mshahara.
 
ā€œMtu anakuja anasema mbona hamjapandisha mishahara?, ukishampandisha Mtu daraja mshahara wake haubadiliki?, tumerekebisha PAE kutoka 11% hadi 9%, tumelipa malimbikizo ya Wafanyakazi zaidi ya Bil 500 hiyo sio fedha!?ā€- JPM akiwa Mara
#MillardAyoUPDATES
Kiwango cha iq yako tafadhali ,maana kwa haraka haraka naona ubongo wako kama umefeli hivi
 
Mgombea urais wa ccm amesema, hawezi kuongeza wafanyakazi mshahara na huku anajenga reli,elimu bure,miradi mikubwa kwa sababu na wafanyakazi watatumia hivyo vitu

Poleni wafanyakazi ,twende na Lissu

=====
View attachment 1559428
DKT MAGUFULI: MARA

> Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

> Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, ukatumia hiyo hela kupandisha mishahara

#Uchaguzi2020
That’s a fact kutoka kwa mwanaume! Mawazo ya maendeleo. Reli ndiyo itazalisha ili kizazi cha baadaye kinufaike. Hata ulaya walifunga mikanda na leo hii wajukuu wanafaidi.
 
Huwez kuelewa ila ndo kweli
Kama baba wa familia siwezi nikaacha kufanyia biashara hella nilonayo nikaenda kuwanunulia familia yng wale kuku kila siku wale, lazima uandae ubaadae wako ata kama ni kunywa uji kila siku, enzi zile nyumban miaka ya late 90's nyumban tulikuwa tunakula mlo moja kwa siku,
Tuliishi vibaya ila ni kwakuwa wazazi walikuwa wanatafta na wakazipata, lazima uelewe unaenda wapi na msimamo wako
Kuna mschana nilikuwa nae nikamuacha bila sababu, sijui ka alikuwa ananidanganya ama ni kweli, yeye kwao kila siku ni pilau, kuku, nyama, mbuzii, birthday noma, japo alikuwa ana bonge la tako na kashiba ila familia yao ilikuwa ni kama kichu cha muhim kwao ni kula tu na hamna maendeleo
Nikamuacha maana niliona hawana akili
Hizo pilau ulikuwa unawanunulia wewe? Je walikuwa wanatoka kichakani.

Kasome kwa Maslow Hierachy of need anamaelezo kuhusu satisfaction of need kwa kila mtu.

Tuseme nchi kama nchi haina vipaumbele ila ni vipaumbele vya marais tumetoka ā€œkilimo kwanza na matokeo makubwa sasaā€ tumeenda kwa ā€œ Tanzania ya viwanda namadege na barabaraā€ zote hizi ni hulka za marais tuu.

Nimalize kwa kusema ulipo mwacha huyo demu wako unamiliki ndege yamkini yeye alikuwa kikwazo?
 
That’s a fact kutoka kwa mwanaume! Mawazo ya maendeleo. Reli ndiyo itazalisha ili kizazi cha baadaye kinufaike. Hata ulaya walifunga mikanda na leo hii wajukuu wanafaidi.
Je hilo lipo kwenye development plan ya nchi au ni matakwa ya rais na waliomzunguka kutaka namna ya kuchajachua hela maana kama ni hivyo basi Prof. Assad asngestaafishwa kwa lazima.
 
Na ndiyo maana hayupo mfanyakazi wa nchi hii mwenye akili zake timamu kichwani, anaweza kumfagilia huyo magufuli kwa chochote.

Kiufupi tu hana faida kwa wafanyakazi wa nchi hii. Amejawa tu na dharau, kiburi, roho mbaya na ya kikatili, ubinafsi, unafiki, ubaguzi, nk. Nachelea tu kumuombea mabaya kwa sababu na yeye ni binadamu kama mimi! ila kiukweli anatuzingua sana wafanyakazi.
Kwa anayofanya kufagiliwa muhimu, lakini kwa ajenda ya kupandisha mishahara na malimbikizo vita iko palepale. Tukutane 28October
 
Mgombea urais wa ccm amesema, hawezi kuongeza wafanyakazi mshahara na huku anajenga reli,elimu bure,miradi mikubwa kwa sababu na wafanyakazi watatumia hivyo vitu

Poleni wafanyakazi ,twende na Lissu

=====
View attachment 1559428
DKT MAGUFULI: MARA

> Huwezi ukaacha kujenga reli, ukasema hii hela naenda kupandisha mishahara

> Huwezi ukaacha kujenga vituo vya afya, ukatumia hiyo hela kupandisha mishahara

#Uchaguzi2020
Kasema ukweli kwa sababu akifanya hivyo bila mipango ni matokeo ya mfumuko wa being kwenye mahitaji ya Kila siku, wafanyakazi msiangalie masirahi yenu tu angalieni na masirahi ya watu wenye maisha ya kawaida.
 
Ni baba mpumbavu pekee anayeweza kuwanyima watoto wake chakula, au anayeweza kuwaambia watoto wake siwanunulii chakula kwa kuwa najenga nyumba
 
Kasema ukweli kwa sababu akifanya hivyo bila mipango ni matokeo ya mfumuko wa being kwenye mahitaji ya Kila siku, wafanyakazi msiangalie masirahi yenu tu angalieni na masirahi ya watu wenye maisha ya kawaida.
Hao watu wenye maisha ya kawaida wakipata matatizo wanawaomba wafanyakazi wawasaidie. Wala hawaendi kuomba msaada kwa SGR. Annual increment ipo kisheria na ni haki ya kila mfanyakazi. Aende akaombe kura vitu alivyojenga vimpigie kura
 
Na ndiyo maana hayupo mfanyakazi wa nchi hii mwenye akili zake timamu kichwani, anaweza kumfagilia huyo magufuli kwa chochote.

Kiufupi tu hana faida kwa wafanyakazi wa nchi hii. Amejawa tu na dharau, kiburi, roho mbaya na ya kikatili, ubinafsi, unafiki, ubaguzi, nk. Nachelea tu kumuombea mabaya kwa sababu na yeye ni binadamu kama mimi! ila kiukweli anatuzingua sana wafanyakazi.
Wafanyakazi wapo laki tano na nusu wakati jumla ya watanzania ni milioni 59.7.

Tuondokane na akili za kibinafsi, kuna mahitaji mengi sana ya watanzania wa mikoani na yana thamani kubwa na ya kudumu kulinganisha na hao waajiriwa laki tano.
 
Hao watu wenye maisha ya kawaida wakipata matatizo wanawaomba wafanyakazi wawasaidie. Wala hawaendi kuomba msaada kwa SGR. Annual increment ipo kisheria na ni haki ya kila mfanyakazi. Aende akaombe kura vitu alivyojenga vimpigie kura
Unamaanisha kuwa ukiishiwa ugali nyumbani unaenda kwa mwalimu au daktari akusaidie unga?? Niweke sawa yawezekana sijakuelewa vizuri, Suala la haki yako kisheria silipingi mkuu, Lakini sina imani kama utafurahi kuona asiye na kitu anazidi kunyimwa ili wewe uliye na kidogo uongezewe kwa kile unachokiita kuwa ni sheria, Siwezi kukuingilia kwenye maamuzi yako, lakini Kama wewe ni msomi tayari wewe ni kioo Cha jamii. Ni vizuri kufikiri sana katika kila maamuzi utakayotaka kuyachukua.
 
huyu atapata kura za wajinga,wahitimu was vyuo vikuu hawajaariwa toka 2015,ila hela za kugawa mitaani anazo
 
Kwanini hiyo kauli hakuitoa 2015 wakati akiomba kura za wafanyakazi?
Nani kamtuma kuwadhulumu wafanyakazi haki zao za msingi ikiwemo nyongeza ya mishahara?

Magufuli asituzubaishe na hadaa za maneno, toka ameingia madarakani deni la taifa limeongezeka maradufu, anakopa kila siku, hizo pesa anapekeka wapi?

Mishahara ya wafanyakazi inalipwa kisheria kutoka mkondo wake mahususi wa mapato ya serikali, na kamwe hazipaswi kuchukuliwa kufanyia mambo mengine ya maendeleo. Sasa hizi blah blah za kusema anajengea reli nani kamtuma? Nani aliidhinisha hilo? Nani anazikagua? Ipo siku tutamshtaki kwa haya madubwasha yake.
 
Haki ni pamoja na usawa, huwezi zungumzia haki wakati usawa hakuna, yani wafanyakazi wawe na mishahara mikubwa wakati wanafunzi wanakaa chini, wawe na laptop wakati hatuna maabara, mishahara yenyewe ikiwa mikubwa watashindwa kujenga na kununua magari kwasababu miundombinu ya kuendesha magari itakuwa mibovu, watashindwa kusafirisha vifaa vya ujenzi kwani gharama itakuwa kubwa sana kutokana na usafirishaji ndio maana tunajenga reli, mabwawa ya umeme n.k

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Hayo anayoyataja hayana uhusiano wowote,kupanga ni kuchagua.Mh.anataka kutuaminisha kuwa reli zilishindikana kujengwa kwa sababu ya kuajiri na kuongeza mishahara?ATC ilikosa ndege kwa sababu ya kupandisha watumishi mishahara,wanafunzi kusoma kwa ada au kutoa mikopo kwa wanavyuo?Anaposema ameongeza mishahara kwa kupunguza PAYE pia siyo kweli,hizo asilimia 9 za punguzo la PAYE ni tangia Mzee Kikwete na linawahusu kundi LA KCC ambacho ni <300,000/=.Je,hiyo PAYE ni Msahafu/Biblia kiasi cha kuing'ang'ania?Hawa watumishi wanapoenda mtaani kufanya manunuzi hulipa kodi zote kama RAIA wengine,why PAYE?Huo ni unyonyaji,mtumishi analipa kodi zaidi kuliko hata wafanyabiashara wakubwa.
Hata anayotuaminisha Mh.kuwa anayafanya siyo halisi na siyo maendeleo ya watu.Tukatae.
 
Back
Top Bottom